08 Oct 2020 Toleo la habari Youth, education & environment

UNEP na Bunge la Dini Duniani wazindua kitabu kipya kuchochea uchukuaji wa hatua za kutunza mazingira

Nairobi/Chicago, Octoba 8, 2020 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Bunge la Dini Duniani leo wamezindua kitabu kipya,"Faith for Earth — A Call for Action", kinachotoa fursa kwa wasomaji wake kusoma mada mbalimbali kuhusiana na historia na uanuai wa mafundisho ya kidini na uhamasishaji wake wa kutunza mazingira.

Kitabu kinachopatikana mtandaoni na toleo lililochapishwa leo wakati wa Kongamano la "Faith for Nature Global Conference", (tarehe 4 hadi 8 mwezi wa Octoba mjini Skálhol, nchini Iceland.

Kitabu hicho kinaelezea kwa mapana utamaduni wa dini na matokeo ya utafiti wa kisayansi yanayotuwezesha kuelewa na kutafakari kuhusu mwelekeo wa dini kuhusu mazingira endelevu duniani. Kuna kauli zinazoeleweka kwa urahisi kutoka kwa maandiko ya kidini na kwa viongozi wa kidini.

Kinasema kuwa kutunza Sayari, kuboresha mifumo ya ekolojia, kukomesha uchafuzi, na kuhakikisha kuwa mazingira yako katika hali nzuri kwa manufaa ya vizazi vijavyo ni sehemu ya maadili na ni sehemu ya uwajibikaji wa kiroho. Tukiwa na majumba ya kuabudia zaidi ya milioni mia moja kote duniani, kukumbatia kanuni za majengo yasiyochafua mazingira ni ishara tosha ya kujitolea ili kuwa na maendeleo endelevu.

"Changamoto yetu si kuwa hatufahamu tunachohitaji kufanya—ni mda tunaotumia kufanya tunachohitaji kufanya. Tunakimbizana na mda na tunahitaji kujitolea kwa wanasasia, ubunifu, kutobagua, kuvuliana, maadili, ufadhili na ubia," alisema Iyad Abumoghli, Mkurugenzi wa UNEP wa "Faith for Earth".

"Tunatoa wito kwa wote – nchi, miji, sekta ya binafsi, watu binafsi, na mashirika ya kidini kujiunga na vuguvugu la kimataifa linalojumuisha dini mbalimbali linaloendelea kuleta watu pamoja ili kutunza na kuhifadhi viumbe duniani", aliongezea. "Tuna matumaini kuwa kitabu hicho kitaelimisha watu na kuwachochea kujifunza zaidi kuhusu sayari yetu na kuwafanya kujiunga na vuguvugu linaloendelea kua na kuleta watu pamoja ili kutunza na kuhifadhi viumbe duniani."

"Watu wengi siku hizi hawafahamu mafundisho ya kidini kuhusu kuyajali na kuyatunza mazingira, hasa mafunzo kuhusu tamaduni wasizosifahamu," alisema Kusumita P. Pedersen, mwandishi wa sehemu ya dini wa kitabu hiki. "Faith for Earth ni kitabu kinachoweza kutumiwa kuelimisha, kuwasilisha ujumbe, na kuhamasisha kupitia njia rasmi na zisizo kuwa za rasmi."

David Hales, Mwenyekiti wa Climate Action kwenye bunge hilo na ayeandika sehemu ya mazingira katika kitabu hicho, anasema kuwa miongo ijayo "itaathiriwa na madili tunayozingatia sasa."

"Kwa kipindi cha nusu ya karne, tumeweza kufahamu kuwa maamuzi tunayofanya yatakuwa na athari kubwa kwa vizazi vijavyo, kwa wanetu na kwa wajukuu wetu," alisema.

"Sisi ndio wa kwanza katika historia ya binadamu tulio na fursa ya kuhakikisha tuna jamii endelevu yenye haki," aliongezea. "Kutambua furusa tulizonazo, ni sharti tuwajibike — sio tu kuchagua kuwajibika — ila kujitolea kujenga uwezo — katika ngazi zote — kuelewa vifaa, na matokeo halisi na ya kimaadili kutokana na uamuzi wetu. Uamuzi wetu utaathiri mustakabali wa sayari yetu."

Faith for Earth ni kitabu kilichoandikwa na kuhaririwa baada ya kushauriana na viongozi kadhaa wa dini na wasomi wa dini, na kuchangunuliwa kisayansi na wakurugenzi wa UNEP, Muungano wa Wanasayansi Wanaojali (Union of Concerned Scientists), na Kituo cha Mawasiliano kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi cha Chuo Kikuu cha George Mason.

Toleo linalopatikana mtandaoni la Faith for Earth linapatikana bila malipo na unaweza kulipakua kwenyeTovuti ya UNEP ya Faith for Earth na kupitia kwa tovuti ya Parliament’s Climate Action, na linajumuisha linki za makala tendi, rasilimali, na taarifa zinazopatikana papo hapo kuhusu hali ya mazingira duniani.

Ufadhili wa Faith for Earth ulitolewa na UNEP, Wakfu wa Thomas Berry, na Sikh Gurdwara San Jose, pamoja na ufadhili zaidi kutoka kwa wafadhili binafsi.

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP in mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.  Mradi wa UNEP wa Faith for Earth huanganisha dini mbalimbali kote ulimwenguni ili kushughulikia masuala ya mazingira.

Kuhusu Bunge la Dini Duniani la Kushughulikia Mazingira (World’s Religions Climate Action)

Bunge la Dini Duniani la Kushughulikia Mazingira lilibuniwa ili kuleta mshikamano kati ya jamii kidini na za kiroho na kuziwzesha kushirikiana duniani pamoja na taasisi zake kuu ili kuwa na dunia endelevu, yenye haki na amani. Kikosi cha Bunge la Dini Duniani la Kushughulikia Mazingira kinatambua kuwa hali ya maisha ya binadamu na utafiti wa kisayansi vinaonyesha ukweli kwamba hatari zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi haiwezi kuepukika na inasambaa kwa haraka.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na: 

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

Joshua Basofin, Mkurugenzi, Parliament of the World’s Religions Climate Action