Nairobi, Novemba22, 2022 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) leo lilitangaza washindi wake wa mwaka wa 2022 wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia. Linawatuza mhifadhi wa Mazingira, shirika, mwanauchumi, mwanaharakati wa haki za wanawake, na mwanabiolojia wa wanyamapori kwa hatua zao za kuleta mabadiliko chanya ya kuzuia, kusitisha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia.   

Tangu kuzinduliwa kwake katika mwaka wa 2005,  tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa kila mwaka, limetolewa kwa watu walio msitari mbele kufanya juhudi za kuhifadhi ulimwengu asilia. Ni tuzo la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu zaidi linalotolewa kwa heshima ya mazingira. Kufikia sasa,  limewatuza washindi 111: viongozi wa dunia 26, watu binafsi 69 na mashirika 16. Mwaka huu, idadi ya watu 2,200 walipendekezwa kushiriki kutoka pembe zote za dunia.

"Mifumo dhabiti ya ekolojia, inayofanya kazi ni muhimu ili kuzuia dharura ya tabianchi na kuzuia uharibifu wa bayoanuai kusababisha uharibifu usioweza kurekebika kwa sayari yetu. Mabingwa wa Dunia wa mwaka huu wanatupa matumaini kwamba uhusiano wetu na mazingira unaweza kuboreshwa,” alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Mabingwa wa mwaka huu wanaonyesha jinsi kuboresha mifumo ya ekolojia na kuimarisha uwezo wa kipekee wa mazingira wa kujiimarisha ni wajibu wa kila mtu: serikali, sekta ya kibinafsi, wanasayansi, jamii, NGOs na watu binafsi."

Mabingwa wa Dunia wa Mwaka wa 2022 ni:

  • Arcenciel (Lebanon), kampuni inayotuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni shirika linalokuza mazingira safi na bora na kuchangia msingi wa kuwekwa kwa mkakati wa kitaifa wa kushughulikia taka nchini Lebanon. Kwa sasa, arcenciel huchakata zaidi ya asilimia 80 ya taka za hospitali zinazoweza kuambukiza magonjwa nchini Lebanon kila mwaka.
  • Constantino (Tino) Aucca Chutas (Peru), ambaye pia ametuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ameanzisha mfumo wa upandaji miti katika jamii unaoendeshwa na wenyeji na jamii za kiasili. Hali ambayo imepelekea miti milioni tatu kupandwa nchini Peru.  Pia anaongoza juhudi kabambe za upandaji miti katika nchi zingine za eneo la Andes.
  • Hababi (Sir) Partha Dasgupta (Uingereza), anayetuzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu, ni mwanauchumi mashuhuri ambaye ukaguzi wake wa kipekee kuhusu uchumi wa bayoanuai unatoa wito kutafakari upya mno kuhusu uhusiano wa binadamu na mazingira asilia ili kuzuia mifumo muhimu ya ekolojia kuporomoka.
  • Dkt Purnima Devi Barman (India), anayetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali, ni mwanabiolojia wa wanyamapori anayeongoza "Jeshi la Hargila", vuguvugu la wanawake pekee la uhifadhi mashinani linalojitolea kulinda Korongo aina ya Greater Adjutant Stork dhidi ya kuangamia.  Wanawake hawa hutengeneza na kuuza nguo zilizo na michoro ya ndege hao, na kusaidia kuhamasisha kuhusu spishi hii huku wakiweza kujitegemea kifedha.
  • Cécile Bibiane Ndjebet (Kameruni), anayetuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni mtetezi asiyechoka wa haki za wanawake za kumiliki ardhi barani Afrika, hali inayohitajika kuwawezesha kutekeleza wajibu muhimu wa koboresha mifumo ya ekolojia, kupambana na umaskini na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.  Pia anaongoza juhudi za kushawishi kuwepo na sera kuhusu usawa wa kijinsia katika usimamizi wa misitu katika nchi 20 barani Afrika.

Kufuatia uzinduzi wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia (2021-2030), matuzo ya mwaka huu yanaangazia juhudi za kuzuia, kusitisha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote duniani.

