• Maelezo ya Jumla
  • Nyenzo

Anwani: Kongamano la Kikanda la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini la  NDCs 3.0 

Tarehe: Septemba 23-25 , 2024

Mahali:  Tunis, Tunisia

Maelezo:

Ripoti ya Pengo la Uzalishaji wa Hewa Chafu ya mwaka wa 2023 inaonya kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweza kupelekea ongezeko la joto la kati ya nyuzijoto kati ya 2.5 na 2.9 zaidi ya viwango vya kabla ya viwanda, hali inayoashiria umuhimu wa kushughulikia mazingira kwa dharura.

Wahusika wanapaswa kuimarisha ahadi na kuzungumzia awamu ijayo ya NDCs (NDCs 3.0) kufikia mwaka wa 2025 ili kuendana na malengo ya Mkataba wa Paris. NDC hizi zitakuwa muhimu kwa juhudi za kimataifa, na kutumika kama mwongozo wa mustakabali endelevu na lazima ziwe wazi, zinazoweza kutekelezeka, na zilizo na uwezo wa kuvutia ufadhili. 

Kwa kutoa mawazo kwa GST ya kwanza, NDC mpya zinapaswa kuwa nguzo ya utekelezaji ulio na mabadiliko, kuimarisha uthabiti, na kurandana na mipango ya kitaifa na mikakati ya maendeleo. Zinapaswa kujumuisha miongozo madhubuti ya kisera na mipango ya ufadhili ili kushughulikia mabadiliko ya tabianchi huku zikitumia fursa za ukuaji katika sekta zote.

Wakati nchi katika kanda za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini zinapojiandaa kwa awamu inayofuata ya NDCs, kuna fursa ya kipekee ya kuimarisha mikakati ya tabianchi ili kuwa na ahadi zaidi, na kutumia mafunzo kutoka kwa juhudi za awali za utekelezaji. Maendeleo ya haraka ya teknolojia ya nishati jadidifu, masuluhisho yanayotumia nishati vizuri, na miundomsingi inayostahimili tabianchi hutoa kwa nchi za MENA zana mpya za kufikia malengo yao ya tabianchi kwa ufanisi zaidi na kwa gharama nafuu. Kwa kuongezea, nchi nyingi za MENA, ambazo kijadi zilitegemea mapato ya mafuta na gesi, zinazidi kutambua manufaa ya kiuchumi ya kuwa na bidhaa mbalimbali katika uchumi wao. Uwekezaji katika teknolojia zisizochafua mazingira na viwanda endelevu unaweza kubuni nafasi za kazi, kuchochea ukuaji wa uchumi, na kupunguza utegemezi wa mafuta ya visukuku. Kwa hivyo, awamu mpya ya NDCs inayojali jamii nzima na malengo mapana kwa uchumi itakuwa na fursa nyingi.

Jukwaa hili litaangalia jinsi matokeo ya COP28, hasa uamuzi wa GST, unavyoweza kuongoza michakato ya kitaifa ili kuimarisha ahadi za NDC za siku zijazo na kuchangia kwa maendeleo endelevu. Kupitia kuelimishana, nchi zitajadili mbinu na fursa bora, na kuimarisha masuluhisho na miundo bunifu ya ufadhili. Zana na mwongozo utasaidia kujumuisha hatua na malengo mahususi wakati wa kuhakiki NDC. 

Nchi mwenyeji:

Wizara ya Mazingira ya Tunisia

Waandaaji

UNEP, UNDP, Ushirikiano wa NDC, na UN ESCWA kwa Ushirikiano na Sekretarieti ya UNFCCC (Shirika la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi) wanaandaa Mikutano ya Kikanda ya NDCs 3.0  

Waandaaji wenza 

Muungano wa Mazingira na Hewa Safi ulioitishwa na UNEP, Kituo cha Umoja wa Mataifa cha Kuratibu Mifumo ya Chakula 

Nyenzo zaidi: 

Ajenda - Muhutasari

Toleo la Habari - Mikutano ya kikanda inalenga kuongeza ahadi za nchi kabla ya awamu ijayo ya mipango ya tabianchi

Tarehe - Mikutano ya Kikanda

Wasiliana na

Giorgia Patarnello - giorgia.patarnello@un.org

Jihan El Osta - jihan.elosta@un.org