20 Jan 2020

Wito wa kupendekezea UNEP washiriki wa tuzo la Mabingwa wa Dunia wa mwaka wa 2020 unaendelea

Nairobi, January 20, 2020 – Kupendekeza washiriki wa mwaka wa 2020 wa  tuzo la Mabingwa wa Dunia, tuzo la ngazi ya juu linatolewa na Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira kulianza leo na lengo la kuwatuza viongozi waliofanya juhudi za kipekee wakijumuisha viongozi wa serikali, mashirika ya uraia na sekta ya binafsi ambao juhudi zao zimeathiri mazingira kwa njia chanya . Kupendekeza huko kutaendelea hadi tarehe 20 mwezi wa Machi  mwaka wa 2020.

Tangu lilipoanzishwa katika mwaka wa 2005, watu hutuzwa kwa vitengo vinne: Uongozi unaozingatia sera ; Motisha na kuchukua hatua; Maono ya ujasiriamali, na Sayansi na ubunifu. 

“Kupitia kwa tuzo la Mabingwa wa Dunia, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linalenga kutambua mchango mkuu wa watu kutoka nyanja mbalimbali wanaofanya sayari iwe mahali pazuri pa kuishi," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Wakati ambapo watu wanaendelea kuathiri mazingira visivyo, tunajivunia watu hawa, jamii, makampuni ya biashara na serikali ambao hufanya juhudi zaidi ili kuyatunza mazingira.”

Kila mwaka, mabingwa huchaguliwa kutoka kwa mamia ya majina ya watu wanaopendekezwa kote duniani, yanayotolewa kupitia mchakato wa kupendekeza watu hadharani; orodha ya majina ya watu waliopendekezwa hukabidhiwa waamuzi- ambao hujumuisha wataalamu mbalimbali wa masuala ya mazingira- kisha ambao huchagua washindi.

Tangu kuzinduliwa kwake, UNEP imewatuza Mabingwa wa Dunia 93 ikiwa ni pamoja na viongozi duniani, watu wanaopigania maslahi ya mazingira na watu wanaobuni teknolojia.  Inajumuisha viongozi 22 duniani, watu binafsi 57 na vikundi au mashirika 14.

"Kutuzwa kama Mabingwa wa Dunia ni jambo tunalolionea fahari, na linalotutia motisha ya kuimarisha juhudi zetu za kutunza wanyama nchini Afrika Kusini," alisema  Collet Ngobeni wa Black Mambas, kikundi the kwanza kinachojumuisha wanawake wengi na kinachopigana dhidi ya uwindaji haramu kwenye mbuga ya wanyama. "Sisi wote tunaweza kuwa  Mabingwa wa Dunia kwa kutunza mazingira."

 Mabingwa wa Dunia wa mwaka wa 2019 ni: Taifa la Costa Rica, Kitengo cha Uongozi unaozingatia sera; Ant Forest, Programu ndogo kutoka Uchina yenye mradi wa upanzi wa miti, na vuguvugu la vijana la mazingira, Fridays for Future, katika kitengo cha Motisha na kuchukua hatua; Profesa Katharine Hayhoe, mwanasayansi wa mazingira kutoka katika Chuo Kikuu chaTexas Tech katika kitengo cha Sayansi na ubunifu; na Kampuni ya Patagonia ya kushona mavazi ya  kutumia mchana, katika kitengo cha Maono ya ujasiriamali.

Washindi wa mwaka huu watatuzwa kwenye sherehe itakayoandaliwa baadaye mwakani.

Pendekeza Bingwa wa Dunia

MAKALA KWA MHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni mtetezi mkuu wa masuala ya mazingira duniani.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano wa kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP, +254717080753

Related