Mifumo ya ekolojia katika kila bara na katika kila bahari inakabiliwa na vitisho vikuu. Kila mwaka sayari hupoteza maeneo ya misitu kiasi sawa na taifa la Ureno. Samaki huvuliwa baharini kupita kiasi na bahari kuchafuliwa, huku tani milioni 11 za plastiki pekee zikielekea katika mazingira ya baharini kila mwaka. Spishi milioni moja ziko katika hatari ya kutoweka kwani makazi yao yanapotea au kuchafuliwa.

Uboreshaji wa mifumo ya ekolojia ni muhimu ili kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzijoto 2 na kuweza kusaidia jamii na uchumi kukabiliana na mabadiliko yatabianchi. Pia ni muhimu ili kukabiliana na baa la njaa: uboreshaji kupitia kilimo cha misitu pekee una uwezo wa kuongeza utoshelezaji wa chakula kwa watu bilioni 1.3. Kurejesha tu asilimia 15 ya ardhi ambayo matumizi yamebadilishwa kunaweza kupunguza hatari ya kutoweka kwa spishi kwa asilimia 60. Uboreshaji wa mifumo ya ekolojia utafaulu tu ikiwa kila mtu atajiunga na vuguvugu la #GenerationRestoration.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kuhusu  Tuzo la UNEP la Mabingwa wa Dunia

Tuzo la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi, makundi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. Tuzo linalotolewa mara moja kwa mwaka la Mabingwa wa Dunia ni tuzo la umoja wa mataifa la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira. Hutuzwa kwa viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi.      

Kuhusu Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia 

Baraza la Umoja wa Mataifa lilitangaza kuanzia mwaka wa 2021 hadi mwaka wa 2030 kuwa  Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia. Muongo unaongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, pamoja na msaada kutoka kwa wabia lilibuniwa kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni. Unalenga kuboresha mabililioni ya hekta za aridhi ya nchi kavu pamoja na mifumo ya ekolojia ya majini. Mwito kwa jamii ya kimatifa, Muongo wa UN huungwa mkono na wanasiasa, utafiti wa kisayansi, na ufadhili ili kuimarisha uboreshaji.  

 Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

 

Video

Arcenciel (Lebanon), kampuni inayotuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni shirika linalokuza mazingira safi na bora na kuchangia msingi wa kuwekwa kwa mkakati wa kitaifa wa kushughulikia taka nchini Lebanon. Kwa sasa, arcenciel huchakata zaidi ya asilimia 80 ya taka za hospitali zinazoweza kuambukiza magonjwa nchini Lebanon kila mwaka. 

Video

Constantino (Tino) Aucca Chutas (Peru), ambaye pia ametuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ameanzisha mfumo wa upandaji miti katika jamii unaoendeshwa na wenyeji na jamii za kiasili. Hali ambayo imepelekea miti milioni tatu kupandwa nchini Peru. Pia anaongoza juhudi kabambe za upandaji miti katika nchi zingine za eneo la Andes.

Video

Sir Partha Dasgupta (Uingereza), aliyetuzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu, ni mwanauchumi mashuhuri ambaye ukaguzi wake wa kipekee kuhusu uchumi wa bayoanuai unatoa wito kutafakari upya mno kuhusu uhusiano wa binadamu na mazingira asilia ili kuzuia mifumo muhimu ya ekolojia kuporomoka.

Video

Dkt Purnima Devi Barman (India), anayetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali, ni mwanabiolojia wa wanyamapori anayeongoza "Jeshi la Hargila", vuguvugu la wanawake pekee la uhifadhi mashinani linalojitolea kulinda Korongo aina ya Greater Adjutant Stork dhidi ya kuangamia. Wanawake hawa hutengeneza na kuuza nguo zilizo na michoro ya ndege hao, na kusaidia kuhamasisha kuhusu spishi hii huku wakiweza kujitegemea kifedha. 

Video

Cécile Bibiane Ndjebet (Cameroon), anayetuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni mtetezi asiyechoka wa haki za wanawake za kumiliki ardhi barani Afrika, hali inayohitajika kuwawezesha kutekeleza wajibu muhimu wa koboresha mifumo ya ekolojia, kupambana na umaskini na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia anaongoza juhudi za kushawishi kuwepo na sera kuhusu usawa wa kijinsia katika usimamizi wa misitu katika nchi 20 barani Afrika.

