• Tuzo la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi, makundi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira.
  • Mwaka huuupendekezaji wa watu binafsi na mashirika ambayo yamesaidia kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia haswa wanahimizwa kushiriki.  
  • Upendekezaji utaanza tarehe 15 Machi hadi tarehe 11 Aprili mwaka wa 2022.

Nairobi, Machi 15 2022 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) leo limezindua wito wa kupendekeza watakaowania tuzo lake la Mabingwa wa Dunia linalotolewa kila mwaka – tuzo la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira ili kujivunia viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi kwa mchango wao chanya kwa mazingira.

Ili kuonyesha umuhimu wa kuboresha mifumo ya ekolojia, wito wa mwaka wa 2022 unahimiza upendekezaji wawatu na mashirika ambayo yamechangia  kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote duniani. Takribani mwaka mmoja tangu kuzinduliwa kwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, hakujawahi kuwa na hitaji la kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kuliko sasa. Mifumo yetu ya ekolojia ikiwa dhabiti, watu na sayari vitanawiri.

Tangu kuzinduliwa kwake katika mwaka wa 2005, tuzo hili limemulika viongozi ambao wamejitolea kufanya kazi kuhakikisha kuna sayari endelevu isiyobagua. Jumla ya washindi 106, kuanzia kwa wakuu wa nchi na wanaharakati katika jamii hadi kwa vinara wa viwanda na wanasayansi waanzilishi, wametuzwa kama Mabingwa wa Dunia

Katika mwaka wa 2021, Tuzo la Mabingwa wa Dunia lilishuhudia tena kiwango kikubwa cha watu waliopendekezwa kutoka pembe zote za dunia. Kuongezeka kwa wanaowania kwa kipindi cha miaka iliyopita kunaonyesha kuongezeka kwa idadi ya watu wanajitolea kupigania mazingira na kutambua mno umuhimu wa kazi yao. 

Washindi wa UNEP wa mwaka wa 2021 wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia walikuwa:

  • The Sea Women of Melanesia  (Papua na Visiwa vya Solomoni), wanaotuzwa katika kitengo cha Uongozi Unaozingatia Sera, hutoa mafunzo kwa wanawake kutoka eneo hilo kufuatilia na kutathmini athari za uchujukaji wa matumbawe kwenye baadhi ya miamba ya matumbawe iliyo hatarini kuangamia kwa kutumia sayansi na teknolojia ya baharini. 
  • Maria Kolesnikova (Jamhuri ya Kyrgyz), aliyetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali, ni mwanaharakati wa mazingira, mtetezi wa vijana na msimamizi wa MoveGreen, shirika linalofanya kazi kufuatilia na kuboresha hewa katika eneo la Asia ya kati.
  • Dkt. Gladys Kalema-Zikusoka (Uganda), aliyetuzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu, alikuwa daktari wa mifugo wa  kwanza kabisa wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Uganda, na ni mamlaka inayotambulika duniani inayoshughulikia wanyama wa familia ya nyani na magonjwa kutoka kwa wanyama.

Watu binafsi, mashirika ya serikali, makundi na mashirika yanaweza kuteuliwa chini ya vitengo vya Uongozi Unaozingatia Sera, Kujitolea na Kuchukua Hatua, Maono ya Ujasiriamali na Sayansi na Ubunifu.  Yeyote anaweza kutoa mapendekezo.  Tarehe ya mwisho ya kutuma mapendekezo ni Aprili 11, 2022. 

Pendekeza Bingwa wa Dunia 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Tuzo la UNEP la Mabingwa wa Dunia

Tuzo la UNEP la  Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi, makundi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira.  Tuzo linalotolewa mara moja kwa mwaka la Mabingwa wa Dunia ni tuzo la umoja wa mataifa la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira.  Hutuzwa kwa viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi.

Kuhusu Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia

Baraza la Umoja wa Mataifa limetangaza kuanzia mwaka wa 2021 hadi mwaka wa 2030 kuwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia. Muongo unaongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa na msaada kutoka kwa wabia ulibuniwa kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni.  Unalenga kuboresha mabililioni ya hekta za aridhi ya nchi kavu pamoja na mifumo ya ekolojia ya majini.  Mwito kwa jamii ya kimatifa, Muongo wa UN huleta pamoja wanasiasa, watafiti wa kisayansi, na wabia ili kuimarisha uboreshaji. 

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

UNEP@50: Ni wakati wa kutafakari kuhusu yaliyopita na kutazamia yajayo

Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira ya Binadamu mjini Stockholm, Uswidi katika mwaka wa 1972, lilikuwa kongamano la kwanza la Umoja wa Mataifa kutumia neno "mazingira" kwenye anwani yake kwa mara ya kwanza. Kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ni mojawapo wa matokeo makuu ya kongamano hili lililoanzisha mambo mengi. UNEP ilianzishwa kuwa kitengo cha kushughulikia mazingira cha Umoja wa mataifa kote ulimwenguni.  Shughuli zinazoendelea katika mwaka wa 2022 zitaangazia hatua kubwa zilizopigwa na yanayojiri katika miongo ijayo. 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa MataifaMoses Osani, Afisa wa Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

 

 

Huenda ikawa ni tumbili wa jirani aliyeshuka chini kujiunga naye alipokuwa anajifunza piano, au klabu ya wanyamapori aliyoanzisha katika shule ya msingi mjini Kampala, Uganda.  Lakini tangu akiwa mdogo sana, Dkt. Gladys Kalema-Zikusoka, Bingwa wa Dunia kwenye kitengo cha Sayansi na Ubunifu mwaka huu, alifahamu kuwa alitaka kufanya kazi na wanyama.

 "Kimsingi, wanyama kipenzi walikuwa marafiki zangu wa kwanza," alisema Kalema-Zikusoka, daktari wa wanyamapori kwa kusomea ambaye ameendelea kwa miongo mitatu kusaidia kuwalinda baadhi ya wanyama wa familia ya sokwe walioadimu zaidi duniani, ikiwa ni pamoja na sokwe wa milimani walio hatarini kuangamia.  Nyingi ya kazi yake imekuwa katika jamii maskini za Afrika Mashariki ambazo zinapakana na maeneo ya hifadhi, ambapo amesaidia kuboresha huduma za afya na kuunda fursa za kujipatia fedha, na kufanya wenyeji wengi kuwa washirika wa kuhifadhi.

"Gladys Kalema-Zikusoka ni mwanzilishi wa uhifadhi wa wanyamapori unaoongozwa na jamii," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.  "Katika sehemu nyingi, matatizo ya kifedha yanaweza kusababisha migogoro kati ya wanadamu na wanyama. Lakini kazi yake imeonyesha jinsi mizozo inavyoweza kusuluhishwa jamii za wenyeji zikichukua usukani wa kutunza mazingira na wanyamapori wanaowazunguka, na hivyo kuleta manufaa kwa viumbe vyote.”

Akiungwa mkono na familia yake, Kalema-Zikusoka alianza safari yake ya elimu ya kimataifa, alipata shahada za digrii nchini Uganda, Uingereza na Marekani. Alipofikisha miaka 20 ikianza, alirejea nchini Uganda kwa mafunzo ya kazi, ambayo hatimaye ilikuwa nguzo ya kazi yake baadaye, Mbuga ya Kitaifa ya Bwindi Impenetrable iliyoko vijinini  maeneo maskini kusini magharibi mwa nchi.

Ilikuwa mwanzo wa utalii wa sokwe huko Bwindi na Kalema-Zikusoka, ambapo wakati huo alikuwa mwanafunzi mdogo wa udaktari wa mifugo, aligundua kuwa uhifadhi haikuwa kazi rahisi. "Kulikuwa na watu waliozingatia utalii na uhifadhi katika jamii," alikumbuka. "Kulikuwa na walinzi na askaripori na Peace Corps na mahali pa wageni kulala wakati nilipoondoka huko, nilielewa jinsi utalii na uhifadhi ulivyokuwa mgumu."

Kuna ukosefu wa uwakilishi wa wenyeji miongoni mwa wahifadhi. Tunahitaji mabingwa zaidi kutoka kwa wenyeji, kwa sababu hawa ndio watakaofanya uamuzi kwa niaba ya jamii na nchi zao.

Dkt. Gladys Kalema-Zikusoka

 

Kalema-Zikusoka alikuwa daktari wa mifugo wa kwanza kabisa wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Uganda. Huko, alianza kutumia mbinu mpya ya kufanya kazi kwa wanyamapori - ambayo ilijikita katika kuboresha maisha na mapato vijijini karibu na Bwindi.

