22 Jul 2020 Video Ocean & Coasts

Tafiti kuhusu Mifumo ya ekolojia ya baharini inayotegemeana

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa limebuni njia zitakazokufanya kuwa makini za kidijitali ili kuendeleza kampeni yake ya #WildforLife. "Safari" hizi nne zinazohusu mifumo ya ekolojia zinanaonyesha umuhimu wa kutegemeana kwa mifumo asilia na kuhimiza watu kuchukua hatua za kutunza mifumo hizi za kipekee.

Safari ya kwanza, Safari ya Baharini. Safari hii ya majini inafundisha na kuhamasisha watu kuhifadhi mifumo ya ekolojia ya matumbawe, ya nyasi ya baharini na  ya mikoko.

https://youtu.be/J_OGCudXDPo

Safari hiyo itahusisha maeneo ya savana, misitu na ardhi ya mboji.

Utangulizi kuhusu kampeni:

Ijapokuwa mazingira ndiyo nguzo ya maisha duniani, yamo hatarini. Mnamo Mei mwaka wa 2019, ripoti ya Jukwa la Kimataifa la Sayansi la Kuhudumia Bayoanuai na Mifumo ya Ekolojia (IPBES)  ilidhibitisha kuwa bayosifia duniani, "inayotegemewa na viumbe vyote" inaharibika kwa kasi kuliko kipindi kingine chochote katika historia.

Spishi milioni moja ya mimea ya porini na wanyama wa porini zinaangamia-nyingi zikiangamia kwa kipindi cha miongo tu.  Robo tatu za mazingira katika maeneo ya ardhi, asilimia 85 ya ardhi ya mboji, na theluthi tatu za bahari zimeathiriwa vibaya mno kutokana na shughuli za binadamu.

Kwa kuongezea, Biashara Haramu ya Wanyamapori  inafanya spishi kuangamia huku ikiathiri mazingira, uchumi, maendeleo na usalama. Lakini tunaweza kubadilisha mienendo hii. Nchi kote ulimwenguni, Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na ya kitaifa, biashara, serikali na viongozi wakuu wanashirikiana kuhamasisha, kuunda na kutekeleza sheria dhabiti, na kuimarisha msaada kwa jamii za wenyeji illi kukomesha biashara haramu ya wanyamapori.

 Hata wewe unaweza kushiriki. Pamoja, tuchukue juhudi za kutotokomeza spishi na khuhifadhi na kuboresha mazingira kwa manufaa ya watu na wa manufaa ya mazingira.

Maudhui Yanayokaribiana