Ujumbe Kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji

Mwaka jana ulishuhudia utimizaji wa ahadi nyingi na kuvunjwa kwa ahadi nyingi pia. Tulishuhudia viwango vipya vya juu vya uzalishaji wa gesi ya ukaa, hali ya joto ikiyumbayumba na athari za mabadiliko ya tabianchi kushuhudiwa kwa kishindo na kwa kasi zaidi. Fedha za kusaidia jamii zilizo hatarini zaidi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hazijatolewa. Wakati uo huo, mengi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yako mbali kufikia nusu ya Ajenda ya 2030. Kuna sababu nyingi za kuwepo kwa hali hii, lakini ni wazi kwamba ushughulikiaji hafifu wa changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na uharibifu wa bayoanuai, na uchafuzi na taka ni chanzo kikuu.

Hii ndio hali hasi. Hali chanya ni kwamba juhudi za kimataifa za kushughulikia changamoto za aina tatu duniani ziliamarika. Juhudi za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira na taka zilipigwa cheki kutokana na makubaliano ya Mfumo wa Kimataifa kuhusu Kemikali na hatua zilizopigwa kwenye chombo cha kimataifa kuhusu uchafuzi wa plastiki, ambacho kinapaswa kuwa tayari kufikia mwaka 2024. Mataifa yalipitisha mkataba wa kulinda bayoanuai katika bahari nje ya mipaka ya kitaifa, huku miongozo muhimu ya kusaidia sekta ya kibinafsi kupunguza athari zake kwa mazingira ikitolewa - kupigwa cheki kwa Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal, ambao utekelezaji wake ulianza kwa kasi. Hatimaye, Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi, COP28, lilitoa wito unaoleweka wazi kwa nchi kuacha matumizi ya nishati ya visukuku - pamoja na mfumo wa Lengo la Kimataifa la Kukabiliana na Hali, kutekeleza Mfuko wa Hasara na Uharibifu, na ahadi mpya kuhusu upunguzaji wa joto kwa njia endelevu, upunguzaji wa methani, kuzidisha uzalishaji wa nishati jadidifu mara tatu na mafanikio ya kujali mazingira. 

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) lilitekeleza wajibu muhimu katika nyingi ya michakato hii – kwa kutoa sayansi muhimu na masuluhisho kuhusiana na changamoto za aina tatu duniani, kuitisha na kuwezesha mazungumzo muhimu, kuandaa mikataba muhimu ya kimataifa ya mazingira, kufanya kazi na watu binafsi na sekta za fedha ili kuoanisha ufadhili na michakato ya kimataifa na kusaidia nchi wanachama kutekeleza ahadi zao.

Hatua zinapigwa. Kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kuimarisha hatua hizi ili zisonge haraka kuliko kuongezeka kwa janga la changamoto za aina tatu duniani. Kama mamlaka kuu ya kimataifa ya mazingira, UNEP itafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwezesha hili lifanyike - kupitia kutoa teknolojia za kidijitali ili kutoa sayansi inayofaa na inayotoa mtazamo wa mambo ya mbeleni, kuimarisha utekelezaji wa makubaliano ya kimataifa ya mazingira ambayo hufanya mabadiliko yawezekane, na kuunga mkono Nchi Wanachama ili kukuza uthabiti wa tabianchi, kuishi kwa amani na mazingira na kukuza mustakabali usio na uchafuzi. Hivi ndivyo tutakavyofanikisha Ajenda ya 2030 na kuunda mazingira ya ulimwengu wenye amani na ustawi zaidi. 

Inger Andersen
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP
Endurance swimmer and UNEP Ocean Advocate Lewis Pugh
Mwogeleaji wa kustahimili na Mtetezi wa UNEP wa Bahari Lewis Pugh, anaonekana hapa wakati wa safari ya kwenda Aktiki, alisaidia kuhamasisha kuhusu vitishio kwa maji duniani. Picha: UNEP/Kelvin Trautman
Kushughulikia
Mabadiliko ya Tabianchi

UNEP iko mstari wa mbele katika juhudi za kimataifa za kusaidia nchi kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo ni mambo msingi ya SDG13 kuhusu kushughulikia mabadiliko ya tabianchi. Kazi hii pia inachangia kwa mengi ya malengo mengine ambayo yanaunga mkono afya ya binadamu na hali bora ya sayari, ustawi na usawa, ikiwa ni pamoja na kutokomeza umaskini (SDG1), kukomesha baa la njaa (SDG2), kuimarisha upatikanaji wa nishati nafuu na isiyochafua mazingira (SDG7), kupunguza ukosefu wa usawa (SDG10) na kukuza jamii endelevu (SDG11). 

