Maelezo ya jumla
Lini: Novemba 4-8, 2024
Wapi: Cairo, Misri
Jisajili kwa WUF12 kabla ya tarehe 30 Oktoba.
Kongamano la Miji Duniani (WUF) huitishwa na Shririka la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-Habitat) kama kongamano kuu la kimataifa kuhusu ukuzaji wa miji endelevu. Katika mwaka wa 2024 katika kikao chake cha kumi na mbili (WUF12), Kongamano la Miji Duniani linarejea barani Afrika baada ya zaidi ya miaka 20 baada ya kuanzishwa kwake mjini Nairobi, Kenya, katika mwaka wa 2002.
Wawakilishi wa serikali za kitaifa, kikanda na serikali za mitaa, wasomi, wafanyabiashara, viongozi katika jamii, wapangaji miji na wawakilishi wa mashirika ya uraia watakuwa miongoni mwa maelfu ya watu wanaotarajiwa kuhudhuria WUF12 ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.
Maelezo ya jumla kuhusu hafla zinazoongozwa na UNEP katika WUF12. Jiunge nasi!