Nyoka aina ya the black mamba ina sumu mbaya zaidi katika eneo la Kusini mwa jangwa la Afrika. Ukiumwa mara moja unaweza kupoteza maisha yako ndani ya masaa machache. Pia ndilo jina linalotumiwa na kitengo cha kukabiliana na uwindaji haramu kinachojumuisha wanawake tu kinachofanya kazi katika Hifadhi ya Asili ya Balule, hifadhi ya kibinafsi katika heka 56,000 katika Mbuga ya Kitaifa ya Kruger nchini Afrika Kusini.
Jina lililochaguliwa linawakilisha "nguvu walizonazo Mamba, na madhara yanatokea kwa haraka," alisema Valeria van der Westhuizen, meneja wa mawasiliano wa kikundi cha Mamba. "Nguvu za wanawake Afrika Kusini, ni nguvu za Mamba."
Kikundi cha Black Mambas kilianzishwa mwaka wa 2013 na kinajumuisha wanawake 14, wengi wao wakitoka katika jamii ya Phalaborwa inayoishi karibu na mbuga hiyo. Kabla ya kikundi hiki kuundwa, uwindaji haramu ili kupata pembe za vifaru na nyama ya wanyama mwitu lilikuwa ni jambo la kawaida, huku wawindaji haramu- wengi wao kutoka kwa jamii ya wenyeji- walipata dola za Marekani 26,000 kwa mauzo ya pembe moja. Leitah Mkhabela, msimazi wa kikundi cha Mamba, alisema kuwa sababu iliyofanya wanajamii wanaoishi karibu na mbuga kutojitolea ilitokana na sababu kuwa hawakuhisi kuwa na uhusiano na wanyama pori. Hii ni kwa sababu wengine wao hawajawahi kuona wanyama pori. Uwindaji haramu ilikuwa njia ya kutengeneza pesa nyingi, kwa haraka.
Hii ndiyo sababu mojawapo wa kazi ya kikundu cha Mamba ni kuelimisha kuhusu umuhimu wa kuhifadhi na kukusanya taarifa kutoka kwa wenyeji kuhusu wawindaji haramu.
"Jamii inapaswa kunufaika kutokana na mbuga zilizoko karibu," alisema Mkhabela, huku akionyesha majadiliano yanayoendelea kote barani Afrika kuhusu maeneo yaliyohifadhiwa. "Iwapo mbuga za wanyama zinaweza kuzinufaisha jamii za wenyeji kwa kuzipa vyanzo vya maji safi au kutoa ufadhili kwa elimu ya ngazi za juu, tutashuhudia upunguaji wa uwindaji haramu wa vifaru na wa kupata nyama ya wanyama pori."
Kupitia Programu ya Kuelimisha kuhusu Mazingira ya Wana wa Misitu (Bush Babies Environmental Education Program), haswa kwa watoto kutoka kwa jamii zilizo karibu na mbuga ili waone wanyama. "Kuna baadhi ya watu ambao
wanaishi kilomita 10 tu kutoka kwenye mbuga, lakini hawajawahi ona kifaru, simba na tembo katika maisha yao," alisema Mkhabela.
Kando na kuelimisha jamii za wenyeji, kikundi cha the Black Mambas huchunga kilomita 126 za mpaka wa mbuga hiyo killa siku, huku wakitafuta mitego, kukagua ua unaotumia umeme, na kukagua magari. Kazi yao imepunguza uwindaji haramu katika mbuga hiyo kwa asili mia 75.
"Katika mwaka wa 2013, wakati mradi huu ulipoanzishwa, tulikuwa tunapata mitego mipya 80 iliyowekwa baada ya ukaguzi, alisema Mkhabela. "Sasa tunapokagua eneo lote tunaweza kurudi tu na mitego mitano, baadhi yake ikiwa kuukuu.
Cecilia Njenga, mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa katika eneo la Afrika Kusini alisema kuwa kikundi cha the Black Mambas kilionyesha wazi umuhimu na mafanikio ya elimu kwa wenyeji na kujitolea kwao ni muhimu kukabiliana na biashara haramu ya wanyama pori.
Kikundi cha the Black Mambas kinatoa motisha, siyo tu kwa wenyeji, bali kote ulimwenguni kwa wote wanaofanya kazi ili kukomesha janga ya biashara haramu ya wanyama pori," alisema Njenga. "Tunatambua mafanikio ya kasi na ya kupendeza walioyapata, na ushupavu unaohitajika kuyafikia.
Ijapokuwa hakuna chochote kilicho na umuhimu kuliko utunzaji wa wanyama pori, Mkhabela anasema kazi hii siyo ya kila mtu. Kutokana na mishahara duni, ya takribani dola 224 za Marekani kila mwezi, mazingira mabaya ya kufanyia kazi, na hatari ya kila mara kutoka kwa wawindaji haramu, unahitaji kuwa shupavu ili kuwa askari pori.
"Mimi huhatarisha maisha yangu kila siku, ili kuhakikisha wanyama pori wa kipekee wa Afrika Kusini wako salama," alisema Mkhabela.
Kwa mfano, katika mwaka wa 2017, Mkhabela na wenzake wawili kutoka kwa kikundi cha the Black Mambas walikuwa wanavizia wawindaji haramu katika eneo la Balule, wakati ambapo wawindaji haramu, waliokuwa wanawafuata, walipowaona kutokana na nuru ya mwezi mzima jioni hiyo. Wanawake hao-ambo hupiga doria bila kuwa na sila-walibahatika kuhepa bila majeraha baada ya kupata sehemu ya ua la mbuga iliyoharibiwa, ambayo ilikuwa imetumiwa kumwondoa tembo siku hiyo.
Ila kwa mjibu wa Mkhabela hali ya kuhatarisha maisha yao ina manufaa. Alisema kuwa kwa kuwa wao ni wanawake na kina mama, kikundi cha the Black Mambas kinaelewa ni nini maana ya ya kulea na kutunza.
"Tunastahili kuzungumza kwa niaba ya wanyama kwa sababu iwapo hatutafanya hivyo, hakuna atakayezungumza kwa niaba yao. Ni sharti tupiganie maslahi yao, kwa sababu iwapo hatutafanya hivyo, hakuna atakayepigania masilahi yao. "Tunafahamu mapenzi ni nini," alisema.