UNEP/Kelvin Trautman

Ripoti ya UNEP inaonyesha kuwa pengo la uzalishaji wa hewa chafu ni mfano wa korongo kuu la uzalishaji wa hewa chafu. Korongo lililotapakaa ahadi zilizovunjwa, maisha yaliyokatizwa, na rekodi zilizovunjwa.

António Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye uzinduzi wa Ripoti ya UNEP ya Pengo la Uzalishaji wa Hewa Chafu
Kupitia takwimu
42%
ni kiasi ambacho ulimwengu unahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2030 ili kudhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 1.5.
Penguin
Huku mazingira yakiwa chini ya shinikizo linaloongezeka, UNEP inasaidia nchi kote duniani kulinda na kurejesha maeneo yake ya pori.
Kushughulikia
Mazingira

Wakati ambapo mazingira na bayoanuai vipo chini ya shinikizo kubwa, UNEP inaongoza juhudi za kulinda, kuboresha na kusimamia malighafi kwa njia endelevu. Kwa kuwa mazingira ni nguzo kwa jamii na uchumi, kazi hii inasaidia kulinda maisha chini ya maji (SDG14) na maisha juu ya ardhi (SDG15), miongoni mwa malengo mengine. Juhudi nyingi za UNEP katika mwaka wa 2023 zililenga kusaidia nchi kutekeleza Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal (GBF).

UNEP/Olle Nordell

Tukiwa na miaka saba tu ya kutekeleza (Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai) ni lazima sisi wote tuchukue hatua sasa. Na ni lazima tuendelee kuchukua hatua hadi pale ambapo mfumo wetu wa maisha utakapokuwa salama.

Inger Andersen
Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP
Kupitia takwimu
138
ni idadi ya nchi ambazo UNEP na UNDP inasaidia zinapoendeleza mikakati ya kitaifa ya kulinda bayoanuai.
Scientist
UNEP ilituza Baraza la Afrika Kusini la Utafiti wa Kisayansi na Viwanda kama Bingwa wa Dunia mwaka wa 2023, tuzo la ngazi ya juu zaidi la Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira. Matuzo ya mwaka jana yalilenga wanaosaidia kukabiliana na plastiki.
Uchafuzi
Kushughulikia

UNEP inazisaidia nchi kuachana na kemikali hatari, kudhibiti plastiki zinazotumika mara moja, kufunga mahali wazi pa kutupia takataka, kuboresha hali ya hewa na kukuza uchumi unaotumia bidhaa tena na tena. Kukabiliana na uchafuzi wa mazingira na janga la taka ni muhimu ili kuhakikisha kuna afya njema na ustawi (SDG3), kutoa maji safi na usafi wa mazingira (SDG6), kukuza miji na jamii endelevu (SDG11), kuanzisha mifumo endelevu ya uzalishaji na matumizi ya bidhaa (SDG12), na kulinda maisha chini ya maji (SDG14).

UNEP/Ihsaan Haffejee

Kila mtu kwenye sayari hii anapaswa kuweza kuishi na kufanya kazi bila woga wa kuugua au kufa kutokana na kemikali hatari.  Mfumo huu unaashiria maono ya dunia isiyo na madhara ya kemikali na taka, ili kuwa na mustakabali salama, bora na endelevu.

Inger Andersen
Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, kuhusu makubaliano ya kimataifa ya kudhibiti uchafuzi wa kemikali.
Kupitia takwimu
300M
ni idadi ya watu walioona Siku ya Mazingira Duniani kwenye mitandao ya kijamii mwaka wa 2023.
Kupunguza ukosefu wa usawa wa kijinsia