“(Hiyo inawezesha) binadamu kufurahia maisha bora na kuwa na mwelekeo chanya zaidi kuhusu uhifadhi.  Unapowaonyesha watu kwamba unawajali na kujali afya na ustawi wao, unawasaidia kuishi vyema na wanyamapori.”

Hiyo ikawa kanuni iliyoongoza shirika ambalo Kalema-Zikusoka alianzisha takribani miaka 20 iliyopita:  Conservation Through Public Health. Limepanua kielelezo chake cha afya viijijini hadi maeneo yaliyohifadhiwa karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Virunga katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pamoja na maeneo mawili yasiyohifadhiwa ya Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Elgon nchini Uganda. Mbali na kuhimiza usafi na mazoea bora ya usafi wa mazingira, kikosi hiki pia kinaunga mkono upangaji uzazi.

Kukubali kuna maingiliano kati ya wanadamu na wanyamapori, na kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyama kati ya watu na wanyama, ilikuwa muhimu kwa Kalema-Zikusoka kwani alichukua wajibu mkuu wa kutoa mwongozo kwa serikali ya Uganda jinsi ya kukabiliana na janga la COVID-19.

A woman walking in a forest
Kalema-Zikusoka alikuwa daktari wa mifugo wa kwanza kabisa wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Uganda. ​​Picha: UNEP/ Kibuuka Mukisa

Kuzuia watu kusafiri kote duniani kuliathiri sekta ya utalii kusini-magharibi mwa Uganda, na kulazimisha wengine kurudia kazi moja hatari: ujangili. Hilo lilitishia mafanikio makubwa yaliyofikiwa ya kuimarisha idadi ya sokwe wa milimani katika eneo la Bwindi, ambao idadi yao imeongezeka polepole hadi wamefikia zaidi ya 400. Hii inawakilisha karibu nusu ya idadi ya viumbe hao walio hatarini kuangamia ambao bado wanaishi porini. 

Conservation Through Public Health lilitoa mazao yanayokua haraka kwa familia, na kuwawezesha angalau kulima chakula cha kutosha kujilisha wenyewe.   Pia waliiachia jamii ujumbe muhimu.  "Tuliwaambia, lazima muendelee kulinda wanyamapori kwa sababu imewasaidia kiasi hiki.  Huu ndio mustakabali wenu.”

Mzozo kati ya watu na wanyama ni mojawapo ya vitishio vikuu kwa maisha ya muda mrefu ya baadhi ya viumbe vya kipekee zaidi duniani, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Mfuko wa Mazingira Duniani wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).  Katika nchi nyingi kama Uganda, mzozo huo, pamoja na hatari za kiafya za COVID-19 umehatarisha zaidi maisha ya viumbe vilivyo hatarini kuangamia.

Kalema-Zikusoka alifanya kazi na wafanyikazi wa mbuga za kitaifa kuhimiza wageni na askaripori kuvaa barakoa, sio tu kuzuia maambukizi ya COVID-19 kati yao wenyewe, lakini pia kutunza sokwe, ambao wanaweza kuambukizwa na vimelea vinavyoenezwa na binadamu.  Kazi hiyo inaweza kua na kuwa miongozo ya kuzuia kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyama - maambukizi ambayo hutokea kati ya wanadamu na wanyama - na mafunzo kwa wafanyakazi wa afya wa eneo hilo ili kukabiliana na COVID-19.  Sasa mataifa 21 barani Afrika - ikiwa ni pamoja na nchi 13 ambazo zina idadi ya nyani wanaopungua - zimetia saini miongozo hiyo.

"Kwa kweli tunabadilisha kielelezo cha kuzuia ugonjwa kutoka kwa wanyama ili kuzuia COVID-19 kutegemea eneo," Kalema-Zikusoka alisema.  

A young gorilla in a forest
Kwa kipindi cha miongo kadhaa iliyopita, idadi ya sokwe wa milimani katika Mbuga ya Kitaifa ya Wanyama ya Bwindi Impenetrable imeongezeka polepole hadi wamefikia zaidi ya 400. Picha: UNEP / Kibuuka Mukisa

Conservation Through Public Health lilitoa mazao yanayokua haraka kwa familia, na kuwawezesha angalau kulima chakula cha kutosha kujilisha wenyewe.   Pia waliiachia jamii ujumbe muhimu.  "Tuliwaambia, lazima muendelee kulinda wanyamapori kwa sababu imewasaidia kiasi hiki.  Huu ndio mustakabali wenu.”

Anayetambulika duniani kote kwa kazi yake, Kalema-Zikusoka, anasema kuwa anatumai atawatia moyo vijana wa Kiafrika kuchagua kazi za uhifadhi. 

"Kuna ukosefu wa uwakilishi wa wenyeji miongoni mwa wahifadhi.  Sio wengi wanatoka sehemu ambazo kuna wanyama walio hatarini kuangamia hupatikana," alisema.  "Tunahitaji mabingwa zaidi kutoka kwa wenyeji, kwa sababu hawa ndio watakaofanya uamuzi kwa niaba ya jamii na nchi zao."

 

Matuzo ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Mabingwa wa Dunia na Vijana Bingwa Duniani hutuzwa watu binafsi, makundi na mashirika ambayo juhudi zao huwa na mabadiliko chanya kwa mazingira. Tuzo linalotolewa kila mwaka la Mabingwa wa Dunia ni tuzo la ngazi la UN linalotolewa kwa heshima ya mazingira.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza miaka ya kuanzia 2021 hadi 2030 kuwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia.  Muongo unaoongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), la Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano wa wabia, unalenga kuzuia, kusitisha, na kukukabiliana na uharibifu na kudidimia kwa mifumo ya ekolojia kote duniani. Unalenga kuboresha mabilioni ya hekta ya ardhi ya nchi kavu pamoja na mifumo ya ekolojia ya majini.  Wito wa kimataifa wa kuchukua hatua, Muongo wa Umoja wa Mataifa u

Tembelea www.decadeonrestoration.org ili kujifahamisha zaisi zaidi.

 

  • Tuzo la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu zaidi mwaka huu linamtuza waziri mkuu, mwanasayansi, wanawake wa kiasili, na mjasiriamali kwa kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira.
  • Mabingwa hawa wa Dunia huhamasisha, kutetea, kuhamasisha na kuchukua hatua ili kukabiliana na changamoto kuu za mazingira za wakati wetu, ikiwa ni pamoja na kutunza na kuboresha mifumo ya ekolojia.
  • Tuzo la mwaka huu linatolewa kwa washindi katika vitengo vya Mafanikio ya Kudumu,  Motisha na Kuchukua hatua, Uongozi Unaozingatia Sera, Maono ya Ujasiriamali na Sayansi na Ubunifu.

Washindi wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia wa mwaka wa 2020 ni:

  • Waziri Mkuu Mia Mottley wa Barbados, anayetuzwa katika kitengo cha Uongozi Unaozingatia Sera kwa juhudi zake za kuhakikisha kuna dunia endelevu kwenye nchi za kipato cha chini. Mara kwa mara yeye huhamasisha kuhusu hatari inayokumba Mataifa ya Visiwa Yanayoendelea kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Waziri Mkuu huongoza juhudi za kushughulikia mazingira katika eneo lote la Amerika Kusini na Karibean - yeye ni wa kwanza kukubali kuhusu Mikakati ya Utekelezaji wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo wa Ekolojia.. Chini ya uongozi wake, Barbados imeweka malengo kabambe ya nishati jadidifu, imeahidi kuwa na sekta ya umeme na uchukuzi isiyo na mafuta ya visukuku kufikia mwaka wa 2030. Wakati uo huo, Barbados inatekeleza miradi mingi ya uhifadhi na uboreshaji wa mifumo ya ekolojia, kuanzia kwa misitu, kupitia mijini, hadi ukanda wa pwani na bahari.  Ni mwenyekiti mwenza wa One Health Global Leaders' Group on Antimicrobial Resistance.
  • The Sea Women of Melanesia (Papua na Visiwa vya Solomoni), wanaotuzwa katika kitengo cha Uongozi Unaozingatia Sera, hutoa mafunzo kwa wanawake kutoka eneo hilo kufuatilia na kutathmini athari za uchujukaji wa matumbawe kwenye baadhi ya miamba ya matumbawe iliyo hatarini kuangamia kwa kutumia sayansi na teknolojia ya baharini.
  • Dkt. Gladys Kalema-Zikusoka (Uganda), anayetuzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu, alikuwa daktari wa mifugo wa  kwanza kabisa  wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Uganda, na ni mamlaka inayotambulika duniani inayoshughulikia wanyama wa familia ya nyani na magonjwa kutoka kwa wanyama. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Conservation Through Public Health (CTPH), anasimamia utekelezaji wa programu tatu zilizounganishwa kimkakati kwa kutumia mbinu ya ‘Afya Moja’.
  • Maria Kolesnikova (Jamhuri ya Kyrgyz), aliyetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali, ni mwanaharakati wa mazingira, mtetezi wa vijana na msimamizi wa MoveGreen, shirika linalofanya kazi kufuatilia na kuboresha hewa katika eneo la Asia ya kati. Chini ya Kolesnikova, MoveGreen ilitengeneza apu ijulikanayo kama AQ.kg, ambayo hukusanya data kila baada ya saa moja hadi tatu kutoka majiji makubwa zaidi ya Kyrgyz, Bishkek na Osh, kuhusu kiwango cha vichafuzi hewani, ikiwa ni pamoja na PM 2.5, PM 10 na dioksidi ya nitrojeni.

