Usajili wa kushiriki UNEA umehitimika kwa sasa.
Taarifa zilizotolewa awali zinapatikana hapo chini.
UNEA-6 (Februari 26 - Machi 1, 2024) iko wazi kwa washiriki kutoka kwa Mataifa 193 Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Pia unaweza kushiriki kama mwaangalizi kutoka:
(i) wajumbe wa mashirika maalumu ambayo si wanachama wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (kanuni ya 68 ya sheria za utaratibu za Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa)
(ii) mashirika maalum na mashirika ya aina hii, mashirika na taasisi za Umoja wa Mataifa, mashirika ya serikali mbalimbali na mashirika ya kikanda ya ushirikiano wa kiuchumi (kanuni ya 69)
iii) na mashirika ya kimataifa yasiyo ya serikali (kanuni ya 70)
Washiriki wa UNEA-6 lazima wawe na umri wa angalau miaka 18. Washiriki walio na umri wa chini ya miaka 18 watachukuliwa kuwa watoto na wataambatana na mtunzaji. Wote watatii masharti yaliyowekwa katika miongozo ya kuingia na kushiriki kwa watoto katika mkutano wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa na kutia saini fomu ya makubaliano ya Mtunzaji.
Washiriki wanaojiandikisha kushiriki kwenye UNEA-6 wanaweza pia kujiandikisha kwa OECPR (Februari 19 - 23, 2024) kupitia linki ileile.
Tafadhali fahamu kuwa hakuna usajili unaoweza kufanywa kupitia barua pepe. Usajili wote lazima ufanywe mtandaoni kupitia mfumo wa usajili wa INDICO.
Kwa taratibu za usajili, tafadhali angalia kwa makini kundi mwafaka hapo chini. Tafadhali kumbuka kuwa usajili utahitaji kuundwa kwa akaunti ya INDICO kwa watumiaji wa mara ya kwanza. Washiriki wote lazima wasajiliwe ili kuweza kuhudhuria UNEA-6 na OECPR. Washiriki pia wanapaswa kuhakikisha kwamba barua pepe inayotumiwa kwa usajili ni sahihi na kuangalia barua pepe zao mara kwa mara ili kupokea mawasiliano na taarifa kuhusu UNEA, ikiwa ni pamoja na taarifa muhimu kama vile utoaji wa visa.
Washiriki wanahimizwa kujiandikisha mapema kabla ya tarehe ya mwisho ya usajili. UNEA-6 itafanyika ana kwa ana, hii inamaanisha kwamba wawakilishi wote wa Nchi Wanachama na washiriki wengine wanahimizwa kuhudhuria mikutano yote rasmi ana kwa ana.
Tafadhali kumbuka kuwa mchakato wa ukaguzi na uthibitishaji wa usajili wa mtandaoni si wa kiotomatiki na unaweza kuchukua hadi siku kadhaa, ambazo zinaweza kutofautiana kutegemea kiasi cha idadi ya waliojisajili.
Washiriki walioidhinishwa watapokea arafa kupitia kwa barua pepe pamoja na msimbo wa QR wa uthibitishaji kutoka kwa tovuti ya INDICO, ambao utatumika kukamilisha mchakato wa kujiandikisha watakapowasili katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi (UNON) kibinafsi na kuchukua beji mapema na wakati wa kikao.
Tafadhali kumbuka kuwa Serikali ya Kenya imefanyia marekebisho kanuni za viza kwa kuanzisha Uidhinishaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Usafiri (eTA) na kuondoa mahitaji ya viza kwa raia wote wa kigeni wanaosafiri kwenda Kenya kuanzia Januari mwaka wa 2024. Washiriki wote lazima wawe na eTA iliyoidhinishwa kabla ya kuanza safari zao. Wajumbe waliotuma maombi ya visa hapo awali na kupewa visa ya kuingia wanaweza kuitumia kuingia Kenya ikiwa bado inatumika kwa siku 90 zinazohitajika. Wale ambao bado hawajatuma maombi wanashauriwa kutumia the jukwaa la eTA kutuma maombi yao mtandaoni, huku yakionyesha madhumuni yao ya usafari kama Mjumbe wa Kigeni kwa kuzingatia mwongozo wa hatua kwa hatua uliotolewa. Inapendekezwa sana kwamba wasafiri watume ombi pindi tu baada ya kupata mahali watakapoishi na tiketi za usafiri.
Washiriki wote waliosajiliwa na walioidhinishwa watapewa beji ilio na picha ili kuweza kuingia kwenye ukumbi kwa kipindi cha OECPR na UNEA-6 tu. Washiriki wote watalazimika kukaguliwa kila siku kwenye lango kuu la kuingia UNON.
Tafadhali angalia kwa makini kundi mwafaka hapo chini.