Hababi David Attenborough ndiye mshindi wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia la Mafanikio ya Kudumu kutokana na juhudi zake za utafiti, uandaji wa makala, na uhamasishaji kuhusu utunzaji na uboreshaji wa mazingira.

 

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) lilitangaza leo kuwa Hababi David Attenborough ndiye mshindi wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia la Mafanikio ya Kudumu  kutokana na juhudi zake za utafiti, uandaji wa makala, na uhamasishaji kuhusu utunzaji na uboreshaji wa mazingira. 

"Hababi David Attenborough amejitolea katika maisha yake kurekodi hadithi ya upendo uliopo kati ya wanadamu na mazingira, na kuitangaza kwa ulimwengu.  Iwapo tutaweza kukabiliana na hali mbaya ya hewa na uharibifu wa bayoanuai na kusafisha mifumo ya ekolojia iliyochafuliwa, hili litatokea tu kwa sababu baadhi yetu kwa mamilioni tulianza kupenda sayari ambayo alituonyesha kwenye televisheni," Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP alisema.  “Kazi ya Hababi David itaendelea kuhamasisha watu wa umri wowote kutunza mazingira na kuwa kizazi cha uboreshaji.”

Kazi ya Attenborough kama mtangazaji, mwanahistoria wa asili, mwandishi, na mhamasishaji wa mazingira imedumu kwa zaidi ya miongo saba.  Anajulikana zaidi kwa kazi yake katika Kitengo cha Historia ya Asili cha BBC, ikijumuisha makala kama vile Life on Earth, the Living Planet, Our Planet and Our Blue Planet.  Kwa kuongezea, uhamasishaji wake wa kuhifadhi na kuboresha bayoanuai, kutumia nishati jadidifu, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ya kukuza matumizi ya lishe kutoka kwa mimea huchangia kufikiwa kwa mengi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

"Ulimwengu unapaswa kushirikiana.  Matatizo haya hayawezi kutatuliwa na taifa moja - haijalishi ukubwa wa taifa hilo.  Tunajua matatizo ni yepi na tunajua jinsi ya kuyatatua.  Tunachokosa ni ushirikiano wa kuyashughulikia, "Attenborough alisema alipopokea Tuzo la Mafanikio ya Kudumu.   “Miaka 50 iliyopita, nyangumi walikuwa karibu kutoweka kote ulimwenguni.  Kisha watu wakashirikiana na kwa sasa kuna nyangumi wengi zaidi baharini kuliko ilivyowahi kushuhudiwa na wanadamu. Tukichukua hatua kwa pamoja, tunaweza kutatua matatizo haya.”    

Attenborough amekuwa mfuasi wa muda mrefu na shupavu wa ushirikiano wa kimataifa kuhusiana na mazingira.  Katika mwaka wa 1982, wakati wa  mkutano wa 10 wa Baraza Linaloongoza UNEP, aliambia Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa: “Kile ambacho wewe na mimi na watu wengine wa kawaida kote ulimwenguni tunaweza kufanya hakitaokoa ulimwengu asilia. Maamuzi makuu, majanga makubwa yanayotukabili, yanaweza tu kushughulikiwa na serikali na ndiyo sababu shirika hili ni muhimu sana.”

Tuzo hiii la Mafanikio ya Kudumu linatolewa katika mwaka wa kihistoria kwa jumuiya ya kimataifa ya mazingira. Mwaka wa 2022 ni maadhimisho ya miaka hamsini tangu kutokea kwa Kongamano la Umoja wa Mataifa la mwaka wa 1972 kuhusu Mazingira ya Binadamumjini Stockholm, Uswidi, ambalo lilikuwa mojawapo ya mikutano ya kwanza ya kimataifa kuhusu mazingira. Kongamano hilo lilichochea uundaji wa wizara na mashirika ya mazingira kote duniani, lilianzisha mikataba mipya ya kimataifa ya kushirikiana kutunza mazingira, na kupelekea kuundwa kwa UNEP, ambayo inaadhimisha miaka 50 mwaka huu.   