Kwa kuhamasisha kuhusu kazi muhimu inayofanywa na wanaharakati wa mazingira, tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa kutoa motisha kwa watu zaidi kukabiliana na changamoto tatu duniani- mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira, wa bayoanuai na uchafuzi, kemikali na taka.

Matuzo ya mwaka huu yanaangaziaMuongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha ya Mfumo wa Ekolojia, ambao unaendelea hadi 2030, unaingiliana na makataa ya kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Kwa kusitisha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia ya nchi kavu na majini, tunaweza kuzuia uharibifu wa viumbe milioni moja vilivyo hatarini kutoweka. Wanasayansi wanasema kuboresha asilimia 15 tu ya mifumo ya ekolojia katika maeneo yanayohitaji kushughulikiwa kwa dharura na kwa hivyo kuboresha makazi kunaweza kupunguza kuangamia kwa asilimia 60. 

Hakujawa na hitaji la dharura zaidi la kuboresha mifumo ya ekolojia iliyoharibiwa kuliko sasa.  Mifumo ya ekolojia inawezesha maisha ya viumbe wote Duniani.  Mifumo yetu ya ekolojia ikiwa dhabiti, sayari yetu itakuwa dhabiti na watu watakuwa na afya njema. Uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia utafaulu tu iwapo kila mtu atajiunga na vuguvugu la #GenerationRestoration ili kuzuia, kukomesha na kukabilina na uharibifu wa mifumo ekolojia kote duniani.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu  Tuzo la UNEP la Mabingwa wa Dunia Tuzo la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi, makundi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. Tuzo linalotolewa mara moja kwa mwaka la Mabingwa wa Dunia ni tuzo la umoja wa mataifa la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira.  Hutuzwa kwa viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi.

Kuhusu Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia Baraza la Umoja wa Mataifa lilitangaza kuanzia mwaka wa 2021 hadi mwaka wa 2030 kuwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia. Muongo unaongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa na msaada kutoka kwa wabia ulibuniwa kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni. Unalenga kuboresha mabililioni ya hekta za aridhi ya nchi kavu pamoja na mifumo ya ekolojia ya majini. Mwito kwa jamii ya kimatifa, the Muongo wa UN huungwa mkono na wanasiasa, utafiti wa kisayansi, na ufadhili ili kuimarisha uboreshaji.

UNEP@50: Ni wakati wa kutafakari kuhusu yaliyopita na kutazamia yajayo Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira ya Binadamu mjini Stockholm, Uswidi katika mwaka wa 1972, ulikuwa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kutumia neno "mazingira" kwenye anwani yake kwa mara ya kwanza. Kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ni mojawapo wa matokeo makuu ya kongamano hili lilianzisha mambo mengi. UNEP ilianzishwa kuwa kitengo cha kushughulikia mazingira cha Umoja wa mataifa kote ulimwenguni. Shughuli zitakazoendelea katika mwaka wa 2022 zitaangazia hatua zilizopigwa na yatakayojiri katika miongo ijayo.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.  

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:Moses Osani,, Afisa wa Mawasiliano, UNEP

  • Tuzo la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) la Mabingwa wa Dunia hutolewa kwa watu binafsi, makundi ya watu na mashirika ambayo matendo yao yameleta mabadiliko chanya kwa mazingira.
  • Mapendekezo ya watakaowania mwaka huu yanakubaliwa tangu tarehe 28 Januari hadi tarehe 12 Februari 2021.

Nairobi, Januari 28, 2021 – Umoja wa Mataifa (UN) leo ulitoa wito wa kupendekeza majina ya watakaoshiriki katika tuzo lake la Mabingwa wa Dunia  – tuzo la ngazi ya juu linalotolewa kwa watu binafsi na mashirika yanayotunza mazingira yetu na kuleta mabadiliko katika jamii.

Wito wa kupendekeza watakaoshiriki umetolewa mwezi mmoja baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kutoa onyo kuwa binadamu wametangaza vita dhidi ya mazingira kupitia uharibifu wa bayoanuai, kudidimia kwa mifumo ya ekolojia, uchafuzi wa hewa na maji, hali inayopelekea vifo vya mamilioni ya watu na hali ya mabadiliko ya tabianchi inayozidi kuwa mbaya kutokana na mioto na mafuriko.

Kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita, tuzo la Mabingwa wa Dunia limekuwa likiangazia kazi inayofanywa na watu binafsi na mashirika ambayo yamejitolea kufanya kazi ili kuboresha sayari ili kutokuwa na ubaguzi na kuifanya kuwa endelevu. Washindi wameshirikisha wakuu wa nchi, wahamasishaji katika jamii, wakuu wa kampuni na wanasayansi waanzilishi.

Idadi kubwa ya watu ilipendekezwa katika mwaka wa 2020 kuliko mwaka mwingine wowote; hii ni idhibati ya kuongezeka kwa watu wanaojitolea kushughulikia mazingira. Washindi wa tuzo la Mabingwa wa Dunia 2020 ni:

  • Waziri Mkuu Frank Bainimarama kutoka Fiji, aliyetuzwa katika kitengo cha Uongozi Unaozingatia Sera kwa juhudi zake za kimataifa za kushughulikia mazingira na kujitolea kwake kuweka mikakati ya kitaifa ya kushughulikia mazingira
  • Dkt. Fabian Leendertz (Ujerumani), alituzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu kutokana na uvumbuzi wake kuhusiana na magonjwa kutoka kwa wanyama na kazi yake kwenye One Health
  • Mindy Lubber (Marekani), alituzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali kwa kujitolea kwake kuhimiza wawekezaji kuwekeza kwenye kampuni zisizochafua mazingira na kuwajibisha mashirika ya biashara kushughulikia mazingira na kuwa endelevu
  • Nemonte Nenquimo (Ecuador), alituzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua kwa kuwa mstari mbele kushirikiana na jamii za kiasili, hali iliyowezesha kusitisha uchimbaji wa visima kwenye misitu ya Amazon nchini Ecuador
  • Yacouba Sawadogo (Burkina Faso), aliyetuzwa pia katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua kwa kuwafundisha wakulima njia zake za kiasili zinazojali mazingira za kuboresha mchanga wao na kuwezesha ardhi yao mbovu kutumika kwa kilimo na kupanda misitu barani Afrika

Washindi wa mwaka huu wanashirikisha Professor Robert D. Bullard (Marekani) aliyetuzwa tuzo la Mabingwa wa Dunia katika kitengo cha Mafanikio ya Kudumu kwa kujitolea kwake kuhakikisha kuwa mazingira yanafanyiwa haki.

Yeyote anaweza kupendekeza, awe mtu binafsi, taasisi za serikali, kampuni au mashirika. Makataa ya kupendekeza ni Februari 12, 2021.

Pendekeza Bingwa wa Dunia hapa.

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP, +254717080753

 

 

  • Tuzo la Vijana Bingwa Duniani hutolewa kila mwaka kwa wajasiriamali saba walio na umri usiozidi miaka 30 walio na maono dhabiti ya kusababisha mabadiliko ya kudumu kwa mazingira.
  • Washindi saba, kutoka katika maeneo mbalimbali kote ulimwenguni, hupokea hisa zisizo na riba ya kudumu, ushauri na msaada wa mawasiliano ili kuimarisha juhudi zao.

