- Mfumo wa Tahadhari na Kushughulikia Methani ulitoa arifa 1,200 kuhusu uzalishaji mkuu; ni 15 tu zilizoshughulikiwa
- Uzuiaji wa uvujaji wa methani nchini Algeria, Nigeria unashughulikia uzalishaji wa hewa chafu sawa na takriban kiwango cha magari milioni moja kila mwaka.
- Kampuni 140 za mafuta na gesi zimejitolea kupima na kupunguza uzalishaji wa methani chini ya OGMP 2.0
Baku, 15 Novemba 2024 – Mfumo wa teknolojia ya kiwango cha juu unaotambua uvujaji mkuu wa methani umewasilisha arifa 1,200 kwa serikali na makampuni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lakini ni asilimia moja tu ya arifa hizo zilishughulikiwa kulingana na data mpya ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).
Licha ya ahadi chini ya Ahadi ya Kimataifa ya Methani ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kwa asilimia 30 kufikia mwaka 2030, Jicho kwa Methani: Haionekani lakini haimainishi haiko inaangazia kwamba tahadhari ya viputo vya methani kutoka Mfumo wa Kuangazia na Kushughulikia Methani (MARS), sehemu ya Uchunguzi wa Kimataifa waUzalishaji wa Methani (IMEO) wa UNEP, ni kiwakilishi cha fursa ambayo haijatumiwa ya kushughulikia mabadiliko ya tabianchi haraka.
Methani angani ni kichocheo cha pili kikuu cha ongezeko la joto la anthropojeniki duniani baada ya kaboni dioksidi (CO2) na ina nguvu zaidi ya mara 80 kuliko CO2 kwa kipindi cha muda mfupi. Uzalishaji wa methani duniani ni sharti upunguzwe kwa asilimia kati ya 40 na 45 kufikia mwaka wa 2030 ili kufikia lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzijaoto 1.5 kwa gharama nafuu. Ila sayansi ya hivi karibuni inaonyesha kuwa viwango vya methani angani vinavyoongezeka kwa kasi ya juu katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.
"Ili kuweza kudhibiti ongezeko la joto duniani, uzalishaji wa methani ni sharti ushuke, na ushuke haraka," Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP alisema. "Sasa tuna mfumo uliothibitishwa wa kutambua uvujaji mkuu ili uweze kusimamishwa haraka - mara nyingi kwa ukarabati rahisi. Kwa kweli tunazungumzia kunyosha mambo zaidi katika hali zingine.
“Serikali na kampuni za mafuta na gesi ni sharti ziache kuzungumzia tu changamoto wakati yapo. Badala yake, wanapaswa kutambua fursa muhimu iliopo na kuanza kushughulikia arifa kwa kuziba uvujaji ambao unamwaga methani inayoongeza joto angani. Zana ziko tayari, malengo yameshawekwa - sasa ni wakati wa kuchukua hatua."
Kuthibitisha umuhimu wake
Ingawa kushughulikia methani kunapaswa kuimarika haraka, kuna mifano ya mataifa na makampuni yanayoshughulikia hali - na kuthibitisha umuhimu wa masuluhisho yanayotokana na data kama vile MARS. Katika mwaka wa 2024, IMEO ilithibitisha hatua za kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kutokana na uvujaji mkuu nchini Azabajani na Marekani.
Nchini Algeria na Nigeria arifa na ushirikiano wa MARS ulisababisha hatua za moja kwa moja kutoka kwa serikali na makampuni ya mafuta na gesi zakushughulikia uvujaji mkuu wa methani. Katika kisa cha Algeria, ambayo ilishuhudia uvujaji wa methani uliofanyika kwa miaka kadhaa, uzalishaji unaoepukwa kila mwaka ni sawa na kiwango cha magari 500,000 kuondolewa barabarani. Katika kisa cha Nigeria, uvujaji wa miezi sita ulitoa methani sawa na kiwango cha magari 400,000 yakiendeshwa kwa mwaka mmoja na hali iliweza kurekebishwa chini ya wiki mbili kwa kubadilisha tu vifaa vibovu.
Mbali na kushughulikia uzalishaji mkuu wa hewa chafu unaoonekana kutoka angani, mifumo hii ipo kwa tasnia kudhibiti kiwango chake cha methani. Ushirikiano wa Mafuta na Gesi ya Methani 2.0 (OGMP 2,0) wa UNEP, mpango wa makampuni ya mafuta na gesi wa kupima na kupunguza uzalishaji wao wa methani. OGMP 2.0 iliongeza wanachama 20 katika mwaka uliopita, na kukua hadi wanachama 140 wanaojumuisha zaidi ya asilimia 40 ya uzalishaji wa hewa chafu duniani.
Mwaka wa 2024 pia ni mwaka wa kwanza kwa OGMP 2.0 kuanza kutoa "ripoti yake ya Kiwango cha Dhahabu" kwa makampuni ambayo yanaripoti kuhusu uzalishaji wake wa hewa chafu katika viwango vya juu zaidi vya ubora wa data. Kufikia mwaka wa 2024, kampuni 55 zimefanikiwa kuripoti kwa Kiwango cha Dhahabu. Kuhamishia kampuni zote katika sekta zote kwenye ripoti ya uzalishaji wa OGMP 2.0 ya Kiwango cha Dhahabu ni muhimu ili kulenga ipasavyo upunguzaji na data kulingana na kipimo na kufuatilia utendakazi dhidi ya ahadi za kupunguza uzalishaji wa hewa chafu, kama vile Mkataba wa Uondoaji wa Hewa ya Ukaa katika Mafuta na Gesi uliotangazwa katika COP28.
