REUTERS/Hans Lucas
03 Mar 2021 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

UNEP yazindua safari mtandaoni kupitia mifumo mitatu ya kipekee ya ekolojia ya maeneo ya jangwa

REUTERS/Hans Lucas

Majangwa na maeneo kame kwa mara nyingi hayawasilishwi vyema kwa kudhania kuwa hayawezi kuzalisha. Mifumo hii ya ekolojia ni muhimu kwa kudhibiti hali ya hewa – takribani  asilimia 46 ya gesi chafuzi duniani huhifadhiwa kwenye maeneo ya ukame. Licha ya hali mbaya ya hewa, majangwa haya ni makazi kwa watu zaidi ya bilioni 2 na yana baadhi ya mifumo ya bayoanuai ya kipekee duniani. Majangwa mengi yana vyanzo fiche vya maji vinavyokuza spishi mbalimbali za flora na fauna.

Ili kuhamasisha kuhusu mifumo hii muhimu ya ekolojia ambayo mara nyingi hupuuzwa; Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) lilizindua kampeni ya Wild for Life safari inayoendeshwa mtandaoni kupitia kwa majangwa ya kipekee matatu: jangwa la mawemawe la Gobi linalopatikana Asia ya Kati; jangwa la Wadi Rum nchini Jordan na jangwa pana la Sahara.

https://www.youtube.com/watch?v=t1mFAx_AsXo

Matuta ya mchanga yanayometameta katika jangwa hutoa kipato cha kiasili kwa jamii za mitaa kupitia utalii wa ekolojia. Hata hivyo, mabadiliko ya tabianchi, yakijumuishwa na mmomonyoko wa udongo na uharibifu wa maeneo yalio karibu ni hali inayochangia majangwa haya kupanuka.

Ufugaji endelevu wa kuhamahama unaofanywa na na jamii za wafugaji husadia kukabiliana na majangwa, uharibifu wa ardhi na ukame kwenye safu ya milima; huku ukisaidia kuhifadhi bayoanuai na kuchangia kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu. Huku spishi milion zikiwa hatarini kuangamia, bayoanuai imepewa kipaumbele na UNEP. Dunia inapokabiliwa na ukweli kuwa hakuna Malengo ya Aichi  yaliyofikiwa na inapojiandaa kwa mfumo mpya mpana wa baada ya 2020, suala hili linajipatia umaarufu na linahitaji kushughulikiwa kwa dharura duaniani.

Desert image
Shutterstock

Safari majangwani kupitia mtandaoni inaonyesha umuhimu wa mifumo hii ya ekolojia kwa bayoanuai – na shughuli za binadamu zinatishia uwepo wake.

Waliojisajili kushiriki katika safari kwenye jangwa la Gobi watapata fursa ya kupitia kwenye eneo la kilomita mraba milioni 1.3 – jangwa la nne kwa ukubwa duniani.  Licha ya hali mbaya ya hewa, ufugaji wa kuhamahama—watu wanapohama katika eneo fulani ili kupata lishe kwa mifugo wao—ni nyenzo muhimu ya mapato majangwani.

Wale wanapania kuchukua safari kupitia Wadi Rum Kusini mwa Jordan, Eneo linaloanishwa na UNESCO kama Turathi Duniani, watashuhudia matuta yake ya michanga miekundu na muundo wa mawe yanayopendeza, huku wakijifunza kuwa kutoshughulikia taka ipasavyo inayotokana shughuli za kitalii na michezo inatishia uharibifu wa janga hilo.

Safari ya kipekee ya tatu– Jangwa la Sahara – ni jangwa kubwa mno duniani lililo na kiwango cha juu zaidi cha joto, linalokalia eneo la milioni 9.4 kilomeita mraba, na linapitia katika nchi 11 zinazopatina Kusini mwa Afrika. Watakaoshiriki watagundua kuwa Jangwa la Sahara ni makaazi kwa bayoanuai mbalimbali. Spishi 500 za mimea, spishi 70 za mamalia, spishi 100 za reptilia, Spishi 90 za ndege, na athropodi kadhaa – kama vile buibui na nge.

Desert image
Shutterstock

Safari ya jangwani ni mojawapo wa safari 6 za Wild for Life kupitia mifumo maalum ya ekolojia—bahari, mboji, savana, misitu, na milima—ili kujifunza kuhusu jinsi ambavyo hutoa bidhaa na huduma kwa binadamu na changamoto zake na jinsi ya kukabiliana nazo. Kampeni ya Wild for Life, ni juhudi za kimataifa zinazoongozwa na UNEP, ili kuhamasisha kuhusu changamoto za wanyamapori na za makaazi yake.