30 Apr 2019

Kupigania Mabadiliko

Kupitia kwa ushirikiano, tunaweza kutunza mazingira. Haya ndiyo watu wa kiasili wa Kalinga nchini Ufilipino walidhibitishia ulimwengu walipoweza kukomesha Mradi wa ujenzi wa Bwawa kwa Mto Chico. Hali hii ndiyo iliyomtia motisha Joan Carling kujitolea milele kupigania haki za binadamu wakati wa kufanya maendeleo kwenye ardhi.

"Kutokana na kanuni zilezile wanazozitumia watu wa kiasili inamaanisha kuwa tunapaswa kukuza mahusianoo yetu yanayotegemeana na mazingira ambayo ndiyo chanzo chetu," anasema Carlin anayetoka katika kabila la Kankanaey nchini Ufilipino. "Uhusiano huo ndio ninaoamini kwamba unadhalalishwa kutokana na dhana ya kimagharibi ya maendeleo."

Carling, mwenye umri wa miaka 55, alianza kazi yake kama mhamasishaji zaidi ya miaka ishirini iliyopita katika eneo la Cordillera, linalopatikana kazikazini mwa Ufilipino. Eneo hilo, ambalo ni makao ya watu milioni 1.3 wa kiasili, linapatikana sehemu ya nchi iliyo na madini mengi-kuna dhahabu, shaba na manganizi.

Sheria ya Mwaka wa 1995 ya Uchimbaji wa Madini iliruhusu mashirika ya kimataifa kumiliki mashamba yote yalio na utajiri wa madini ikiwa ni pamoja na kuwa na haki miliki kwa maji yote na mbao. Pia walipewa ruhusa ya kuwatimua wanajamii kutoka kwa maeneo yaliyoidhinishwa.

image

Joan Carling. Picha kutoka maktaba ya UN

Kwa hivyo Carling, akishirikiana na wenzake kutoka Muungano wa Cordillera People's Alliance, walianza kukusanya ujumbe kuhusu athari za uchimbaji wa madini ili kupata ushahidi wa kutumiwa ili kutoa wito kwa serikali. Anasema kuwa sababu iliyofanikisha muungano wao kufaulu kukomesha baadhi ya miradi iliyokuwa imepangwa kufanywa, ni kutokana na ushahidi iliathiri mazingira asilia, kama vile kuchafua mito kwa kemikali. Baada ya wazee kutoka katika mikoa yote kutia sahihi mkataba wa umoja ambao ulipinga kuwepo kwa kampuni za kuchimba madini, gavana wa mkoa pia aliapa kuweka sera ya kutoruhusu shughuli za uchimbaji wa madini katika wilaya yake.

"Ni wazi kuwa iwapo watu waliopo nyanjani hawatachukua hatua, wanasasia hatawajibika," alisema Carling.

Carling-kama watangulizi wake wa kiasili-ametoa kauli za kupinga ujenzi wa mabwawa. Ijapokuwa anatambua kuwa watu wengi huchukulia mabwawa kama chanzo cha nishati jadidifu, anasema kuwa mbali na kuharibu ekolojia nyingi za mito kote ulimwenguni, pia yamesabasha watu kupoteza makazi yao.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na chuo kikuu cha Sussex na Shule ya Kimataifa ya Menejimenti nchini Ujerumani uligundua kuwa nchi zinazotegemea nishati ya maji sanasana kutoka kwa mabwawa ili kupata umeme yana viwango vikubwa vya umaskini, ufisadi na madeni ikilinganishwa na nchi nyinginezo.

"Ni wazi kuwa mabwawa hupendelewa kwa sababu ya faida kubwa wanayopata wajengaji wa mabwawa, fursa kubwa kwa viongozi wafisadi kunenepesha mifuko yao. Faida hiyo ndiyo inaendesha biashiara ya mabwawa, kushinda kuhitajika kwake," alisema.

image

Chimbo la Shaba Ufilipino Picha na Wikicommons

Pia, nchi nyingi zinazoendelea, huchukulia ujenzi wa mabwawa kama kitu kinacholeta maendeleo ya uchumi kwa haraka. Carling analifahamu hili, na ndiyo sababu hapingi kabisa kuwepo kwa miradi ya mabwawa, lakini "kuwe na mbinu inayozingatia haki za binadamu wakati wa maendeleo ya kuleta nishati".

"Watu wa kiasili siyo maadui. Hatupingi maendeleo," alisema. "Lakini mojawapo wa mapendekezo makubwa yalitolewa na Kamisheni ya Mabwawa Duniani ni nchi kufanya uchunguzi wa njia mbadala kwa kuzingatia kuhitajika kwa nishati. Kuna njia mbalimbali, siyo mabwawa tu."

Na hii ndiyo sababu Carling anachunguza matumizi ya mbinu zinginezo: ubia na sekta za kibinafsi. Anatumai kuwa kwa kushirikiana na wanaopigania mazingira wakati wa biashara, inaweza kusaidia kuonyesha uwezekano wa kuwa na maendeleo endelevu.

Carling aliatunukiwa tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa na Shirka la Mazingira la umoja wa Mataifa kwa mafanikio yake ya kudumu mwaka wa 2018.

Related