UNEP iliendelea kukuza SDG5 juu ya usawa wa kijinsia, na kuwawezesha wanawake na wasichana kuchukua nafasi za uongozi katika uhifadhi na uboreshaji wa mifumo ya ekolojia kwa kuendeleza Sera na Mikakati ya Jinsia kwa mara ya pili. Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa takriban asilimia 90 ya miradi iliyobuniwa katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2023 ilijumuisha jinsia ipasavyo kulingana na kipimo cha kina kinachotumiwa na Umoja wa Mataifa. UNEP ilizindua awamu ya pili ya mradi wa EmPower (WezEsha), ambao unasaidia wanawake nchini Bangladesh, Kambodia na Viet Nam kununua vifaa vya nishati jadidifu kwa kiwango kidogo, kama pampu za maji zinazotumia nishati ya jua. Wanawake 100,000 wanatarajiwa kufaidika na mpango huu. UNEP pia ilitekeleza wajibu muhimu nchini Kenya kwa kutoa mafunzo kwa wanawake wanaojishughulisha na uvuvi endelevu, kukuza kipato chao, na kuchangia katika uhifadhi wa rasilimali za baharini zinazodidimia. Aidha, nchini Rwanda, Togo na Uganda, UNEP na washirika wake walizindua mpango wa kutoa ruzuku kwa waanzilishi wa usafiri unaotumia umeme na kuzingatia zaidi kubuni fursa za ajira kwa wanawake. 

Picha: Unsplash/Ashwini Chaudhary

Photo: Unsplash/Ashwini Chaudhary
Kutumua teknolojia ili kuwa na dunia endelevu zaidi

UNEP iliendelea kutumia uwezo wa teknolojia kutoa masuluhisho ili kuendeleza malengo ya mazingira.  Kwa ushirikiano na Chuo cha Wafanyakazi cha Umoja wa Mataifa, Muungano wa Uendelevu wa Mazingira Kidijitali na GIZ, UNEP ilizindua mpango wa kujifunza kielektroniki, Digital4Sustainability. Ikihusisha moduli mpya ya tabianchi, jukwaa hili limevutia zaidi ya washiriki 12,000 kutoka serikalini, sekta binafsi, mashirika ya uraia na mashirika ya kimataifa. Mpango wa 10YFP ambao ni mpya unaoongozwa na UNEP wa Uwekaji wa Dijitali na Sekretarieti ili kuwa na uchumi unaotumia bidhaa tena na tena ulisaidia mashirika ya sekta ya umma na ya kibinafsi kutumia teknolojia ya kidijitali. Wakati uo huo, UNEP na washirika wake walitoa Kutafakari, Kupanua, Kutumia Upya: Kutumia Teknolojia za Kidijitali ili Kuwa na Uchumi Unaotumia Bidhaa Tena na Tena, ambayo inaonyesha jinsi bidhaa za pasipoti za kidijitali zinavyoweza kuchangia kushughulikia nyenzo mda wote zinapokuwepo.

Picha: Unsplash/Markus Spiske

Photo: Unsplash/Markus Spiske
Kusaidia mataifa na jamii zilizoathiriwa na mizozo zinapoathiriwa na majanga

Mizozo ilipozidi kuongezeka ulimwenguni, UNEP ilipata njia mpya za kusaidia jamii kudhibiti malighafi na kupunguza uharibifu wa mazingira. Kupitia Mfumo wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa, UNEP ilitoa ushauri wa kisayansi katika ngazi ya nchi. Shirika hili liliunga mkono ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, ambapo mabadiliko ya tabianchi yalichochea zaidi migogoro iliokuwepo kwa muda mrefu. Katika eneo la Asia Magharibi, UNEP ilionyesha jinsi jamii zinavyoweza kukabiliana na matukio mabaya ya hali ya hewa, hasa ukame. UNEP inazidi kutumia data ya kutambua kwa mbali na setilaiti kuelewa kuhusu uharibifu wa mazingira unaohusiwhwa na mizozo na kutoa mapendekezo ya sera.

Maoni haya yalichukuliwa kwa makini katika kutathmini kwa haraka hali ya mazingira ya uvunjaji wa Bwawa la Kakhovka la Ukraine mwezi Juni.  UNEP pia ilisaidia vikosi vya nchi za Umoja wa Mataifa nchini Syria na Türkiye kupima na kudhibiti kiasi kikubwa cha uchafu uliotokana na tetemeko la ardhi lenye uzito wa 7.8 mwezi wa Februari.