Mipango mipya
IMEO pia imezindua jukwaa la data ya Jicho kwa Methani ili kuibua hatua zaidi. Jukwaa hili linatoa data wazi, ya kuaminika na inayoweza kutekelezeka kuhusu uzalishaji wa methani duniani ili kuendesha hatua za kukabiliana na athari za methani kwa ufanisi na serikali na makampuni, huku likitoa data iliyo ya wazi na ya kuaminika kwa mashirika ya uraia na vyombo vya habari.
IMEO pia inaimarisha kazi yake kuhusu uzalishaji wa methani kutoka vyanzo vingine kupita Mpango wa Methaie ya Chuma. Uzalishaji wa methani kutoka kwa makaa ya mawe yanayotumika katika utengenezaji wa chuma huwakilisha wastani ya asilimia 30 ya athari za chuma kwa mazingira kwa mda mfupi. Uchafuzi huu unaweza kupunguzwa kwa takriban asilimia moja ya bei ya chuma.
Mpango huu mpya unatoa mfumo wa kupunguza athari kwa mazingira kutoka sekta ya chuma wakati tasnia inapoanza kutumia nishati isiyochafua mazingira. MARS inapanuliwa ili kushughulikia uzalishaji wa makaa ya mawe na kutambua fursa zaidi za kukabiliana na hali.
Nukuu za ziada:
Kamishna wa Nishati wa Umoja wa Ulaya, Kadri Simson: "Uzalishaji wa methani ni kichocheo kikuu cha mabadiliko ya tabianchi, na EU imedhamiria kupunguza uchafuzi huu kwa asilimia 30 kufikia mwaka wa 2030. Takwimu za kuaminika ni muhimu ili kufikia malengo ya Ahadi ya Kimataifa ya Methani. Kama masoko ya nje, kama vile Umoja wa Ulaya, yanavyozidi kuhitaji nishati isiyochafua mazingira na kuhusu uzalishaji wa hewa chafu, IMEO ya UNEP inatoa data inayowezesha kufanya maamuzi na kupelekea uwajibikaji. Kwa hivyo nakaribisha ripoti ya kina iliyozinduliwa leo."
Waziri wa Mazingira wa Nchina Mbunge, Wizara ya Masuala ya Kiuchumi na Kushughulikia Mazingira ya Ujerumani, Stefan Wenzel: "Methani ni gesi ya ukaa ilio na nguvu zaidi. Hata hivyo, ina faida moja: ni rahisi zaidi kuipunguza kuliko CO2. Inatubidi kutilia maanani. Tunapofanya kazi kufikia malengo yetu makuu ya kushughulikia tabianchi, tunahitaji kila zana inayopatikana ili kupunguza uzalishaji wa methani kwa ufanisi. IMEO ya UNEP inapelekea maarifa yanayotokana na data ili kuwezesha hatua za haraka. Ujerumani imejitolea kuunga mkono hatua hizi bunifu, ambazo zinaonyesha kwamba tukiwa na data bora, tunaweza kufikia upunguzaji mkubwa wa uchafuzi na kupelekea kupiga hatua za kushughulikia tabianchi. Sasa ni wajibu wa wachafuzi wa mazingira kuepuka methani inapowezekana. Mbinu za kufanya hivyo zinapatikana. Ni zaidi kuliko ilivyoonyeshwa kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi yanayoendelea."
Mkurugenzi Mkuu, Baraza la Nigeria la Mabadiliko ya Tabianchi, Dkt Nkiruka Maduekwe: "Kwa Nigeria, kuchukua hatua kuhusu uzalishaji wa methani sio tu kuhusu uwajibikaji wa mazingira, lakini pia ni kuhusu afya ya eneo na maendeleo endelevu. Nigeria inajivunia kushirikiana na IMEO ya UNEP na Tume ya Ulaya ya utafiti wa kisayansi ili kupima uzalishaji wa hewa chafu katika sekta mbalimbali na kuwezesha hatua za kushughulia methani nchini Nigeria. Tumejitolea kutumia maarifa haya kuendeleza malengo yetu ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu na kutimiza ahadi yetu kama Mpiganiaji wa Ahadi ya Kimataifa ya Methani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Methani Duniani, Marcelo Mena: "Data na uwazi unaotolewa na IMEO ya UNEP ni muhimu sana kwa uwajibikaji na kuchukua hatua. Kituo cha Methani Duniani kinaunga mkono mpango huu, na kutambua wajibu muhimu wa data za kuaminika za kufanyia kazi ahadi kuwa upunguzaji wa hewa chafu. Tunahitaji kuimarisha juhudi hizi na kuwa na uadilifu na uthibitishaji huru wa madai ya kukabiliana na hali."
MAKALA KWA WAHARIRI
Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)
UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Kitengo cha Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa