- Mashua ya kwanza duniani kuundwa kutoka kwa taka ya plastiki inatoa suluhu kwa vitu vilivyowahi kutumika kutumika tena na kutoa wito wa kukomesha matumizi yasiyohitajika ya plastiki inayotumika tu mara moja kwenye ukanda huo.
- Safari ya Ziwa Victoria - itakayoanza tarehe 4 mwezi wa Machi - inaunga mkono ushirikiano wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki.
- Ziwa Victoria, Ziwa kubwa mno barani Afrika lililo na maji safi, linakabiliwa na changamoto nyingi za mazingira na za jamii ambazo zinaweza kuathiri watu milioni 40 wanaoishi katika eneo hilo.
Kisumu, Machi 4, 2021 - Flipflopi, mashua kubwa mno duniani ya kwanza kutengenezwa kwa asilimia 100 kutoka kwa plastiki iliyowahi kutumika, inashirikiana na Kampeni ya Bahari Safi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kwa mara ya pili, mara hii ikianzia safari yake kwenye mfumo mkubwa mno wa ekolojia wa maji safi barani Afrika - Ziwa Victoria. Safari hiyo inalenga kupitisha ujumbe muhimu kwa jumuia ya Afrika Mashariki kuhusu umuhimu wa kukomesha matumizi yasiyohitajika ya plastiki inayotumika tu mara moja kwenye ukanda huo.
Ziwa Victoria, linalosaidia watu wa Afrika Mashariki milioni 40 , linadhihirisha madhara mabaya mno ya shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabianchi, kwa kujumuisha mambo mengine yanachangia uchafuzi mkubwa wa maji na kuhatarisha afya na kipato cha wanajamii.
Utafiti wa hivi karibuni ulikadiria kuwa 1 kati ya samaki 5 kwenye Ziwa Victoria walikuwa wamemeza plastiki. Utafiti mwingine wa hivi karibuni ulionyesha kuwa kuna chembechembe za plastiki chini ya maji katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria. Plastiki hiyo inatokana na tatizo la taka kutoka na mfumo wa 'nunua-tumia-tupa' wakati bindaa zinapotengenezwa, kununuliwa. kutumiwa kwa mda mdogo, kisha kutupwa.
Mradi wa Flipflopi unaonyesha matumizi mengineyo ya taka ya plastiki na uwezekano wa kutumia bidhaa tena na tena. Kwa kipindi cha majuma matatu, Flipflopi itasafiri kutoka mji wa Kisumu nchini Kenya hadi kwa maeneo mbalimbali nchini Uganda na Tanzania, huku ikihamasisha watu na kushawishi jamii kutumia mbinu itakowezesha taka kutumika tena ili kukomesha matumizi ya plastiki.
"Ziwa hili, Nam Lolwe, ni muhimu kwangu. Ni sharti sisi sote tuone umuhimu wake. Kuwekeza kwenye utafiti na kukuza uwekezaji wa uchumi wa bahari, kuboresha hali ya Ziwa Victoria na mazingira ya maeneo ya mitoni kwa kuhakikisha kuwa uwekezaji unayajali mazingira tangu unapoanza ndiyo sehemu ya mambo ya mambo ninayoyapa kipaumbele", alisema Gavana wa Kaunti ya Kisumu nchini Kenya Anyang’ Nyong’o.
"Janga la COVID-19 linaonyesha umuhimu wa kushughulikia changamoto anuai za mazingira, ambazo zinaweza tu kutatuliwa kupitia ushirikiano wa kikanda na wa kimataifa kupitia kukubaliana kuhusu masuala kama vile matumizi ya plastiki inayotumika tu mara moja na mabadiliko ya tabianchi," alisema Joyce Msuya, Naibu wa Katibu Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). "Flipflopi ni mfano mzuri Barani Afrika wa hali halisi ya uchumi ulio na bidhaa zinazoweza kutumika tena na tena; tunajivunia kuona ikianza safari hii mpya ya kuzunguka Ziwa Victoria, rasimali inayotumiwa na wengi na tunahohitaji kufanya kila tunachoweza kufanya kuitunza.
Safari ya Flipflopi kwenye Ziwa Victoria itahusisha vituo kadhaa vya kusimama ili kujadiliana na viongozi katika jamii, wanamazingira, wafanyabiashara wakuu na watungasera, ili kuonyesha matumizi mbadala ya taka ya plastiki na mbinu nyinginezo za kutumia taka tena kama wito wa kukomesha matumizi ya plastiki inayotumika mara moja tu.
Flipflopi ilitengenezwa ili kuonyesha ulimwengu kuwa inawezekana kuunda bidhaa muhimu kutokana na taka ya plastiki, na kuwa plastiki inayotumika mara moja tu aihitajiki," alisema Ali Skanda, mwanzilishi mwenza wa mradi wa Flipflopi na muundaji wa mashua iliyotengenezwa kutoka kwa plastiki iliyotumika. Kwa kuzunguka Ziwa Victoria, tunalenga kuwachochea watu kubuni bidhaa za plastiki na kukumbatia masuluhisho ya kutumia bidhaa tena ili kukuza biashara isiyochafua mazingira huku plastiki ikiondolewa kwenye mazingira. Kwa ushirikiano wa jamii katika eneo la Ziwa Victoria, tunatumahi tutahamasisha na kutoa masuhisho bunifu ya kukomesha uchafuzi wa plastiki na kukuza uchumi bila kuchafua mazingira katika eneo la Afrika Mashariki."
Flipflopi ni mfano wa masuluhisho bunifu yanayowezesha vitu vilivyotumika kutumika tena katika ngazi ya kitaifa ili kukabiliana na changamoto ya plastiki. Mjini Kisumu kwenye fukwe za Ziwa Victoria, CIST Africa hutengeneza vieuzi kutoka kwa mmea wa hyacinth.
Wavumbuzi kama vile Sanergy wanatumia taka ya ogani kutengeneza mbolea ya kunyunyuzia mimea, lishe ya mifugo na mabloku ya kupikia. Nchini Uganda, wanawake walianzisha kampuni ya Reform Africa hutumia taka ya plastiki kutengeneza mikoba ya kudumu isiyoingiza maji, na kuwezesha watoto wa vijijni kuwa na begi za kwenda shuleni bila malipo. Nchini Tanzania, wasanii waliungana wanaojulikana kama ‘Made by Africraft’ wanasaidia vijana na watu wasiokuwa na ajira kwa kuunda bidhaa zinazowapa kipato.
Flipflopi, Kampeni ya Bahari Safi na wabia wanalenga kufanya maonyesho ya uvumbuzi usiochafua mazingira wanapozunguka Ziwa Victoria, na kuhamasisha jamii na mashirika ya biashara kuchukua hatua za kukabiliana na plastiki.
Kama sehemu ya safari, safari ya Flipflopi itatoa wito wa kukomesha matumizi ya plastiki inayotumika mara moja kwenye ukanda huo.
Mradi wa Flipflopi unafadhiliwa na wabia mbalimbali ikijumuisha serikali kuu za Kenya, Uganda na Tanzania, UNEP, Ofisi ya Uingereza ya Mambo ya Nje ya Jumuiya ya Madola ya na Maendeleo(FCDO), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Muungano wa Ulaya, UN Live, na sekta binafsi, inayojumuisha taasisi ya sheria yaAnjarwalla and Khanna.
MAKALA KWA WAHARIRI
Kuhusu Flipflopi
Flipflopi ni mradi wa uchumi unaotumia bidhaa tena na tena unapopatikana katika eneo la Afrika Mashariki. Unalenga kukuza dunia isiyokuwa na plastiki inayotumika tu mara moja. Huonyesha matumizi mbadala ya taka ya plastiki na uwezekano wa kukuza uchumi unaotumia bidhaa zaidi ya mara moja barani Afrika kupitia programu za kuelimisha, matumizi ya plastiki iliyotumika kuunda bidhaa na ushughulikiaji wa taka ‘innovation hubs’ na programu za uhamasishaji na usimamiaji.
Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)
UNEP in mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira ulimwenguni. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.
Kuhusu Kampeni ya UNEP ya Clean Seas (Bahari Safi)
Kampeni iliyozinduliwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa katika mwezi wa Februari mwaka wa 2017, Kampeni ya Bahari Safi ni mradi unaoshirikisha serikali, mashirika ya biashara na wananchi kwa lengo la kukomesha matumizi yasiyohitajika ya plastiki inayotumika tu mara moja na kuwezesha mbinu za kukuza uchumi unatumia bidhaa tena na tena. Katika mwaka wa 2021, kampeni inatoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za dharura za kukabiliana na changamoto za mazingira hasa vyanzo vyake hadi baharini.