Washindi wa awali ni pamoja na mhamasishaji wa mazingira Robert Bullard (2020), mtetezi wa haki za mazingira na asili Joan Carling (2018) na mwanabayolojia wa mimea José Sarukhán Kermez (2016).  Washindi huchaguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, ambaye pia hutoa tuzo hilo.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu  Tuzo la UNEP la Mabingwa wa Dunia Tuzo la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi, makundi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira.  Tuzo linalotolewa mara moja kwa mwaka la Mabingwa wa Dunia ni tuzo la umoja wa mataifa la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira.   Hutuzwa kwa viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi.

Kuhusu Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia

Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia 2021-2030 ni wito wa kutunza nakuboresha mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni kwa manufaa ya binadamu na sayari. Unalenga kusitisha uharibifu wa mifumo ya ekolojia, na kuiboresha ili kufikia malengo ya kimataifa. Baraza la Umoja wa Mataifa lilitangaza Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia unaongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa ikijumuisha kuimarisha juhudi za wanasiasa za kuiboresha pamoja na maelfu ya miradi inayoendelea.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.  

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa MataifaMoses Osani, Afisa wa Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

 

Jua linapotua eneo la kati nchini Zambia, miale ya rangi ya machungwa inaakisi kwenye Kinamasi cha Lukanga, eneo kubwa la ardhi oevu lililo na upana wa kilomita mraba 2,600.

Njia yenye maji mengi hupita kwenye mianzi ya kinamasi na yungiyungi za maji ya zambarau, ambayo hutumiwa na mitumbwi kila siku, huku ikivusha wavuvi kwenda na kurudi kwenye kambi zao zinazoelea.  Miongoni mwao ni John Chisela, mmoja wa zaidi ya watu milioni 6 wanaotegemea maeneo oevu - na misitu inayoyazunguka - kupata chakula, kuni na mapato. 

Lakini kwa wengi hapa, maisha yanaendelea kuwa hatari zaidi

"Samaki wanaovuliwa wanaendelea kupungua," anasema Chisela, ambaye anapata dola 60 za Marekani kutokana na kuvua kilo 50 ya samaki, fedha zinazotosha tu kukidhi mahitaji ya familia yake.  "Ila hakuna kazi zingine katika eneo hili." 

Kinamasi cha Lukanga kinashambuliwa. Katika maeneo oevu, ambayo ni makazi ya viumbe wengi walio hatarini kuangamia, mabadiliko ya tabianchi yanapelekea mawimbi ya joto na hali mbaya ya hewa, kama vile mafuriko na ukame.  Baadhi ya sehemu za kinamasi kinachosalia na unyevunyevu mwaka mzima zinazidi kukumbwa na mafuriko, huku maeneo kame yakizidi kukauka. 

Katika Shule ya Msingi ya Mukubwe, Mwalimu Mkuu Mwamba Achilleus Bwalya anaeleza kuwa kwa kuwa na pampu moja tu katika mji mzima ya kusambazia maji kwa wanafunzi 800 na nyumba 300, ukame huathiri uendaji shuleni huku familia zikihangaika kulisha watoto wao.

"Moyo wangu husononeka ninapoona watoto wakizunguka tu na hawaji shuleni," anasema Bwalya.

Wakati uo huo, uvuvi wa kupita kiasi katika maeneo oevu na ukataji miti katika misitu inayozunguka maeneo hayo ni hali inayoendelea kupunguza kwa kasi malighafi ya eneo hilo na kusababisha uharibifu wa udongo.  Kote ulimwenguni, maeneo oevu ndio mfumo wa ekolojia unaokabiliwa na vitisho zaidi, unaotoweka kote ulimwenguni kwa viwango vinavyotisha – mara tatu zaidi kuliko misitu. Kufikia mwaka wa 2000, baadhi ya  asilimia 85 ya maeneo oevu yaliyokuwepo katika mwaka 1700 yalikuwa yamepotea, huku kuanzisha shughuli za kilimo ikiwa miongoni mwa vitishio vikuu vinavyoendelea kukabili mfumo huu wa ekolojia.

"Licha ya umuhimu wake, mifumo ya ekolojia ya maeneo oevu na misitu nchini Zambia kwa sasa inakabiliwa na ukataji miti kwa kiasi kikubwa na uharibifu," alisema Jean Kapata, Waziri wa Ardhi na Maliasili, katika hafla iliyoandaliwa na serikali Aprili 2021.

