Lini: Septemba 4-8 , 2023
Wapi: Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC), Nairobi, Kenya.
Wiki ya Tabianchi barani Afrika (ACW) ni hafla ya kila mwaka ambayo huleta pamoja viongozi kutoka serikalini, mashirika ya biashara, mashirika ya kimataifa na mashirika ya uraia kutafuta njia za kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa huku wakikabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi. Mwaka huu, ACW 2023 itafanyika kuanzia tarehe 4 hadi 8 Septemba jijini Nairobi, Kenya, ikiongozwa na Serikali ya Kenya.
ACW 2023 itaandaliwa sambamba na Mkutano wa Kilele wa Tabianchi wa Afrika utakaoanza tarehe 4 hadi 8 Septemba jijini Nairobi, Kenya, pia utakaoongozwa na Serikali ya Kenya. Wakati wa ACS, viongozi barani Afrika watatakiwa kutoa ahadi kabambe na kujitolea kuzitekeleza ili kupitisha "Mwongozo wa Ahadi na Kujitolea Kuzitimiza."
Mojawapo ya wiki nne ya Kikanda ya Mazingira iliyofanyika mwaka huu, ACW 2023 inaimarisha kasi tunapoelekeaKongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi la COP 28mjini Dubai na kuhitimishwa kwa tathmini ya kwanza ya kimataifa, liyoundwa ili kupanga njia ya kutimiza malengo ya Mkataba wa Paris na kumakinikia michango ya kanda wakati wa kutoa tathmini ya Kimataifa.
ACW 2023 itawekwa katika makundi manne kimfumo, kila moja wapo ikiangazia mada mahususi:
- Mifumo na sekta ya nishati
- Miji, makazi ya mijini na vijijini, miundomsingi na uchukuzi
- Ardhi, bahari, chakula na maji
- Jamii, afya, riziki, na uchumi 2023.
ACW 2023 imeandaliwa na Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Benki ya Dunia, kwa msaada wa wabia wa kikanda: Umoja wa Afrika (AU), Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi wa Afrika (ECA)naBenki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Wawakilishi kutoka UNEP watapanga/kushiriki katika hafla kama ilivyoainishwa kwenye vitufe husika. Saa za eneo: Masaa ya Afrika Mashariki (EAT)
Pitia programu kamili ya ACW 2023.