Kufikia sasa, nchi sitini na mbili kote ulimwenguni zimejiunga na kampeni hii. Hali hii inapelekea kampeni ya Clean Seas kuwa kubwa zaidi, kwa kuunganisha nchi mbalimbali ulimwenguni zinazojitolea kukomesha uchafuzi wa plastiki baharini. Kujitolea kwa nchi wanachama kumefikia zaidi ya asilimia 60 ya nchi zilizo na pwani duniani. Nchi nyingi zimetoa ahadi ya kupunguza au kukomesha matumizi ya plastiki inayotumika tu mara moja katika jamii, au kuwekeza zaidi ili kuunda bidhaa zinatokana na plastiki.
Kuhusu Muungano wa Ulaya
Muungano wa Ulaya ni muungano wa kisiasa na kiichumi ulio na nchi wanachama 27. Kwa jumla, Muungano wa Ulaya na Nchi Wanachama ni wabia wakuu wa maendeleo nchini Uganda. Muungano wa Ulaya hukuza utawala bora, sheria, demokrasia na haki za binadamu nchini Uganda. Muungano wa Ulaya ni mbia mkuu wa kimataifa wa maendeleo na biashara nchini Uganda, huku ukifanya kazi ili kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira na kuwekeza kwa tabianchi nchini Uganda ili kubuni nafasi za kazi.
Kuhusu Ofisi ya Jumuia ya Madola na Maendeleo ya Uingereza
Serikali ya Uingereza kupitia kwa ofisi ya Jumuia ya Madola na Maendeleo ya Uingereza Katika mwezi wa Novemba, Uingereza itakuwa mwenyeji wa kongamano la UN la Mabadiliko ya tabianchi COP26, mjini Glasgow na Italia. Hii ni fursa kwa dunia kujitolea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kutozalisha gesi ya ukaa katika siku zijazo. Uingereza inaishirikiana na Afrika Mashariki kutunza mazingira ya maeneo ya baharini, ikijumuisha kupunguza uchafu wa plastiki, ili kuwezesha vizazi vijavyo kujiimarisha vyema kabla ya COVID-19.
Kuhusu Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD)
Agence Française de Développement (AFD) hutoa ufadhili kwa umma ili kukuza na kuwezesha dunia kuwa na haki na maendeleo endelevu. Kama shirika linalotoa misaada nje ya nchi ili kuwezesha maendeleo endelevu na kufanya uwekezaji, sisi na wabia wenza hushirikiana kupata masuluhisho, kwa ushirikiano na kwa manufaa ya watu walio Kusini mwa dunia.
Vikosi vya AFD vinajishughulisha na miradi zaidi ya 4,000 nyanjani - kwenye nchi nje ya Ufaransa zilizo chini ya Ufaransa na nchi zingine 115. Wanalenga kukuza afya, elimu na usawa wa jinsia, na wanafanya kazi kutunza rasilimali zinazomilikiwa kwa pamoja — amani, bayoanuai, na mazingira dhabiti.
Kuhusu Makavazi ya Umoja wa Mataifa (‘UN Live’)
UN Live ni taasisi inayojitegemea iliyobuniwa ili kuunganisha watu kote ulimwenguni na kazi na maadili ya Umoja wa Mataifa, kwa kuongeza mno idadi ya watu wanaofanya kazi kuyafikia malengo yake. Inalenga kuwajengea uwezo mabilioni ya watu kote ulimwenguni kuchukua hatua na kusaidia kuwa na dunia endelevu isiyobagua na inayotupa matumaini. Kama makavazi mapya, inatumia uwezo wa utamaduni kufikia watu kote ulimwenguni na kuwaunganisha ili kushirikiana kuleta mabadiliko.
Rasilimali media
Kuna mkusanyiko wa picha na video hapa na hapa
Kwa taarifa zaidi au kwa mahojiano, tafadhali wasiliana na:
Mohamed Atani, Msimamizi wa Mawasiliano na Uhamasishaji Barani Afrika, UNEP, mohamed.atani@un.org – Nambari ya simu 0727531253
Pauline Akolo, Mawasiliano na Uhamasishaji Barani Afrika, UNEP, pauline.akolo@un.org - Nambari ya simu 0790219954
Ziwa Victoria, Ziwa kubwa mno barani Afrika lililo na maji safi, linakabiliwa na changamoto nyingi za mazingira na za jamii ambazo zinaweza kuathiri watu milioni 40 wanaoishi katika eneo hilo. Safari ya Ziwa Victoria - itakayoanza tarehe 4 mwezi wa Machi - inaunga mkono ushirikiano wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki.