Kutoka kwa washindi kutoka nyanjani na viongozi wa taasisi hadi kwa wanasiasa wa kipekee na taasisi za utafiti, UNEP inasherehekea Washindi wanaofanya maamuzi ya kipekee kwa manufaa ya dunia yetu.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2005, tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa na Umoja wa Mataifa ni tuzo la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira.
Kila mwaka, UNEP hutuza watu binafsi na mashirika yanayofanya kazi kupata masuluhisho bunifu na endelevu ya kushughulikia changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na bayoanuai, na kemikali, uchafuzi na taka. Mabingwa hubadilisha uchumi wetu, huvumbua, huongoza mabadiliko ya kisiasa, hupambana na ukosefu wa haki ya mazingira na kupigania malighafi zetu.
Mabingwa wa Dunia huwatuza watu katika vitengo vinne:
- Uongozi unaozingatia sera Maafisa wa sekta ya umma wanaoongoza hatua za kimataifa au kitaifa za kushughulikia mazingira. Wao huendeleza mijadiliano, kujitolea kwa dhati na kuchukua kwa manufaa ya sayari.
- Motisha na kuchukua hatua Viongozi wanaochukua hatua madhubuti zinazopelekea mabadiliko chanya ya kutunza dunia yetu. Maongozi yao ni ya kupigiwa mfano, wanatuhimiza kubadilisha mienendo yetu na kutia moyo mamilioni ya watu.
- Maono ya ujasiriamali Watu walio na maono ya kipekee yanayoenda kinyume na hali ya kawaida ya kukuza mustakabali usiochafua mazingira. Wao hukuza mifumo, kubuni teknojia mpya na kujitokeza na maono mapya ya kipekee.
- Sayansi na ubunifu Waanzilishi wanaotumia teknolojia kikamilifu kwa manufaa makuu ya mazingira. Ubunifu wao unaweza kupelekea kuwepo na siku za usoni endelevu.
Tuzo la Mabingwa wa Dunia limewatuza washindi 116, ikijumuisha viongozi duniani na watu wanaobuni teknolojia. Wanajumuisha Viongozi wa dunia 27, watu binafsi 70 na makundi au mashirika 19.