Nairobi, Disemba 15, 2020 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) leo lilitangaza vijana saba ambao ni wanasayansi, wahandisi, wajasiriamali na wanaharakati kutoka pembe zote za dunia kama washindi wa mwaka wa 2020 wa tuzo la Vijana Bingwa Duniani.

Wakitoa masuluhisho ya jinsi ya kupata maji kutoka kwa hewa, kuunda vibamba kutoka kwa plastiki, na kushawishi wavuvi kuondoa matani ya plastiki kutoka baharini, watu hawa wanaosababisha mabadiliko wanaonyesha jinsi ambavyo maono ya uvumbuzi yakijumuisha juhudi za kipekee yanavyoweza kukabiliana na baadhi ya changamoto kuu zinazokumba mazingira.

"Kote duniani, vijana wako mstari mbele kutoa wito wa kutoa suluhu ya kipekee kwa dharura kwa aina tatu ya changamoto zinazokumba dunia; mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi  –tunapaswa kuwasikiliza," alisema Inger Andersen, Katibu mtendaji wa UNEP. "Tunapoingia katika muongo tunaopaswa kuchukua hatua za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na kutunza na kuboresha mifumo ya ekolojia, Washindi wa Tuzo la Vijana Bingwa Duniani ni ishara tosha kuwa sisi sote tunaweza kutoa mchango wetu kwa kuanzia tuliko na kwa kutumia kile tulicho nacho. Juhudi zozote tunazochukua kwa naiaba ya mazingira ni muhimu, na kila mtu kote duniani anapaswa kuwajibika na kutumia fursa iliopo.  

Washindi saba, wote wakiwa na umri usiozidi miaka 30, walichaguliwa na wataalamu ambao ni waamuzi wa kimataifa baada ya kupendekezwa na umma. Washindi wa mwaka wa 2020 wa Tuzo la Vijana Bingwa Duniani ni:

  • Afrika: Nzambi Matee (Mkenya mwenye umri wa miaka 29), mhandisi wa vifaa na msimamizi wa kampuni ya Gjenge Makers, inayounda vifaa endelevu vya kujengea kwa bei nafuu kutoka kwa plastiki iliyotumika na mchanga.
  • a and the Pacific: Xiaoyuan Ren (China, 29) leads MyH2O, a data platform that tests and records the quality of groundwater across a thousand villages in rural China into an app so residents know where to find clean water. The platform also educates communities about sources of contamination and connects villages with potable water companies.Asi
  • Asia na Pasifiki: Vidyut Mohan (Mhindi mwenye umri wa miaka 29) alishirikiana na wenzake kuanzisha Takachar, kampuni inayotengeneza mitambo  inayoweza kuhamishwa ya kuboresha bayomasi, hali inayowezesha wakulima kujipatia pesa zaidi na kuzuia uchomaji wa taka katika maeneo wazi kwa kuunda nishati, mbolea kaboni hai kutoka taka ya mimea.
  • Ulaya: Lefteris Arapakis (Mgiriki mwenye umri wa miaka 26) alianzisha kampuni ta Enaleia, ambayo kikosi chake hutoa mafunzo, kujengea uwezo na kutuza wavuvi kutoka kwa jamii ya wenyeji ili wakusanye taka kutoka baharini, hali inayopelekea ongezeko la idadi ya samaki na uboreshaji wa mifumo ya ekolojia. Kampuni ya Enaleia hutumika kama kielelezo za kutengenezea bidhaa za mtindo wa kisasa kama vile soksi na mavazi ya kuogelea kutoka kwa plastiki.
  • Amerika ya Latini na Karebian: Max Hidalgo Quinto (kutoka Peru, mwenye umri wa miaka 30) alianzisha Yawa, kampuni inayotengeneza mitambo ya upepo inayoweza kuhamishwa inayowezesha kupata maji lita 300 kutoka kwa unyevunyevu na ukungu.
  • Amerika Kaskazini   Niria Alicia Garcia (Mmarekani  mwenye umri wa miaka 28), hushirikiana na wanaharakati kutoka katika jamii za kiasili kuratibu- shughuli ya Run 4 Salmon akitumia mtandao ili kuelimisha watu kuhusu historia ya samoni wa chinook katika mji wa Sacramento unaopatikana katika jimbo la California eneo lililio na maji mengi, na kuhamasisha watu kuhusu mfumo huu muhimu wa ekolojia, spishi zake na watu wanaonufaika.
  • Asia Magharibi: Fatemah Alzelzela (kutoka Kuwait, mwenye umri wa miaka 24) alianzisha Eco Star, mradi wa shirika lisilokuwa la biashara ambalo huchukua taka na kutoa miti kwa majumba, shule na mashirika ya biashara nchini Kuwait. Tangu kuzinduliwa kwake mwaka wa 2019, shirika la Eco Star limetumia taka ya vyuma, ya makaratasi na ya plastiki tani 130 kuundia bidhaa.

Tangazo la washindi wa Tuzo la Vijana Bingwa Duniani limetokea baada ya kutangazwa kulikotokea siku ya ijumaa kwa washindi sita wa tuzo la Mabingwa wa Dunia, tuzo la ngazi ya juu  linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira. Viongozi wa kipekee ambao juhudi zao zimesababisha mabadiliko chanya kwa mazingira hutuzwa.

Kwa kuhamasisha kuhusu kazi muhimu inayofanywa na wanaharakati wa mazingira, Tuzo la Vijana Bingwa Duniani- sehemu ya kampeni ya UNEP ya #ForNature (#TutunzeMazingira) linalenga kutoa motisha kwa watu zaidi na kuchombea vijana zaidi kuchukua hatua za kushughulikia mazingira tunapoelekea  Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Oboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia (2021-2030), Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai (COP 15) lilitakalofanyika mjini Kunming mwezi wa Mei mwaka wa 2021, na Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) mjini Glasgow katika mwezi wa Novemba mwaka wa 2021.   

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kuhusu Vijana Bingwa Duniani

Tuzo la Vijana Bingwa Duniani ni mradi mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa wa kushirikisha vijana kwenye utatuaji wa changamoto kuu zinazokumba mazingira. Washindi saba walitangazwa katika mwezi wa Disemba mwaka wa 2020. Washindi hupokea msaada wa kifedha na ushauri ili kufanikisha miradi yao inayohusiana na mazingira. Tangu kuanzishwa kwake katika mwaka wa 2017, wanamazingira wa kipekee 28 kutoka pembe zote za dunia wametuzwa.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP

 

Karakana ndogo ya Nzambi Matee mjini Nairobi nchini Kenya imejazwa mabomba ya chuma na vyuma kutoka kwa mashine. 

Wasioelewa wanaweza kustaajabu ila kwa kwa Matee, mwenye umri wa miaka 29, mvumbuzi na mjasiriamali, vitu hivyo viko salama hapo. Hapa ndiko alikotengeneza kielelezo cha mashine kinachobadili plastiki iliyotupwa kuwa mawe ya kujengea njia ya wapitao kwa miguu - uvumbuzi mkuu wa kampuni yake, Gjenge Makers.

Kila siku, kampuni hiyo hutengeneza vibamba 1,500 vya plastiki, vinavyonunuliwa na shule na wamiliki wa majumba kwa sababu vinadumu na vinapatikana kwa bei nafuu. Kampuni ya Gjenge Makers inafanya chupa na vyombo vingine vya plastiki kuweza kutumika tena na kutoingia ardhini, au hata kusambaa kwenye barabara kuu mjini Nairobi. 

"Ni jambo la kushangaza kuwa bado tunakumbwa na tatizo la kupata makazi mazuri - yanayohitajika mno kwa binadamu," alisema Matee. "Plastiki hutumiwa vibaya na wengi hawajaielewa. Ni muhimu mno, lakini ikishamaliza kutumika inaweza kuwa hatari mno kwa maisha.

Kampuni ya kutengeneza vibamba ya Gjenge imeithinishwa na Shirika la Kutathmini Ubora wa Bidhaa nchini Kenya. Huyeyuka kwa kiwango cha joto zaidi ya nyuzijoto 350, na ni dhabiti ikilinganishwa na matofali. 

Kutokana na kazi yake, hivi karibuni Matee alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo la Vijana Bingwa Duniani linalotolewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). Tuzo hilo hutoa ufadhili ili kupata hisa kwa kampuni na ushauri kwa vijana wanaharakati wa mazingira wanapoendelea kukabiliana na changamoto kuu zinazoikumba dunia.

"Ni sharti tutafakari jinsi tunavyozalisha viwandani na jinsi tunavyofanya bidhaa tunapomaliza kuzitumia," alisema Soraya Smaoun, mtalamu wa UNEP kuhusiana na mbinu za uzalishaji.  "Uvumbuzi wa Nzambi Matee kwenye sekta ya ujenzi inaoyesha fursa zilizopo kwa uchumi na kwa mazingira tutakapoacha tu kutumia bidhaa mara moja na kuzitupa na kufanya bidhaa kuendelea kutumika kwa kipindi kirefu iwezekanavyo."  

Maafa makubwa kutokana na plastiki

Plastiki inapatikana kote ulimwenguni. Kote ulimwenguni, chupa za maji ya kununuliwa milioni 1 hununuliwa kila dakikatrilioni 5 za mifuko ya plastiki inayotumiwa mara moja tu hutumika kwa mwaka. 

Matee, aliyosomea taaluma kuu ya sayansi ya vifaa na aliyefanya kazi kama mhandisi katika sekta ya mafuta nchini Kenya, alishawishika kuzindua kampuni yake baada ya kukutana mara kwa mara na plastiki kwenye barabara kuu nchini Nairobi. 

Katika mwaka wa 2017, Matee alijiuzulu kama mchanganuzi wa data na akafungua maabara ndogo nyumbani kwa mamake. Hapo, alianza kuunda na kufanyia majaribio vibamba vinavyotengenezwa kwa kuchanganya plastiki na mchanga. Majirani walilalamika kuhusu kelele kutoka kwa mashine alizokuwa anatumia, na kwa hivyo Matee akawaomba wavumilie kwa kipindi cha mwaka mmoja ili akaelewe kiiwango cha kuchanganya wakati wa kuchanganya matofali ya kujengea maeneo ya waotumia miguu. 

"Sikutangamana na watu kwa kipindi cha mwaka mmoja, na nikatumia hela zote nilizokuwa nikiweka kufanya kazi hii," alisema. "Rafiki zangu waliingiwa na wasiwasi."

Kwa kujaribujaribu, yeye na wenzake waligundua kuwa baadhi ya plastiki ilishikana vizuri kuliko ingine. Mradi wake ulipigwa jeki wakati Matee alipopata ufadhili kushiriki programu inayotoa mafunzo kwa wajasiriamali katika jamii nchini Marekani. Huku akiwa amebeba baadhi ya vabamba vyake aliposaafiri, alitumia maabara ya vifaa katika Chuo Kikuu cha Colorado Boulder kufanyia majaribio zaidi na kuboresha viwango vya mchanganyiko wa mchanga na plastiki. 

Matee pia alitumia fursa hii kuunda mashine ambayo angetumia kutengeneza matofali yale. "Pindi tunapofahamu kutengeneza kibamba kimoja, tunahitaji maarifa ya kutengeneza vibamba 1000," alieleza. 

Nzambi Matee is a 2020 Young Champion of the Earth winner with one of her pavers
Nzambi Matee is a materials engineer and head of Gjenge Makers, which produces sustainable low-cost construction materials made of recycled plastic waste and sand. Photo: UNEP

Kukamilisha kazi

Matee anakumbuka siku aliyofaulu kutengeneza kikamilifu vibamba kutoka kwa plastiki. "Ni siku ambayo sitawahi kuisahau!" alimaka. "Ni baada ya kujaribu kwa kipindi cha miaka mitatu. Niliacha kazi yangu. Nikatumia hela zote nilizokuwa nimehifadhi. Nilipungukiwa na pesa kiasi kwamba kila mtu alidhani kuwa nilikuwa nimepagawa na kwa hivyo wengi wao wakanishauri niachane na kazi hii."

Mojawapo ya shule zinazotumia vibamba ni Kituo cha Mafunzo ya Ufundi cha Mukuru (Mukuru Skills Training Centre) kinachopatikana kwenye kitongoji duni cha Mukuru Kyaba. Maeneo yake ya watoto kuchezea na njia zinazopatikana kati ya darasa moja na lingine yamewekwa vibamba maridadi vilivyotengenezwa na Matee. (Kabla ya kuwekwa vibamba, wanafunzi walitembea kwenye njia zilizokuwa na vumbi.)

"Tuna nia ya kuweka vibamba kila mahali shuleni," alisema mratibu wa programu, Anne Muthoni. "Si ghali na tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Nzambi. Vijana wanapaswa kutiwa motisha na kuhamasishwa kuhusu jinsi ya kutunza mazingira, huku wakijitengenezea pesa.

Matee huhimiza vijana kukabiliana na changamoto za mazingira kwenye maeneo wanayotoka. "Athari ghasi tunayosababisha kwa mazingira ni kubwa," alisema Matee. "Ni wajibu wetu kuboresha hali iliopo. Anza na suhuhu yoyote inayopatikana mahali ulipo na uendelee pasipo kuchoka. Utafurahia matunda yake." 

Tuzo la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa la Mabingwa wa Dunia na lile la  Vijana Bingwa Duniani hutolewa kwa watu binafsi, makundi na mashirika ambayo juhudi zao zimesababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. 

Tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa na Umoja wa Mataifa ni tuzo la ngazi ya juu linalolenga kuwashirikisha vijana kwenye utatuzi wa changamoto kuu zinazokumba mazingira. Nzambi Matee ni mmoja wa washindi saba waliotangazwa mwezi wa Disemba mwaka wa 2020, tunapoelekea Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, 2021-2030. 

Kwa kuhamasisha kuhusu kazi muhimu inayofanywa na wanaharakati wa mazingira, tuzo la Mabingwa wa Dunia linatolewa ili kutoa motisha kwa watu zaidi na kuchombea watu zaidi kuchukua hatua za kushughulikia mazingira.  Matuzo haya ni  sehemu ya kampeni ya UNEP ya #ForNature (#TutunzeMazingira) kuongezea uzito Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanua (COP 15) ilitakalofanyika mjini Kunming mwezi wa Mei mwaka wa 2021, na kuimarisha juhudi za kushughulikia mazingira tunapoekea kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi  (COP26) mjini Glasgow katika mwezi wa Novemba mwaka wa 2021.    

  • Tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa na Umoja wa Mataifa ni tuzo la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira. Viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi hutuzwa kila mwaka. 
  • Mabingwa wa Dunia hutia moyo, hupigania, huhamasisha na kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikumba dunia kwa sasa.
  • Tuzo la mwaka huu linatolewa kwa washindi katika vitengo vya Mafanikio ya Kudumu,  Motisha na Kuchukua hatua, Uongozi Unaozingatia Sera, Maono ya Ujasiriamali na Sayansi na Ubunifu.

Nairobi, Disemba 11, 2020 - Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) leo lilitangaza washindi sita wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia la mwaka wa 2020, tuzo la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira. Washindi walichaguliwa kutokana na mchango wao ulioleta mabadiliko kwa mazingira na kuwa mstari mbele kushawishi watu kuchukua hatua dhabiti kwa niaba ya sayari na wanaoishi ndani yake.

Tangu kuzinduliwa kwake katika mwaka wa 2005,  tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa kila mwaka, limetoa umaarufu na kusifia watu walio mstari mbele kupigania mazingira: ikijumuisha wanasayansi chupukizi, viongozi wa kampuni, wakuu wa nchi na mahamasishaji katika jamii.  Tuzo hili husherehekea watu wanaohimiza na wanaoweza kuigwa wanaonyesha kuwa juhudi za mtu mmoja au za kundi la watu zinaweza kuleta mabadiliko duniani.

Akiwapongeza washindi wa mwaka huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema:Wakati wa ugonjwa mtandavu kote ulimwenguni, chumi ziliporomoka na kuzidisha changamoto kwa mazingira, sasa, kuliko kipindi kingine chochote, tunahitaji kuchukua hatua dhabiti kwa dharura ili kuboresha uhusiano wetu na mazingira. Washindi wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia hututia moyo. Wao hutushawishi kutafakari zaidi, kufanyia kazi mawazo yetu kwa kuchukua hatua dhabiti, na kushirikiana kujenga mustakabali mwema."

"Washindi wa mwaka huu wamejizatiti, wamekabiliana na changamoto na kuamua kujitolea kutunza na kuboresha mazingira," alisema Katibu Mkuu Mtendaji wa UNEP Inger Andersen. Mbali na kutia moyo, wao hutukumbusha kuwa suluhu iko mikononi mwetu, na tuna maarifa na teknolojia ya kudhibiti mabadiliko ya tabianchi na kuzuia mifumo ya ekolojia kusambaratika. Ni wakati wa kushughulikia mazingira."

Washindi wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia wa mwaka wa 2020 kwa kuzingatia alfabeti ni:

  • Waziri Mkuu Frank Bainimarama kutoka Fiji, aliyetuzwa katika kitengo cha Uongozi Unaozingatia Sera kwa juhudi zake za kimataifa za kushughulikia mazingira na kujitolea kwake kuweka mikakati ya kitaifa ya kushughulikia mazingira
  • Dr. Fabian Leendertz (Ujerumani), alituzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu kutokana na uvumbuzi wake kuhusiana na magonjwa kutoka kwa wanyama na kazi yake kwenye One Health
  • Mindy Lubber (Marekani), aliyetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali kwa kujitolea kwake kuhimiza wawekezaji kuwekeza kwenye kampuni zisizochafua mazingira na kuwajibisha mashirika ya biashara kushughulikia mazingira na kuwa endelevu
  • Nemonte Nenquimo (Ecuador), aliyetuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua kwa kuwa mstari mbele kushirikiana na jamii za kiasili hali iliyowezesha kusitisha uchimbaji visima kwenye misitu ya Amazon
  • Yacouba Sawadogo (Burkina Faso), aaliyetuzwa pia katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua kwa kuwafundisha wakulima njia zake za kiasili zinazojali mazingira za kuboresha mchanga wao na kuwezesha ardhi yao mbovu kutumika kwa kilimo na kupanda misitu barani Afrika

Washindi wa mwaka huu wanashirikisha Profesa Robert D. Bullard (USA) aliyetuzwa katika kitengo cha Mafanikio ya Kudumu kwa kujitolea kwake kuhakikisha kuwa mazingira yanafanyiwa haki.

Kwa kuhamasisha kuhusu kazi muhimu inayofanywa na wanaharakati wa mazingira, tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa kutoa motisha kwa watu zaidi na kuchombea watu zaidi kuchukua hatua za kushughulikia mazingira. Kutokana na janga la COVID-19, kutangazwa kwa washindi wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia kulifanyika mtandaoni, tunapoelekea Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, utakaoanza mwanzoni mwa mwaka wa 2021. Kama sehemu ya kampeni ya UNEP’ ya #ForNature (#TutunzeMazingira) kuongezea uzito Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai (COP 15) litakalofanyika mjini Kunming mwezi wa Mei mwaka wa 2021, na kuimarisha juhudi za kushughulikia tunapoekea kongamano la a Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) mjini Glasgow katika mwezi wa Novemba mwaka wa 2021.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. 

Kuhusu Mabingwa wa Dunia

Mabingwa wa Dunia  hutuza viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi.Tangu kuzinduliwa kwake katika mwaka wa 2005, Tuzo la Mabingwa wa Dunia  limewatuza washindi 95, ikijumuisha viongozi 24, watu binafsi 57 na mashirika 12. Waliowahi kushinda ni rais mstaafu wa Chile Michelle Bachelet, vuguvugu la vijana wanaokabiliana na mabadiliko ya tabianchi la Fridays for the Future, Mtaalamu wa masuala ya Bahari Sylvia Earle, Mmarekani aliyehudumu kwenye serikali Al Gore, Jumuia ya Kitaifa ya Jiografia, na wengineo. 

 

 

Nairobi, January 20, 2020 – Kupendekeza washiriki wa mwaka wa 2020 wa  tuzo la Mabingwa wa Dunia, tuzo la ngazi ya juu linatolewa na Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira kulianza leo na lengo la kuwatuza viongozi waliofanya juhudi za kipekee wakijumuisha viongozi wa serikali, mashirika ya uraia na sekta ya binafsi ambao juhudi zao zimeathiri mazingira kwa njia chanya . Kupendekeza huko kutaendelea hadi tarehe 20 mwezi wa Machi  mwaka wa 2020.

Tangu lilipoanzishwa katika mwaka wa 2005, watu hutuzwa kwa vitengo vinne: Uongozi unaozingatia sera ; Motisha na kuchukua hatua; Maono ya ujasiriamali, na Sayansi na ubunifu. 

“Kupitia kwa tuzo la Mabingwa wa Dunia, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linalenga kutambua mchango mkuu wa watu kutoka nyanja mbalimbali wanaofanya sayari iwe mahali pazuri pa kuishi," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Wakati ambapo watu wanaendelea kuathiri mazingira visivyo, tunajivunia watu hawa, jamii, makampuni ya biashara na serikali ambao hufanya juhudi zaidi ili kuyatunza mazingira.”

Kila mwaka, mabingwa huchaguliwa kutoka kwa mamia ya majina ya watu wanaopendekezwa kote duniani, yanayotolewa kupitia mchakato wa kupendekeza watu hadharani; orodha ya majina ya watu waliopendekezwa hukabidhiwa waamuzi- ambao hujumuisha wataalamu mbalimbali wa masuala ya mazingira- kisha ambao huchagua washindi.

Tangu kuzinduliwa kwake, UNEP imewatuza Mabingwa wa Dunia 93 ikiwa ni pamoja na viongozi duniani, watu wanaopigania maslahi ya mazingira na watu wanaobuni teknolojia.  Inajumuisha viongozi 22 duniani, watu binafsi 57 na vikundi au mashirika 14.

"Kutuzwa kama Mabingwa wa Dunia ni jambo tunalolionea fahari, na linalotutia motisha ya kuimarisha juhudi zetu za kutunza wanyama nchini Afrika Kusini," alisema  Collet Ngobeni wa Black Mambas, kikundi the kwanza kinachojumuisha wanawake wengi na kinachopigana dhidi ya uwindaji haramu kwenye mbuga ya wanyama. "Sisi wote tunaweza kuwa  Mabingwa wa Dunia kwa kutunza mazingira."

 Mabingwa wa Dunia wa mwaka wa 2019 ni: Taifa la Costa Rica, Kitengo cha Uongozi unaozingatia sera; Ant Forest, Programu ndogo kutoka Uchina yenye mradi wa upanzi wa miti, na vuguvugu la vijana la mazingira, Fridays for Future, katika kitengo cha Motisha na kuchukua hatua; Profesa Katharine Hayhoe, mwanasayansi wa mazingira kutoka katika Chuo Kikuu chaTexas Tech katika kitengo cha Sayansi na ubunifu; na Kampuni ya Patagonia ya kushona mavazi ya  kutumia mchana, katika kitengo cha Maono ya ujasiriamali.

Washindi wa mwaka huu watatuzwa kwenye sherehe itakayoandaliwa baadaye mwakani.

Pendekeza Bingwa wa Dunia

MAKALA KWA MHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni mtetezi mkuu wa masuala ya mazingira duniani.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano wa kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP, +254717080753

  • Patagonia imepokea tuzo  linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira kutokana na kuwa na  maono ya ujasiriamali.
  • Patagonia imetuzwa kutokana na kujitolea kwake kuhakikisha uendelevu na kufanya uhamasishaji ili kutunza rasilimali adimu katika sayari 

 

 

Septemba 24, 2019 -- Kampuni ya kushona mavazi ya kutokea nje wakati maalum Patagonia kutoka Marekani yashinda tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa na Umoja wa Mataifa la Mabingwa wa Dunia. Imepokea tuzo la kiwango cha juu sana linalotolewa na Umoja wa Mataifa kutokana na sera zake zinazotilia maanani uendelevu hali ambayo imewezesha mfumo wake wa biashara kufaulu. 

 

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) lilituza Patagonia katika kitengo cha maono ya ujasiriamali.

 

Tangu Patagonia ilipoanzishwa katika mwaka wa 1973 na mwanaharakati wa mazingira aliye mjasiriamali Yvon Chouinard, imesifiwa kutokana na mfumo wake endelevu wa usambasaji wa bidhaa zake na kuwa mwanaharakati wa mazingira. Kama anavyosema Chouinard: "Patagonia  inafanya kazi ili kuiokoa sayari yetu, iliyo makazi yetu".

