Kaulimbiu ya jumla ya UNEA-6 ni juhudi madhubuti, jumuishi na endelevu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi.
Nchi Wanachama na washikadau watakuja pamoja kwa UNEA-6 kujadili kuhusu jinsi ya kuendeleza Muongo wa Kuchukua Hatua kwa kuzingatia ushughulikiaji wa maingiliano ya changamoto za mazingira za aina tatu duniani. Msururu wa mijadala ya viongozi na na washikadau mbalimbali na zaidi ya hafla rasmi 30 za kando nahafla nyinginezo za aina hii zinatarajiwa kuweka misingi ya siku zijazo wa kuimarishwa kwa juhudi za uratibu wa kimataifa na kikanda na Umoja wa Mataifa, Nchi Wanachama na wabia ili kuchukua hatua zangazi ya juu za kushughulikia sayari.
- Katika aya ya 9 ya uamuzi wa 5/4 wa UNEA, Baraza liliomba Ofisi yake, kwa kushauriana na Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu, kufafanua kaulimbiu ya UNEA-6 kabla ya miezi kumi na miwili kabla ya mkutano.
- Wakati wa mkutano wa pamoja wa Ofisi ya Baraza na Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu tarehe 30 Januari mwaka wa 2023, Ofisi iliamua kaulimbiu ya UNEA-6.
- Rais wa UNEA-6 alituma barua tarehe 6 Februari mwaka kwa Mawaziri wa Mazingira ili kuwajulisha kuhusu kaulimbiu.
Pitia sayansi, sera na hatua za kushughulikia changamoto za aina tatu za mazingira duniani: