Dharura ya tabianchi ni matokeo ya moja kwa moja ya matumizi ya kaboni nzito ardhini na kwa kilimo, uchukuzi, michakato ya ujenzi na michakato ya viwanda na vyanzo chafuzi vya nishati. Bila mabadiliko makubwa kwa sekta hizi na bila kupunguza athari za hewa ya ukaa, kuna matumaini kidogo ya kulinda sayari dhidi ya athari mbaya za joto ulimwenguni.
Upeperushaji huu wa moja kwa moja utakufanya upate habari za hivi punde kutoka kwa Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi, linalojulikana kama Kongamano la Nchi Wanachama (COP29) Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) utakaofanyika nchini Baku, Azerbaijan.