A woman stands next of a basket full of charcoal.
Febby Mukangwa, mama wa watoto wanane, anauza makaa karibu na eneo oevu ya Lukanga, akipokea malipo ya dola za Marekani 0.30 kwa kila gunia analoouza “Bei imeanza kushuka tena.  Nina matatizo ya kulisha familia, na hatuna chakula kama kawaida,” anasema Mukangwa.  Picha: UNEP/Georgina Smith

Kurejesha Ustahimilifu

Ili kusaidia kubadilisha hali hiyo, serikali ya Zambia inatekeleza mradi mpya wa miaka minne ili kusaidia jamii karibu na maeneo oevu ya Lukanga na Bangweulu kwenye mkoa wa Kati na Luapula nchini humo. 

Kwa kuzingatia mkabala unaozidi kuthaminiwa wa kujenga ustahimilifu dhidi ya tabianchi, unaojulikana kama uboreshaji kutegemea mfumo wa ekolojia, mradi huo unarejesha mifumo ya ekolojia ya maeneo oevu na ya misitu ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa jamii.   

Maeneo oevu na misitu hupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kunyonya maji ya mvua kupita kiasi ardhini wakati wa mafuriko na kuwa vyanzo vya maji wakati wa ukame. Kadiri mfumo wa ekolojia unavyotoweka, vivyo hivyo vidhibiti hivi muhimu vya hali ya hewa hutoweka, na hivyo jamii hukumbwa mara kwa mara na vipindi vya mafuriko na ukame.

Mradi wa Zambia unafadhiliwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na kupokea ufadhili wa dola milioni 6 za Marekani kutoka kwa Global Environment Facility, mfadhili mkuu wa miradi ya mabadiliko ya tabianchi. 

Uboreshaji wa mifumo ya ekolojia utajumuisha mbinu inayojulikana kama 'kusaidiwa kujiboresha kiasili', njia ya gharama ya chini ambayo inalenga kukabiliana na vitendo vinavyoharibu maliasili, kama vile mioto misituni, kulisha mifugo kupindukia na kukata miti ili kupata mbao, na kujumuisha shughuli za kuzalisha mapato zisizoharibu maliasili. kama vile ufugaji wa samaki kutokana na maji yanayokusanywa wakati wa mafuriko. 

Mradi huu pia utabainisha mikakati ya kuondoa magugu ya Kariba, spishi vamizi ambayo huziba njia za maji na kudhuru spishi za samaki.  Kwa kuzingatia ari ya masuluhisho yanayotokana na mazingira, mradi huu unafikiria kujumuisha mbinu iliyofanyiwa majaribio ya kutumia wadudu walao nafaka, wanyama wanaokula magugu ya Kariba. 

Children pumping water from a well.
Watoto wanatumia kisima cha pekee katika Shule ya Msingi ya Mukubwe kunyunyuzia sehemu ya mboga shuleni humo. Mabadiliko ya tabianchi yanasababisha ukame wa mara kwa mara katika eneo hili.  Picha:  UNEP/Georgina Smith

Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia ulizinduliwa mwaka jana kwa kutambua manufaa mengi ambayo kuboresha mazingira huletea jamii," alisema Jessica Troni, Mkuu wa Kitengo cha Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi cha UNEP. "Hii ni pamoja na uwezo wa mazingira kututunza na kutukinga dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, na maeneo oevu nchini Zambia ni mfano mzuri wa hali hii kupitia vitendo." 

Kupitia mtaji wa kuanzia na msaada wa kiufundi, mradi huu utafanya kazi na jamii, kama zile zilizo karibu na Shule ya Msingi ya Mukubwe, kupanda mazao yanayostahimili hali ya hewa ili kustahimili ukame vyema, lakini pia kuweka mifumo ya kukusanya maji ya mvua wakati wa misimu ya mvua.

