Nairobi, Aprili 22, 2020 - katika juhudi za kukabiliana na janga la COVID-19, muungano ambao haukutarajiwa umebununiwa ili kuzindua “Earth School,” inayotoa makala ya kiwango cha juu bila malipo ili kuwasaidia wanafunzi, wazazi na walimu kote duniani wakati huu wanaposalia nyumbani. Mpango ulioanzishwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) kwa ushirikiano na TED-Ed, "Earth School" ni safari ya siku 30 inayofanya wanafunzi “Kutalii” dunia halisi.
Makala yaliyotungwa ya "Earth School" yanajumuisha video, makala ya kusomwa na mazoezi — ambayo yatatafsiriwa kwa lugha 10 — ili kuwezesha wanafunzi kuelewa masuala ya mazingira na kutambua wanachoweza kufanya. Huu ni mradi kubwa mno kwenye historia ya UNEP wa kutoa mafunzo mtandaoni bila malipo kwenye Mtandao wa TED-Ed’.
Kwa mjibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), zaidi ya wanafunzi bilioni 1.5 wameathiriwa naufungaji wa shule kutokana na COVID-19 . Janga hilo limeathari afya, uchumi na elimu. Wakati ambapo watu hawawezi kukutana ana kwa ana, kuna haja kubwa ya kuwa na elimu ya kimataifa ya sayansi.
Hii ndiyo sababu iliyopelekea UNEP na TED-Ed — kwa ushirikiano na wabia wengine kama vile Shirika la National Geographic, WWF na UNESCO — kuungana na kuzindua "Earth School" kwa mda upatao majuma mawili. Programu iliyoundiwa wanafunzi wa umri wa kati ya miaka 5 na 18, itachukua siku 30 bila kujumuisha wikendi. Mda huu unajumuisha Siku ya Dunia na Siku ya Mazingira Duniani itakayojiri tarehe 5 mwezi wa Juni. Siku hiyo itakayoadhimishwa mwaka huu chini ya kaulimbiu ya Wakati wa Mazingira.
TED-Ed huunda vipindi vinavyotolewa bila malipo kutoka kwa video zinazohusu chochote kile kuanzia kwa wanyama na mabadiliko ya tabianchi hadi kwa mashamba yanayopatikana chini ya maji. Idara ya Elimu ya TED, iliyo na maktaba ya maelfu ya vipindi vilivyoundwa na walimu 500,000 kutoka pembe nne za dunia uhudumia watu wa umri wowote na somo lolote.
Kila somo limechaguliwa kwa makini na jopo la wataalamu na linaweza kunufaisha watu walio na umri wowote. Kila mojawapo ya somo hilo lina majaribio yanayotoa mafunzo zaidi kuhusu mazingira. Mbali na makala yanayoandaliwa na TED-Ed, "Earth School" itajumuisha video kutoka katika mashirika maarufu ya uandishi wa habari kama vile National Geographic, PBS LearningMedia na BBC ikiwa na nia ya kuwawezesha wanafunzi watakaoshiriki kuitunza sayari yetu.
“Mabilioni ya wanafunzi hawako shuleni sasa kutokana na COVID-19. Lakini masomo ni sharti yaendelee. COVID-19 imeonyesha jinsi ambavyo viumbe wote wanavyotegemeana hapa duniani," alisema Katibu Mtendaji wa UNEP,Inger Andersen. "Nina furaha kuwa UNEP, kwa ushirikiano na TED-Ed na wabia wengine, wanazindua "Earth School". Kujifundisha kuhusu dunia halisi ni muhimu ili kuboresha hatima ya siku zijazo na kuwa na mustakabali endelevu."
"Nyakati hizi ngumu zinaonyesha jinsi ambavyo ni muhimu kwa vijana kushirikishwa na dunia halisi na kuelewa sayansi," alisema Vicki Phillips, naibu wa raisi mtendaji na afisa mkuu wa elimu wa Shirika la National Geographic Society. "Tunafurahi kuungana na mashirika yanayoheshimiwa kama vile UNEP na TED-Ed ili kujenga utamaduni wa kudadisidadisi mambo na kufanya watu kuihurumia dunia. Haijalishi waliko wanafunzi — hata ikiwa ni majumbani kwao, kuchungulia dirishani, au matembezi mafupi kuelekea kwa maeneo jirani."
"Ijapokuwa hawatoki nyumbani, mradi huu unaonyesha ya kwamba wanafunzi, wazazi na walimu kote duniani wanaweza kuendelea kusoma sayansi na kushirikiana. "Earth School" ni ushirikiano wa walimu wengi walio na talanta na wabia wa kipekee kutoka pembe zote za dunia. Hii ndiyo sababu tuna furaha mno na tunajivunia kuona mradi huu ukinufaisha wanafunzi kote ulimwenguni walio na kiu na ambao watapigania masuala ya mazingira katika siku zijazo. Jukwa hili litafungua mlango kwa mafunzo kuhusiana na mali ghafi na mazingira. Kila kipindi kinajumuisha mazoezi na shughuli za kupendeza ambazo wanafunzi wanaweza kushiriki na hata kushirikiana, alisema Logan Smalley, Mkurugenzi mwanzilishi wa mradi wa TED wa vijana na elimu, TED-Ed.
Vipindi viliundwa na wataalamu wa elimu ya mazingira ikiwa ni pamoja na Kathleen Usher Ph.D, Jessie Oliver na Juliane Voss, walioshirikiana na wachangiaji zaidi ya 100 wakati wa kuunda "Earth School". Mradi huu unaunga mkono SDG 4.7 na Muongo wa Matokeo na utatoa mchango wake kwa Global Education Coalition iliyozinduliwa na UNESCO mwezi jana ili kuwezesha serikali, wabia wa teknolojia na viongozi katika sekta ya elimu kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kusoma. Kama mshirika katika muungano huu, UNEP itafuatilia jinsi ambavyo makala haya yanaweza kufanyiwa marekebisho ili yaweze kufikia wanafunzi ambao hawana intaneti.
Washirika ambao wamekubali kufadhili mradi huu ni: BBC Ideas, Basel, Rotterdam and Stockholm Conventions, Bill Nye the Science Guy, Conservation International, CEE, Earth Day Network, Earth Challenge 2020, Environment Online (ENO), GeSI, International Olympic Committee (Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki), IUCN, Institute for Planetary Security(Taasisi ya Usalama wa Sayari), Junior Achievement, Learning in Nature, Littlescribe, Minecraft, National Geographic Society, Ocean Wise, Only One, Royal Geographic Society, SciStarter, Sitra, TAT, TED-Ed, The Nature Conservancy, UN Convention on Biodiversity, UN SDSN / TRENDS, UN Technology Innovation Lab (Maktaba ya Utafiti ya Umoja wa Mataifa), UNCCD, UNDP, UNEP, UNESCO, UNFCCC, UN Food and Agriculture Organization (Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula), University of Pennsylvania (Chuo Kikuu cha Pennsylvania), Vult Labs, World Association of Girl Guides and Girl Scouts (WAGGGS), World Organization of the Scout Movement (WOSM), Wild Immersion and WWF.
MAKALA KWA WAHARIRI
Kuhusu Shirika la Mazingira Duniani
UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira. Hutoa uongozi, na kuwahimiza wabia kufadhili miradi ya kutunza mazingira kwa kushawishi, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuboresha maisha yao bila kudhuru yale ya vizazi vijavyo.
Kuhusu TED-Ed
TED-Ed ni mradi wa TED wa vijana na elimu. Dhima ya TED-Ed’s ni kuchochea na kujivunia mawazo yanayotolewa na walimu na wanafunzi kote duniani. Chochote tunachokifanya ni kwa ajili ya kujwezesha masomo kuendelea — kuanzia na kuwa na maktaba inayokuwa kila uchao iliyo na video zilizohuishwa , hadi kwa kutoa jukwaa la kimataifa kwa walimu ili kujiundia vipindi vyao, hadi kuwasaidia wanafunzi walio na kiu cha kusoma kote duniani kufikisha TED shuleni kwao na kujifunza kuhusu jinsi ya kuwasilisha makala ya elimu, hadi kwa kusherehekea viongozi wabunifu wanaofanya kazi na TED-Ed’s wanaojumuisha zaidi ya walimu 500,000. TED-Ed imekuwa kutoka wazo muhimu linaloweza kuenezwaa na kuwa jukwaa la elimu lillilotuzwa kwa kuhudumia mamilioni ya walimu na wanafunzi kote duniani kila wiki.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na
Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP, +254717080753
Melody Serafino, TED Press