Picha na Roberta Annan
Roberta Annan, mfanyabiashara wa kike kutoka Ghana, alizindua Mfuko wa Kufadhili Mtindo wa Kiafrika katika mwaka wa 2011 kuwawezesha mafundi na watu wabunifu kupata fedha na muundo msingi barani kote. Anasisitiza kuwa kudumu kwake hakutegemei tu vifaa vinavyotumiwa kuunda vitu maridadi; pia kunapaswa kuongeza ujira na kukuza uchumi - hasa kwa wanawake.
Tangu kuzinduliwa kwake, Mfuko huo umetoa msaada wa dola za Marekani 5,000 kwa mafundi ili kuwawezesha kuboresha wanavyotengeneza na kupata soko kwa bidhaa zao. Hutoa kipaumbele kwa aina ya mtindo unaomilikiwa na wanawake, ikijumuisha kampuni ya vipodoshi na wanamtindo wa kutengeneza chokoleti.
"Ni sharti tutumie janga la korona kama fursa ya kutafakari tena kuhusu uendelevu - siyo tu kwa bara la Afrika ila kwa dunia nzima," alisema akiwa nyumbani kwake mjini Accra, Ghana. "Tumetunikiwa na mazingira yetu asilia, na tuna fursa ya kubuni mfumo wa biashara kutokana na umaridadi wa tunu hiyo."
Ijapokuwa hawapunguzi madhara ya korona kwa biashara, Annan na wenzake wanaofanya kazi na Mfuko huo wanunuia kuutumia kama fursa kuimarisha mpango ambao tayari ulikuwepo ili kuweza kushiriki biashara kupitia njia za kiektroniki. Jukwaa la kidijitali tayari limewekwa; kile tu kinachohitajika ni mtandao wa usambasaji wa kimataifa ili kuweza kuwafikishia wanunuzi bidhaa kote duniani.
Mfuko huo pia ulishirikisha fundi mbunifu wa mitindo yake aliyenufaika ufadhili unawezesha mfadhili kuwa na hisa katika kampuni yako. ufadhili alioupata ulimwezesha kusambaza vitanda 130 vya wafumi vinavyoweza kukunjika vijijini nchini Ghana na nchini Nijeria. Hali hii itawezesha kukuza ujasiriamali miongoni mwa mashirika ya wanawake watakaofuma na kuuza nguo.
"Ni muhimu kwa mafundi walio na ujuzi huo kuwa na fursa ta kufikia ulimwengu, pasi na tatizo", alisema. "Tunakimu hitaji la ubunifu wa mazao kutoka barani Afrika kwa kufuata kanuni za kiafrika.
Kuanzia mwezi wa Agosti atakuwa mratibu na msimamizi wa dola za Marekani milioni 100, Mfuko wa Kufadhili Watu Wabunifu Barani Afrika (Impact Fund for African Creatives) unaotoa mtaji wa kukuza biashara zao, kipaumbele kikitolewa kwa vifaa endelevu na kwa wale wanaofuata kanuni mwafaka za kuendeleza biashara.
Uwekezaji wa aina hii kwenye kampuni za Kiafrika unatoa fursa ya "kufanya maamuzi mapya," alisema Annan. "Tunarudia asili yetu tukitilia mkazo watu na sayari huku tukipata faida"
Faida ingine ni fursa ya kuwa mstari mbele katika majadiliano kati ya sekta binafsi na serikali, kuendeleza mabadiliko ya sera ili kufungua masoko na kukuza ubunifu.
"Tunapopokea uwekezaji wa moja kwa moja kutoka kwa makampuni ya kigeni, kwanini nasi tusishiriki," alisema Annan. "Ni sisi tutakaoamua hatima, na tuna fursa ya kuonyesha kuwa kuna uwezo wa kupata faida huku tukisaidia jamii."