Picha: UNEP/Igor Riabchuk

Photo: UNEP/Igor Riabchuk
Ufadhili

Hali ya Kifedha ya mwaka wa 2022 na 2023 kufikia Desemba mwaka wa 2023 (Mamilioni ya Dola za Marekani)

Bajeti
Milioni
Mapato*
Milioni
Matumizi
Milioni
Bajeti ya kawaida ya UN
Mfuko wa Mazingira
Fedha Zilizotengwa**
Hazina za Kimataifa***
*
Takwimu za mapato ni za muda na zinaweza kukamilishwa na kuhitimishwa kupitia akaunti za kifedha za kila mwaka za UNEP
**
Fedha zilizotengwa ni pamoja na fedha zilizotengwa kuzingatia mada na ufadhili mwingine uliotengwa unaoweza kubadilishwa
***
Fedha za kimataifa zinawakilisha: Mfuko wa Mazingira Duniani na Mfuko wa Mazingira ya Kijani

Wachangiaji wakuu wa fedha zilizotengewa miradi maalum mwaka wa 2023 (Mamilioni ya Dola za Marekani)*

Ujerumani66.6
Taasisi za Umoja wa Mataifa36.0
Umoja wa Ulaya/Tume ya Ulaya28.2
Mpango wa Fedha wa UNEP**26.7
Wakfu/NGOs24.7
Canada11.4
Japan11.4
Uingereza ikijumuisha Uingereza Kuu na Ireland Kaskazini10.8
Marekani8.5
Uswidi7.7
Norway5.0
Ufini4.1
Ubelgiji3.8
Austria3.5
Ufaransa2.8

Wachangiaji 15 wakuu wa Mfuko wa Mazingira mwaka wa 2023 (Mamilioni ya Dola za Marekani)

Norway12.3
Uholanzi10.2
Ujerumani8.1
Marekani7.6
Ufaransa7.6
Denmark7.2
Uswidi5.1
Uingereza ikijumuisha Uingereza Kuu na Ireland Kaskazini4.5
Ubelgiji4.2
Uswisi4.0
Canada2.8
Italia2.6
Ufini2.3
Uhispania1.6
Japan1.5
*
Inajumuisha mchango unaoweza kubadilishwa matumizi kutoka kwa Ubelgiji, Ufini, Norway na Uswidi.
**
Ushirikiano kati ya UNEP na sekta ya fedha duniani wa kupata ufadhili wa sekta binafsi wa maendeleo endelevu
Jumla
48
Waliochanga kikamilifu*
32
Wachangaji wengine
113
Wasiochanga
*
Mgawo kamili wa bajeti ya Mfuko wa Mazingira kwa kuzingatia kipimo cha michango ya hiari, kilichoanzishwa na Nchi Wanachama
Waliochanga kikamilifu
  • Albania
  • Armenia
  • Barbados
  • Ubelgiji
  • Bosnia na Herzegovina
  • Bulgaria
  • Canada
  • Cyprus
  • Denmark
  • Jamhuri ya Dominika
  • Eritrea
  • Fiji
  • Ufaransa
  • Georgia
  • Guinea
  • Guyana
  • Iceland
  • Ireland
  • Jamaica
  • Jordan
  • Kenya
  • Latvia
  • Liechtenstein
  • Lithuania
  • Luxembourg
  • Maldives
  • Malta
  • Mauritius
  • Micronesia (Shirikisho la Mataifa ya)
  • Monaco
  • Montenegro
  • Moroko
  • Uholanzi
  • New Zealand
  • Norway
  • Panama
  • Peru
  • Saint Lucia
  • Serbia
  • Ushelisheli
  • Slovenia
  • Sri Lanka
  • Uswidi
  • Uswisi
  • Tajikistan
  • Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Uingereza ikijumuisha Uingereza Kuu na Ireland Kaskazini
  • Uruguay
Wachangaji wengine
  • Andorra
  • Australia
  • Austria
  • Chile
  • Uchina
  • Costa Rica
  • Croatia
  • Ufini
  • Ujerumani
  • Honduras
  • Hungari
  • India
  • Indonesia
  • Iraq
  • Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
  • Italia
  • Japan
  • Kazakhstan
  • Kuwait
  • Malaysia
  • Meksiko
  • Paraguay
  • Ufilipino
  • Ureno
  • Jamhuri ya Korea
  • Singapore
  • Slovakia
  • Afrika Kusini
  • Uhispania
  • Thailand
  • Trinidad na Tobago
  • Marekani

UNEP ingependa kushukuru Nchi Wanachama na washirika wengine wafadhili kwa michango yao katika mwaka wa 2023. Msaada huu wa kifedha ni muhimu katika kusaidia UNEP kutekeleza wajibu wake wa kukabiliana na changamoto za aina tatu duniani na kukuza mustakabali endelevu zaidi kwa wote.