Lini: Oktoba 24, 2024
Ripoti ya Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu (EGR) ni msururu wa ripoti ya kitasisi inayotolewa na UNEP kila mwaka kabla ya mazungumzo ya kila mwaka kuhusu tabianchi. EGR hufuatilia pengo kati ya hali ya uzalishaji wa hewa chafu duniani inavyoelekea kwa kuzingatia ahadi za sasa zilizotolewa na nchi na hali inavyopaswa kuwa ili kudhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 2 na kulenga kufikia nyuzijoto 1.5 kwa kuzingatia malengo ya joto katika mkataba wa Paris. Kila toleo linaangazia mbinu za kupunguza pengo la uzalishaji wa hewa chafu, kushughulikia masuala mahususi na umuhimu wake kwa mazungumzo kila mwaka.
Ripoti hii mwaka huu inaendelea kusisitiza kuhusu umuhimu na uamuzi wa kuimarisha kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kujitokeza na ahadi za kimataifa zinazowiana malengo ya joto katika mkataba wa Paris katika awamu ijayo ya Michango Inayoamuliwa na Taifa, inayotarajiwa katika mwaka wa 2025.
Nyenzo