Cécile Bibiane Ndjebet (Cameroon), anayetuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni mtetezi asiyechoka wa haki za wanawake za kumiliki ardhi barani Afrika, hali inayohitajika kuwawezesha kutekeleza wajibu muhimu wa koboresha mifumo ya ekolojia, kupambana na umaskini na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia anaongoza juhudi za kushawishi kuwepo na sera kuhusu usawa wa kijinsia katika usimamizi wa misitu katika nchi 20 barani Afrika.