Lini: Machi 3 - 4, 2022
Wapi: Nairobi, Kenya
Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kilifuatiwa na kikao maalum kinachotambulika kana UNEP@50, kilichoendeshwa Machi 3 - 4, 2022, ili kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). Kikao hicho maalum kiliendeshwa chini ya kaulimbiu ya "Kuimarisha UNEP ili kutekeleza kipengele cha mazingira cha Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu."
UNEP@50 umekuwa wakati wa kutafakari kuhusu yaliyopita na kutazamia yajayo. Ilitoa fursa ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuchochea hatua za pamoja za kushughulikia changamoto tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibufu wa mazingira na bayoanuai, na uchafuzi na taka. Hakuna nchi au bara linaloweza kutatua changamoto hizi za kimataifa bila kusaidiwa. Lakini kila taifa lina wajibu muhimu wa kutekeleza kulinda watu wetu na sayari yetu.
Tafadhali pokea makala mwafaka na ratiba ya maadhimisho haya kwenye tabu zilizopo hapo juu
Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-5.2) kiliendesha mtandaoni na mjini Nairobi, Kenya, kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 2 Machi mwaka wa 2022. Punde tu baada ya UNEA-5.2, Kikao Maalum cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kiliendeshwa tarehe 3 na 4 Machi mwaka wa 2022, kilichotengewa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa katika mwaka wa 1972 (UNEP@50).
Hafla za kando wakati wa UNEA-5 ziliangazia “Kuimarisha juhudi za kushughulikia mazingira ili kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu" na maadhimisho ya Miaka 50 ya UNEP.
Tazama kalenda inayoingiliana na upeperushaji wa moja kwa moja hapa
Ajenda ya kwanza: Kikao cha ufunguzi
Ajenda ya pili: Kuidhinishwa kwa agenda na ratiba ya shughuli
Ajenda ua mda iliyofafanuliwa Kiingereza | Kiarabu | Kichina | Kifaransa | Kirusi | Kihispania Ilipakiwa Februari 14, 2022
Ratiba ya kazi Ilipakiwa Februari 14, 2022
Makala kuhusu hali ya UNEA 5.2 na UNEP@50 Ilipakiwa Februari 15, 2022
Ajenda ya tatu: Wasifu wa wawakilishi
Ujumbe wa mwisho kutolewa na Mkurugenzi Mtendaji Ilipakiwa Februari 14, 2022
Ajenda ya nne: Hotuba kutoka kwa wawakilishi
Iliyopitiwa - Maelekezo kuhusu utoaji wa hotuba na nchi na washikadau wakati wa kikao maalum cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa UNEP Ilipakiwa Februari 14, 2022
Ajenda ya tano: Uwasilishi wa ripoti na Mkurugenzi Mtendaji kuhusu uhusiano wa sera na sayansi
Hatua za utelezaji wa azimio 4/23 kuhusu kukuza uhusiano kati ya sera na sayansi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa: Kiingereza | Kiarabu | Kichina | Kifaransa | Kihispania | Kirusi Ilipakiwa Februari 14, 2022
Toleo la ripoti "Kutafakari kuhusu yaliyopita na kuwazia siku zijazo: mchango wa mazungumzo kuhusu uhusiano wa sera na sayansi": Kiingereza | Kiarabu | Kichina | Kifaransa | Kihispania | Kirusi Ilipakiwa Februari 15, 2022
Ajenda ya sita: Wasilisho la ripoti ya washikadau inayojulikana kama "UNEP Tunayoitaka"
Tamko la Pamoja Lililotolewa na Makundi Makuu na Washikadau kote Duniani Ilipakiwa Februari 21, 2022
Wasilisho la ripoti ya washikadau inayojulikana kama "UNEP Tunayoitaka" Ilipakiwa Februari 23, 2022
Ajenda ya saba: Majadilialo ya viongozi
Kikao maalum cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP@50)- Makala la Majadiliano ya Ngazi ya Juu Ilipakiwa Februari 14, 2022
Maelekezo kuhusu kushiriki kwa majadiliano ya viongozi Ilipakiwa Februari 14, 2022
Ajenda ya nane: Majadilialo ya washikadau anuai
Kikao maalum cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP@50)- Makala ya Majadiliano ya Ngazi ya Juu ya Washikadau Anuai Ilipakiwa Februari 14, 2022
Maelekezo kuhusu kushiriki kwa majadiliano ya ngazi ya juu ya washikadau anuai Ilipakiwa Februari 14, 2022
Ajenda ya tisa: Kukubali matokeo ya kisiasa ya kikao
Ajenda ya kumi: Kupitishwa kwa ripoti ya kikao na muhtasari wa Mwenyekiti
Ajenda ya kumi na moja: Kuhitimisha kikao
Rasimu ya majadiliano ya Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa la katika kikao chake maalum cha kwanza: maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Ilipakiwa Februari 14, 2022
Nchi Wanachama
Baraza la Inuit Circumpolar Council
Makundi Makuu na Washikadau