 

Ijapokuwa ilianza kama kampuni ndogo ya kuunda vifaa vya kukwea milima, Patagonia imekuwa mfano wa kuigwa duniani kwa masuala ya uendelevu. Hamu yao ya kutunza mfumo wa ekolojia wa sayari inajitokeza katika biashara yao kuanzia kwa utengenezaji wa bidhaa, kupitia kwa vifaa vinavyotumiwa kutengeneza bidhaa na hadi kwa msaada wao wa kifedha unaosaidia kutunza mazingira. 

 

Taktibani asilimia 70 ya bidhaa za Patagonia huundwa kutokana na vifaa vilivyotumika, ikiwa ni pamoja na chupa za plastiki. Lengo lao ni kutumia asilimia 100 ya nishati jadidifu au kuunda bidhaa kutokana na vitu vilivyotumika kufikia mwaka wa 2025. Kampuni hii pia inatumia katani na pamba iliyopandwa bila kutumia kemikali. Wamejitolea kutongeneza nguo za kawaida, zinazopendeza na zinazodumu --  kazi ya kupigiwa upatu katika dunia ambapo kampuni nyingi na wanunuzi wengi hupendelea mitindo inayoweza kuuzwa kwa haraka. 

 

Tangu mwaka wa 1985, kampuni hiyo imetoa mchango wa asilimia isiyopungua 1 ya mauzo yake ili kusaidia kutunza na kuhifadhi mazingira asilia. Mnamo mwaka wa 2002, Chouinard na Craig Mathews, waanzilishi wa Blue Ribbon Flies, walianzisha shirika lisilokuwa la biashara -- asilimia 1 ya Kutunza Sayari -- ili kuvutia kampuni zingine kuwaiga. 

 

Kutokana na ahadi yake ya asilimia 1, Patagonia imetoa mchango wa dola za Marekani milioni 90 kwa mashirika nyanjani na kutoa mafunzo kwa wanaharakati vijana kwa kipindi cha miaka 35. 

 

"Kupitia kujitolea kwake kuhakikisha uendelevu unadumishwa na kukabiliana na changamoto kuu zinazokabili mazingira, Patagonia ni dhihirisho tosha la jinsi sekta ya kibinafsi inavyoweza kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na matishio mengine kwa binadamu na sayari,"  alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. 

 

"Patagonia inaonyesha kuwa uendelevu una manufaa kwa uchumi na kufauulu kwa kampuni hiyo kunaonesha kuwa matumizi wa bidhaa wana hamu ya kuona wamiliki wa biashara wakiwa mstari wa mbele kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira. Patagonia ni dhihirisho tosha kuwa inawezekana, na inawezekana kabisa," alisema. 

 

Wakati wa Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Mazingira wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika tahere 23 Septemba katika mji wa New York, Suala la umuhimu wa kuchukua hatua kali ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi litaangaziwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa viongozi duniani, wamiliki wa biashara na mashirika ya uraia kuhudhuria mkutano wakiwa na suluhisho jinsi watakavyopunguza uchafuzi wa hewa kwa asilimia 45 kufikia karne ijayo na kuepukana na hewa chafu kabisa kufikia mwaka wa 2050. Hii ni sambamba na Makataba wa Paris kuhusu  tabianchi na Malengo ya Maendeleo Endelevu.  

 

Biashara zina mchango mkubwa kwa sababu ili kupunguza uzalishaji wa hewa chafu, tunahitaji kubuni nafasi za kazi, kujenga miji mizuri, na kuboresha afya na uwezo wa watu wa kupata mali na kuhakikisha hakuna ubaguzi. 

 

"Tuna furaha isiyokuwa na kifani kutuzwa na Umoja wa Mataifa na tuna matumaini kuwa kampuni zingine zitatuiga kwa kuelewa kuwa kuna uwezo wa kuwa na biashara inayofaulu na pia kutunza mazingira kwa wakati uo huo. Kwa kweli, hiyo ndiyo njia ya pekee ya kukuwezesha kustawi huku sayari ikistawi," alisema said Rose Marcario, Afisa Mkuu Mtendaji wa Patagonia. 

 

"Nimekuwa na fursa ya kuona biashara nyingi, katika sekta za kibinafsi na sekta za umma, zinazotambua kuwa tunahitaji mabadiliko. Ili kuwa na sayari inayopendeza, ni sharti tubadilishe mifumo ya ubepari. Katika kampuni ya Patagonia, tuna imani kuwa changamoto zinazokabili mazingira zinaweza kutatuliwa nasi tumejitolea kutafuta suluhisho," alisema. 

 

Mnamo mwaka wa 2018, Patagonia ilisema itatoa dola milioni 10 ilizohifadhi kutokana na ushuru kwa serikali kama mchango kwa vikundi nyanjani vinavyohamasisha kuhusu utunzaji wa hewa, wa maji na wa ardhi pamoja na wale wanaojishughulisha na kilimo bila kutumia mbolea za kemikali-- mbinu ya kupanda mimea inayozingatia kuimarisha mchanga na inalenga kupunguza hewa ya ukaa.

Mabingwa wa Dunia, ni tuzo la kimataifa linalotolewa na Umoja wa Maataifa kwa heshima ya mazingira. Lilianzishwa na UNEP mwaka wa 2005 kuwatuza watu wa kipekee ambao matendo yao yamekuwa na athari chanya zinazoleta mabadiliko kwa mazingira.  Kutoka kwa viongozi duniani hadi kwa watetezi wa mazingira na hadi kwa wanaobuni teknolojia, waanzilishi hawa wanaleta mabadiliko ili kutunza sayari yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo.  

 

Patagonia ni mmoja wa washindi tano wa huu mwaka. Vitengo vingine ni pamoja na uongozi wa sera , motisha na kuchukua hatua  na sayansi na ubunifu. Washindi wa mwaka wa 2019 watatuzwa wakati wa sherehe ya gala mjini New York tarehe 26 Septemba wakati wa kikao cha 74 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.   Wengine watakaotuzwa pia wakati wa hafla hii ni wanamazingira wa kipekee saba wa umri wa kati ya miaka 18 hadi miaka 30. Watatuzwa tuzo la Vijana Bingwa Duniani.

 

Watu waliowahi kushinda tuzo la Mabingwa wa Dunia katika kitengo cha maono ya ujasiriamali ni pamoja na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Cochin, uwanja wa ndege wa kwanza kutumia nishati ya jua duniani (mwaka wa 2018); Paul Polman, aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji (mwaka wa 2015); na shirika la Marekani la  Green Building Council, shirika lisilokuwa la kibiashara linaleta mabadiliko katika sekta ya ujenzi (mwaka wa 2014). 

 

 

MAKALA KWA WAHARIRI

 

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni msemaji mkubwa wa kimataifa kuhusu mazingira.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.   

 

Kuhusu Weibo

Mabingwa wa Dunia huandaliwa kwa msaada wa ufadhili kutoka kwa  Weibo – Mtandao mkuu wa kijamii nchini China unaowezesha watu kuunda, kushiriki na kupata makala mtandaoni. Weibo ina zaidi ya watumizi 486 kila mwezi. 

 

Kuhusu Mabingwa wa Dunia

Tuzo linalotelewa kila mwaka la Mabingwa wa Dunia, hutuza viongozi vya kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta ya kibinafsi ambao matendo yao yamesababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. Tangu mwaka wa 2005, tuzo la Mabingwa wa Dunia limewatuza washindi 88, kuanzia kwa wakuu wa nchi hadi kwa wanaobuni teknolojia .

 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keisha Rukikaire, UNEP Habari na Vyombo vya Habari, rukikaire@un.org, +254 722 677747

  • Costa Rica yashinda tuzo muhimu la mazingira linalotolewa na Umoja wa Mataifa katika kitengo cha sera na uongozi
  • Nchi kotoka Amerika ya Kati imetuzwa kwa kuwa mstari mbele kuhakikisha kutokuwepo kwa hewa ya ukaa siku zijazo

 

 

Septemba 20, 2019 -- Costa Rica imekabidhiwa  tuzo la Mabingwa wa Dunia, tuzo kuu la mazingira linatolewa na Umoja wa Mataifa kutokana na juhudi zake za kutunza mazingira na sera zake za kipekee zinazowezesha kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

 

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa lilituza Costa Rica katika kitengo cha sera na uongozi.

