Picha za kabla na baada ya athari za uborejeshaji wa mifumo ya ekolojia nchini Tanzania. Kupitia uchimbaji wa mashimo nusu duara, kiwango cha maji kwenye mchanga kimeimarishwa ili kukuza tena miti na nyasi(Just Diggit: 2018-2021)
Tunahitaji kupunguza kiwango cha gesi ya ukaa kwa karibu nusu kufikia mwaka wa 2030 ili kudumisha kiwango cha joto ulimwenguni chini ya nyuzijoto 2 na kuepuka madhara yake hatari zaidi. Hatuwezi kufikia lengo hilo bila kuboresha mifumo ya ekolojia na hifadhi zake za gesi ya ukaa. Uboreshaji kabambe wa mifumo ya ekolojia na uondoaji wa gesi ya ukaa katika uchumi yanapaswa kutendeka sambamba.
Kwa kukomesha na kurekebisha uharibifu wa nchi na bahari, tunaweza kuzuia kupotea kwa viumbe milioni 1 walio katika hatari ya kutoweka. Wanasayansi wanasema kuboresha asilimia 15 tu ya mifumo ya ekolojia katika maeneo yaliyopewa kipaumbele kunaweza kupunguza kutoweka kwa asilimia 60 kupitia kuboresha makaazi.
Uboreshaji ndicho chanzo cha ufanisi na hali njema ya watu. Mifumo dhabiti ya ekolojia huzalisha faida kuanzia kwa chakula na maji hadi kwa afya na usalama ambao idadi yetu inayoongezeka inahitaji leo na itahitaji katika wakati ujao.
Ripoti mpya kutoka kwa Shirika la la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Shirika la Chakula na Kilimo yangazia udharura wa kuboresha Dunia – na faida ambazo binadamu atapata ikiwa atafanya hivyo.
Mataifa kote ulimwenguni tayari yamejitolea kuboresha karibu hekta bilioni 1 za ardhi iliyoharibiwa – eneo kubwa kuliko Uchina. Tume ya Ulaya italeta pendekezo la malengo ya kuboresha mazingira yanayoweza kutekelezwa kisheria katika mwaka wa 2021. Mikutano mikubwa ya kujadili tabianchi na bayoanuwai iliyopangwa katika mwaka wa 2021 ni fursa ya kuamsha umahiri wetu, hasa kuhusiana na bahari na maeneo ya pwani. Lakini tunachohitaji hasa ni utekelezaji, na kuandaa rasilimali zinazohitajika ili kuiwezesha.
Miaka kumi ya kuchukua hatua thabiti na wahusika wote katika jamii ina uwezo wa kuokoa siyo tu tabianchi ya Dunia na bayoanuwai inayostaajabisha, lakini inaweza kuboresha sayari yetu yenye thamani, kwa manufaa kwa watu na mazingira.
Elekeza kasa kwenye nchi kuona ahadi zilizotolewa
Chanzo: Hifadhidata ya Ahadi za Uboreshaji Ulimwenguni, PBL Shirika la Kutathmini Mazingira la Uholanzi. Ahadi kamili za taifa chini ya Mapatano ya Rio na Azimio la Bonn, zimerekebishwa kwa kuzingatia makadirio yanayopishana (PBL, 2020). Hifadhidata itasasishwa kadiri ahadi mpya zinavyoibuka.
Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia unaangazia aina nane kuu za mifumo ya ekolojia ambayo tumeharibu kabisa. Kila mmoja unaweza kuboreshwa kwa kupunguza changamoto zinaziikabili na hatua zinazoweza kuchukuliwa kuharakisha uimarishaji.
Hio inamaanisha kulinda michakato muhimu – kama vile usanidi-mwanga, kuondoa hewa ya ukaa, mzunguko wa virutubisho na usafishaji wa maji – huku tukilinda na kuboresha bayoanuwai.
Hii ni baadhi ya mifano ya mambo tunayoweza kufanya ili kkuboresha mifumo muhimu ya ekolojia. Soma yote kuhusiana na changamoto na fursa za kila mfumo wa ekolojia katika ripoti muhimu ya kisayansi: Kuwa #GenerationRestoration na Mwongozo wa Uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia.
Kuboresha mifumo mbalimbali ya ekolojia na katika viwango tofauti ulimwenguni kote kutaleta faida kubwa kwa watu na mazingira. Ni muhimu ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu kufikia mwaka wa 2030, ikijumuisha kukomesha umaskini na njaa. Soma zaidi kuhusu faida za urejeshaji katika ripoti ya muhimu: Kuwa #GenerationRestoration
Kuboresha misitu, ardhi ya mboji na mikoko, pamoja na kutumia njia nyingine za asili kama suluhisho, kunaweza kusababisha upungufu wa zaidi ya thuluthi moja ya gesi ya ukaa kunakohitajika kufikia mwaka wa 2030.
Uwezo wa mazingira unaweza kutusaidia kustahimili mabadiliko ya tabianchi. Kurejesha maeneo ya pwani yenye unyevunyevu katika Ghuba ya Pwani ya Marekani kunaweza kuokoa dola bilioni 18 zinazotumiwa kutokana na uharibifu wa dhoruba kufikia mwaka wa 2030.
Kusitisha udidimiaji wa huduma za mifumo ya ekolojia kunaweza kuzuia hasara ya dola trilioni 10 katika mapato ya ulimwengu kufikia mwaka wa 2050.
Uboreshaji kupitia upandaji wa miti katika mashamba ya kilimo kunaweza kuimarisha utoshelezaji wa chakula kwa watu bilioni 1.3.
Uboreshaji wa misitu na mbinu bora zaidi za kilimo kunaweza kupunguza uchafuzi wa vyanzo vya maji kwa asilimia 81 ya miji ulimwenguni.
Kuongeza miti katika miji kunaweza kupunguza hatari zinazotokana na uchafuzi na joto huku zikichangia hali njema ya kiakili na kimwili ya mabilioni ya watu.
Kurejesha asilimia 15 ya ardhi zilizobadilishwa matumizi yake katika maeneo yaliyopewa kipaumbele kunaweza kuzuia kutoweka kwa spishi kwa asilimia 60 kunakotarajiwa.
Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia ni fursa yetu ya kuboresha mazingira. Kwa kuhamasisha ulimwengu kuhusu uboreshaji, tunaweza kuunda upya uhusiano uliosawazika baina ya watu na mifumo ya ikolojia wanayoitegemea.
Uboreshaji unahitaji kufanyika katika kila kiwango na kila mmoja ana wajibu muhimu ya kutekeleza: kuanzia kwa mashirika ya kimataifa na serikali hadi kwa viwanda na wawekezaji hadi kwa jamii na watu binafsi.
Uborejeshaji una umuhimu mkubwa. Lakini pia ni changamoto. Mafanikio yanahitaji ujuzi, rasilimali na subira. Ndio sababu Muongo wa Umoja wa Mataifa unaandaa vifaa ili kukusaidia kujifunza kuhusu uborejeshaji wa mifumo ya ekolojia na kupata utegemezo. Tazama ripoti muhimu na upate njia yako ya kuwa #GenerationRestoration