Anwani: Kongamano la Kikanda la Bara la Afrika la NDCs 3.0
Tarehe: Octoba 7 - 9
Mahali: Kigali, Rwanda
Ripoti ya Pengo la Uzalishaji wa Hewa Chafu ya mwaka wa 2023 inaonyesha kiwango cha juu cha joto na kuonya kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweza kupelekea ongezeko la joto la kati ya nyuzijoto kati 2.5 na 2.9 zaidi ya viwango vya kabla ya viwanda katika karne hii, na kusisitiza umuhimu wa kushughulikia mabadiliko ya tabianchi kwa dharura.
Wahusika wanapaswa kuimarisha ahadi na kuzungumzia awamu ijayo ya Michango Inayoamuliwa na Taifa NDCs(NDCs 3.0), kufikia mwaka wa 2025 ili kuendana na malengo ya Mkataba wa Paris. NDC zijazo za 3.0, zinawakilisha wakati muhimu wa juhudi za kimataifa, na kutumika kama mwongozo wa mustakabali endelevu. Ni sharti ziwe zinazozoweza kutekelezeka, za wazi, na zilizo na uwezo wa kuvutia ufadhili.
Kwa koungezea, kwa kutoa mawazo kwa Tathmini ya Kimataifa GST ya kwanza, NDC mpya zinapaswa kuwa nguzo ya utekelezaji ulio na mabadiliko, zilizo na uwezo wa kuvutia ufadhili, kuimarisha uthabiti, na kurandana na mipango ya kitaifa na mikakati ya maendeleo. Zinapaswa kuungwa mkono na miongozo madhubuti za sera, mipango ya ufadhili, na kuonyesha jinsi nchi zitakavyoshughulikia mabadiliko ya tabianchi huku zitumia fursa hizo kukua na kuleta mabadiliko katika sekta mbalimbali.
Wakati nchi barani Afrika zinapojiandaa kwa awamu inayofuata ya NDCs, kuna fursa ya kipekee ya kuimarisha mikakati ya kushughulikia tabianchi ili kuwa na ahadi zaidi, na kutumia mafunzo kutoka kwa juhudi za awali za utekelezaji. Huku kanda hii ikisalia kuwa mojawapo ya maeneo yanayokumbwa na maafa zaidi duniani, na kushuhudia athari ghasi za kiwango cha juu za mabadiliko ya tabianchi na majanga ya kiasili kwa jamii zilizo hatarini na jamii zingine, nchi barani Afrika zimeendelea kutambua mara kwa mara kukabiliana na tabianchi kama kipaumbele muhimu cha sera katika eneo hili.
Jukwaa hili litaangazia jinsi matokeo ya COP28, hasa uamuzi wa GST, unavyoweza kuongoza michakato ya kitaifa ili kuimarisha ahadi za NDC za siku zijazo na kuchangia kwa maendeleo endelevu kwa kushughulikia na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa pamoja. Kupitia kuelimishana na kubadilishana mawazo, nchi katika kanda hii zitajadili kuhusu mbinu bora zaidi, changamoto na fursa, na kuimarisha masuluhisho na miundo bunifu ya ufadhili. Zana na mwongozo vitatolewa ili kutasaidia kujumuisha hatua na malengo mahususi wakati wa kuhakiki NDC.
Nchi mwenyeji:
Serikali ya Rwanda
Waandaaji
UNEP, UNDP, Ushirikiano wa NDC, kwa ushirikiano na sekretarieti ya UNFCCC
Taarifa zingine
Toleo la Habari - Mikutano ya kikanda inalenga kuongeza ahadi za nchi kabla ya awamu ijayo ya mipango ya tabianchi
Ajenda - Itakuwepo hivi karibuni
Tarehe - Mikutano ya Kikanda