 

Kiongozi anayedumisha uendelevu duniani, kutoka Amerika ya Kati, ni taifa lililoweka  mpango maalum wa kukomesha uzalishaji wa hewa ya ukaa katika uchumi wake ifikiapo mwaka wa 2050 kwa mjibu wa Mkataba wa Paris kuhusu  Tabianchi na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.   Lina matumaini ya kuweka mfano utakaoigwa na mataifa mengine ili kukabiliana na uzalishaji wa hewa chafu unaopelekea mabadiliko sugu ya tabianchi kutokea kwa kasi. 

 

Costa Rica imefaulu kufanya maamuzi ya kisera na kisiasa ya kushughulikia changamoto za mazingira na ni wazi kuwa kuna uwezekano wa kuwa na uendelevu kwa manufaa ya uchumi. 

 

"Costa Rica imekuwa  mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira na kudumisha amani na ni mfano wa kuigwa kwenye kanda na kote ulimwenguni;" alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.  

 

"Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, sisi sote tunapaswa kufanya maamuzi ya dharura yanayoleta mabadiliko. Na mpango wake kabambe wa kukomesha hewa ya ukaa katika uchumi wake, Costa Rica ina uwezo wa kufaulu", aliongezea. "Uzalishaji wa hewa chafu ulimwenguni unaongezeka kwa kasi. Wakati wa kufanya maamuzi ya kuwa na uchumi dhabiti usiochafua mazingira ni sasa.”

 

Suala la haja ya kuchukua hatua kali kote ulimwenguni ili kukabiliana ya mabadiliko ya tabianchi litaangaziwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres’ utakaofanyika tarehe 23 Septemba mjini New York.  Katibu Mkuu ametoa wito kwa viongozi duniani, wamiliki wa biashara na mashirika ya uraia kuhudhuria mkutano wakiwa na suluhisho tosha la jinsi watakavyopunguza uchafuzi wa hewa kwa asilimia 45 kufikia karne ijayo na kuepukana na hewa chafu kabisa kufikia mwaka wa 2050. Hii ni sambamba na Mkataba wa Paris na Malengo ya Maendeleo Endelevu.   

 

Mpango wa Kitaifa wa Kukomesha Hewa ya Ukaa ulizinduliwa Feburuari na una malengo ya kipindi kifupi na malengo ya kipindi kirefu ya kuleta mabadiliko kwenye sekta za usafiri, nishati, taka na matumizi ya ardhi. Lengo lake ni kutozalisha kabisa hewa ya ukaa kufikia mwaka wa 2050. Hii inamaanisha kuwa nchi hii haitazalisha tena hewa chafu kwa kuchukua hatua kama vile za kutunza misitu na kupanua eneo la misitu. 

 

Tayari, zaidi ya asilimia 98 ya nishati inayotumiwa na Costa Rica ni jadidifu na zaidi ya asili mia 53 ni eneo lililo na misitu baada ya juhudi kubwa za kukabiliana na hali ya ukataji miti iliyoshudiwa kwa karne nzima. Katika mwaka wa 2017, nchi hiyo ilitumia tu nishati jadidifu kwa siku 300. Lengo likiwa kutumia asilimia 100 ya umeme unaotokana na nishati jadidifu ifikapo mwaka wa 2030. Asilimia sabini ya mabasi na teksi zote zinatarajiwa kutumia umeme kufikia mwaka wa 2030, na inatarajiwa kuwa ifikiapo mwaka wa 2050, magari yote yatakuwa yanatumia umeme.

 

Kujitolea kwa Costa Rica kuwa taifa anzilishi la kukuza teknolojia ya kudumu isiyochafua mazingira ni suala la kupigiwa upatu kutokana na ukweli kuwa taifa hili lililo na idadi ya takribani watu milioni 5 huzalisha tu 0.4 ya hewa chafu duniani. 

 

"Ninapopokea tuzo la Bingwa wa Dunia kwa niaba ya Costa Rica, wananchi wake wote, vizazi vilivyopita vilivyotunza mazingira, na kwa niaba ya vizazi vijavyo, ni jambo ninalonifanya kujivuna kutokana na mafanikio ya Costa Rica na yale ambayo tunaweza kuendelea kufanya ili kupata mafanikio zaidi. Ninajivunia kuwa mwananchi wa Costa Rica," alisema Rais Carlos Alvarado Quesada.

 

"Takribani miaka 50 iliyopita, nchi hii ilianzisha kubuni sera kadhaa za mazingira kwa sababu mageuzi ya kuleta maendeleo endelevu ni sehemu ya maisha ya kila mwananchi wa Costa Rica. Mpango wa kutozalisha kabisa hewa ya ukaa unalenga kuongeza nafasi za kazi ili kuimarisha uchumi, kwa wakati uo huo ukipunguza matumizi ya nishati ya visukuku ili kupunguza uchafuzi wa hewa. Tutatimiza lengo hili vipi? Kupitia vyombo vya usafiri wa umma visivyochafua mazingira; miji imara ya kisasa; ushughulikiaji mzuri wa taka; kilimo endelevu na sera zilizoboreshwa," aliongezea. 

 

Tuzo la Mabingwa wa Dunia linatambua uwezo wa Costa Rica wa kuwa endelevu na kuonyesha umuhimu wa udharura wa kupata masuluhisho ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Mwaka jana, Jopo la Kimataifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi liligundua kuwa ili kudhibiti joto duniani kuwa nyusi joto 1.5 mabadiliko ya dharura yanahitajika ili kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa asilimia 45 kufikia mwaka wa 2030 ikilinganishwa na kiwango kilichoshuhudiwa mwaka wa 2010, na kuepukana na hewa chafu kabisa kufikia mwaka wa 2050.

 

Mabingwa wa Dunia, ni tuzo la kimataifa linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira. Lilianzishwa na UNEP mwaka wa 2005 kuwatuza watu wa kipekee ambao matendo yao yamekuwa na athari chanya zinazoleta mabadiliko kwa mazingira. Kutoka kwa viongozi duniani hadi kwa watetezi wa mazingira na hadi kwa wanaobuni teknolojia, waanzilishi hawa wanaoleta mabadiliko ili kutunza sayari yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo hutuzwa.  

 

Costa Rica ni mojawapo wa washindi tano wa mwaka huu. Vitengo vingine ni pamoja na maono ya ujasiriamali; motisha na kuchukua hatua; na sayansi na ubunifu.  Washindi wa mwaka wa 2019 watatuzwa wakati wa sherehe ya gala mjini New York tarehe 26 Septemba wakati wa kikao cha 74 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Wengine watakaotuzwa pia wakati wa hafla hii ni wanamazingira wa kipekee saba wa umri wa kati ya miaka 18 hadi miaka 30. Watatuzwa tuzo la Vijana Bingwa Duniani.

 

Washindi wa awali kutoka eneo hili ni  pamoja na Michelle Bachelet, aliyekuwa Rais wa Chile, kutokana na uongozi wake wa kipekee wa kuunda maeneo ya bahari yaliyohifadhiwa na kukuza nishati jadidifu (mwaka wa 2017); aliyekuwa waziri wa mazingira wa Brazil Izabella Teixeira kutokana na sera zake za uongozi na kazi aliyoifanya ya kupunguza ukataji wa miti katika misitu ya Amazon (mwaka wa 2013); na mwanaekolojia kutoka Meksiko José Sarukhán Kermez kwa uongozi wake wa kudumu na ubunifu wake wa kutunza bayoanuai nchini Meksiko na kote ulimwenguni (mwaka wa 2016). 

 

MAKALA KWA WAHARIRI

 

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ni msemaji mkubwa wa kimataifa kuhusu mazingira.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.    

 

Kuhusu Weibo

Mabingwa wa Dunia huandaliwa kwa msaada wa ufadhili kutoka kwaWeibo – Mtandao mkuu wa kijamii nchini China unaowezesha watu kuunda, kushiriki na kupata makala mtandaoni.  . Weibo ina zaidi ya watumizi milioni 486 kila mwezi. 

 

Kuhusu Mabingwa wa Dunia

Tuzo linalotelewa kila mwaka la  Mabingwa wa Dunia   hutuza viongozi vya kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta ya kibinafsi ambao matendo yao yamesababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. Tangu mwaka wa 2005, tuzo la Mabingwa wa Dunia limewatuza washindi 88, kuanzia kwa wakuu wa nchi hadi kwa wanaobuni teknolojia.   

 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keisha Rukikaire, UNEP Habari na Vyombo vya Habari, rukikaire@un.org, +254 722 677747