Mifumo bora ya chakula ina athari chanya kwa mazingira asilia. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) iinashirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo FAO na Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira (WWF) kujumuisha juhudi za vijana kwa mifumo ya chakula!
Vijana ni muhimu katika kuwezesha mifumo ya chakula kuwa endelevu na ya haki kwa wote. Mawazo yao bunifu na masuluhisho ni muhimu kwa uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa bidhaa za chakula. Ongeza sauti yako ili kuleta mabadiliko.