Kukabiliana na  Hali Mbaya Inayojirudiarudia

Mwanafunzi Clement Katemba anasema kuwa jamii yake inaendelea kutafuta njia mbadala za kujikimu zisizodhuru maeneo oevu na misitu - jambo ambalo mradi huu utalishughulikia moja kwa moja. Lakini uzalishaji wa makaa, unaohusisha ukataji wa miti inayozunguka eneo oevu, unaonekana kama njia ya pekee ya kujipatia mapato siku baada ya siku. 

"Tunakata miti kupata makaa kwa sababu hiyo ndiyo njia ya pekee tunayoweza kutumia kukimu mahitaji ya familia zetu.  Wakati wa kiangazi, sisi hulazimika kufanya chochote ili kuwa na maisha bora, ili kuhakikisha kuwa mahitaji ya wazazi yanatimizwa.  Lakini msitu ni muhimu kwetu - hatutaki kuuharibu,” anasema Katemba. 

Mbewe, Msimamizi wa mradi huu, anasema wanajamii watasaidiwa na mradi huu ili kuwa na njia mbadala za kujikimu, ikijumuisha ufugaji wa nyuki, ambao unapunguza shinikizo la uvuvi.

"Hatua ya kwanza itakuwa kufanya tathmini ya madhara ya tabianchi ili kuonyesha eneo oevu na kujua ni hatua gani zinahitajika kwa haraka na ni wapi zinapohitajika," alisema Mbewe.  "Kisha tunaweza kusaidia jamii kukuza mbinu endelevu zaidi za kuzalisha mapato, ili kuchoma makaa, uvuvi wa kupita kiasi na ukataji miti zisiwe njia pekee za kutegemewa.

Changamoto ya kimataifa

Licha ya uwezo wa kusaidia kukabiliana na hali ya hewa kama makazi kwa wanyamapori, kuchuja uchafuzi wa mazingira na kufanya kazi kama hifadhi muhimu za kaboni, maeneo oevu hukabiliwa na vitisho vinavyoongezeka kote ulimwenguni kutokana na kupanda kwa usawa wa bahari, uchujukaji wa matumbawe na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea kwa kasi. 

Chini ya Lengo la 6 la Maendeleo Endelevu, nchi zote zimejitolea kutunza na kuboresha maeneo oevu kufikia mwaka wa 2030.  UNEP ina jukumu maalum la kusaidia kufuatilia na kufikia lengo hili, na kwa kuchukua hatua ya kuboresha mifumo ya ekolojia iliyoongeza kuharibiwa kwa kasi wakati wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia.  

Ili kuunga mkono masuluhisho yanayotokana na mazingira kote ulimwenguni kukabiliana na tabianchi, UNEP na Muungano wa Kimataifa wa Kuhifadhi Mazingira (IUCN) wanasimamia kwa pamoja Mfuko wa Global EbA Fund, kwa sasa wanatoa angalau yuro milioni 30 kwa mtaji wa kuanzia kufadhili mbinu bunifu.

 

Kwa habari zaidi kuhusu mradi huu, kwa jina rasmi la Kujengea Ustahimilivu Jamii nchini Zambia kupitia Matumizi ya Mbinu Inayotegemea Mifumo ya Ekolojia katika Mifumo iliyopewa Kipaumbele, tafadhali wasiliana naJessica.Troni@un.org. Jiifahamishe zaidi kuhusu kazi yetu inayoungwa mkono na GEF katika  kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hapa.

 

 

  • Tuzo la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi, makundi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira.
  • Mwaka huuupendekezaji wa watu binafsi na mashirika ambayo yamesaidia kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia haswa wanahimizwa kushiriki.  
  • Upendekezaji utaanza tarehe 15 Machi hadi tarehe 11 Aprili mwaka wa 2022.

Nairobi, Machi 15 2022 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) leo limezindua wito wa kupendekeza watakaowania tuzo lake la Mabingwa wa Dunia linalotolewa kila mwaka – tuzo la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira ili kujivunia viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi kwa mchango wao chanya kwa mazingira.

Ili kuonyesha umuhimu wa kuboresha mifumo ya ekolojia, wito wa mwaka wa 2022 unahimiza upendekezaji wawatu na mashirika ambayo yamechangia  kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote duniani. Takribani mwaka mmoja tangu kuzinduliwa kwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, hakujawahi kuwa na hitaji la kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kuliko sasa. Mifumo yetu ya ekolojia ikiwa dhabiti, watu na sayari vitanawiri.

