Tarehe: Alhamisi, Novemba 7, 2024
Wakati: 7 am EST / 1 pm CET / 3 pm EAT
Tunapoelekea Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP29), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) litazindua rasmi Ripoti yake ya kila mwaka ya Kukabiliana Na Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Uzalishaji wa Gesi Chafu wakati wa mkutano na waandishi wa habari mtandaoni tarehe 7 Novemba mwaka wa 2024.
Msururu wa Ripoti ya UNEP ya Kukabiliana Na Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Uzalishaji wa Gesi Chafu inatoa kila mwaka tathmini ya kisayansi ya hatua zilizopigwa duniani za mikakati, ufadhili, utekelezaji wa juhudi za kukabiliana na hali. Pia inaangazia jinsi ya kuimarisha na kuendeleza juhudi za kukabiliana na hali za kitaifa na kimataifa na kutoa uchanganuzi wa kina wa masuala muhimu mahususi.