Tangu kuzinduliwa kwake katika mwaka wa 2005, tuzo hili limemulika viongozi ambao wamejitolea kufanya kazi kuhakikisha kuna sayari endelevu isiyobagua. Jumla ya washindi 106, kuanzia kwa wakuu wa nchi na wanaharakati katika jamii hadi kwa vinara wa viwanda na wanasayansi waanzilishi, wametuzwa kama Mabingwa wa Dunia

Katika mwaka wa 2021, Tuzo la Mabingwa wa Dunia lilishuhudia tena kiwango kikubwa cha watu waliopendekezwa kutoka pembe zote za dunia. Kuongezeka kwa wanaowania kwa kipindi cha miaka iliyopita kunaonyesha kuongezeka kwa idadi ya watu wanajitolea kupigania mazingira na kutambua mno umuhimu wa kazi yao. 

Washindi wa UNEP wa mwaka wa 2021 wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia walikuwa:

  • Waziri Mkuu Mia Mottley wa Barbados, aliyetuzwa katika kitengo cha Uongozi Unaozingatia Sera kwa juhudi zake za kuhakikisha kuna dunia endelevu kwenye nchi za kipato cha chini. Mara kwa mara yeye huhamasisha kuhusu hatari inayokumba Mataifa Madogo ya Visiwa Yanayoendelea kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
  • Maria Kolesnikova (Jamhuri ya Kyrgyz), aliyetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali, ni mwanaharakati wa mazingira, mtetezi wa vijana na msimamizi wa MoveGreen, shirika linalofanya kazi kufuatilia na kuboresha hewa katika eneo la Asia ya kati.
  • Dkt. Gladys Kalema-Zikusoka (Uganda), aliyetuzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu, alikuwa daktari wa mifugo wa  kwanza kabisa wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Uganda, na ni mamlaka inayotambulika duniani inayoshughulikia wanyama wa familia ya nyani na magonjwa kutoka kwa wanyama.

Watu binafsi, mashirika ya serikali, makundi na mashirika yanaweza kuteuliwa chini ya vitengo vya Uongozi Unaozingatia Sera, Kujitolea na Kuchukua Hatua, Maono ya Ujasiriamali na Sayansi na Ubunifu.  Yeyote anaweza kutoa mapendekezo.  Tarehe ya mwisho ya kutuma mapendekezo ni Aprili 11, 2022. 

Pendekeza Bingwa wa Dunia 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Tuzo la UNEP la Mabingwa wa Dunia

Tuzo la UNEP la  Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi, makundi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira.  Tuzo linalotolewa mara moja kwa mwaka la Mabingwa wa Dunia ni tuzo la umoja wa mataifa la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira.  Hutuzwa kwa viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi.

Kuhusu Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia

Baraza la Umoja wa Mataifa limetangaza kuanzia mwaka wa 2021 hadi mwaka wa 2030 kuwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia. Muongo unaongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa na msaada kutoka kwa wabia ulibuniwa kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni.  Unalenga kuboresha mabililioni ya hekta za aridhi ya nchi kavu pamoja na mifumo ya ekolojia ya majini.  Mwito kwa jamii ya kimatifa, Muongo wa UN huleta pamoja wanasiasa, watafiti wa kisayansi, na wabia ili kuimarisha uboreshaji. 

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

UNEP@50: Ni wakati wa kutafakari kuhusu yaliyopita na kutazamia yajayo

Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira ya Binadamu mjini Stockholm, Uswidi katika mwaka wa 1972, lilikuwa kongamano la kwanza la Umoja wa Mataifa kutumia neno "mazingira" kwenye anwani yake kwa mara ya kwanza. Kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ni mojawapo wa matokeo makuu ya kongamano hili lililoanzisha mambo mengi. UNEP ilianzishwa kuwa kitengo cha kushughulikia mazingira cha Umoja wa mataifa kote ulimwenguni.  Shughuli zinazoendelea katika mwaka wa 2022 zitaangazia hatua kubwa zilizopigwa na yanayojiri katika miongo ijayo. 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP

Moses Osani, Afisa wa Vyombo vya Habari, UNEP