Ukweli kuhusu Hitaji la Kushughulikia Mabadiliko ya Tabianchi kwa Dharura

UNEP
UNEP

Unachopaswa kufahamu kuhusu hitaji la kushughulikia Mabadiliko ya Tabianchi kwa dharura

Sayansi kuhusu mabadiliko ya tabianchi imekuzwa ipasavyo:

  • Mabadiliko ya tabianchi yapo na husababishwa haswa na shughuli za binadamu. (IPCC)
  • Mkusanyiko kwa gesi ya ukaa kwenye mazingira duniani kunahusishwa moja kwa moja na wastani wa kiwango cha joto duniani. (IPCC)
  • Mkusanyiko umekuwa ukiongezeka kwa kasi, na wastani wa kiwango cha joto duniani ikiongezeka pia, tangu wakati wa Mapinduzi ya Viwanda. (IPCC)
  • Kiwango kikubwa zaidi the gesi ya ukaa, kinachokadiria angalau theluthi mbili ya gesi ya ukaa, kabonidioksidi (CO2), kwa kiasi kikubwa hutokana na fueli ya visukuku. (IPCC)
  • Methani, kijenzi kikuu cha gesi asilia, ni chanzo cha zaidi ya asilimia 25 ya ongezeko la joto tunaloshuhudia kwa sasa. Ni kichafuzi kikuu kilicho na uwezo wa kuongeza kiwango cha joto duniani kwa zaidi ya mara 80 kuliko CO2 wakati wa kipindi cha miaka 20 baada ya kutolewa angani. (Ukweli kuhusu Uzalishaji wa Methani, UNEP)

Jopo la Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) lilibuniwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ili kuwa chanzo kisichokuwa na upendeleo cha habari ya kisayansi kuhusu mabadiliko ya tabiachi. Katika mwaka wa 2013, IPCC ilitoa ripoti iliyopitiwa na wenzao ulimwenguni kote kuhusu nafasi ya shughuli za binadamu kwa mabadiliko ya tabianchi wakati ilipotoa Ripoti yake ya Tano ya Tathmini. Ripoti hiyo ilieleza wazi kwenye hitimisho lake: mabadiliko ya tabianchi yapo na shughuli za binadamu, haswa kuachiliwa kwa gesi chafuzi kutokana na kuchoma fueli ya visukuku (makaa ya mawe, mafuta, gesi), ndicho chanzo kikuu.

In Climate Action

Athari na madhara ya mabadiliko ya tabianchi ni yepi?

Athari za ongezeko la nyuzijoto 1.1 ziko hapa leo na zinaongezeka kwa kasi na hali ya matukio mabaya mno ya hali ya hewa kuanzia kwa mawimbi ya joto, ukame, mafuriko, dhoruba za msimu wa baridi, vimbunga na mioto ya mwituni. (IPCC)

  • Joto la wastani ulimwenguni katika mwaka wa 2019 lilikuwa nyuzijoto 1.1,  juu kuliko kipindi cha kabla ya viwanda, kwa mjibu wa WMO.
  • 2019 ilihitimisha muongo wa joto la kipekee ulimwenguni, kupungua kwa barafu na usawa wa bahari kutokana na gesi za ukaa zinazozalishwa na shughuli za binadamu. (WMO)
  • Asilimia 30 ya idadi ya watu ulimwenguni wanakabiliwa na mawimbi mabaya ya joto yanayotokea zaidi ya siku 20 kwa mwaka. (Ukweli kuhusu Kupunguza Kiwango cha Joto na Mabadiliko ya Tabianchi, UNEP)
  • Wastani wa joto kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2019) na kipindi cha miaka kumi (2010-2019) ndio ya juu zaidi kuwahi kurekodiwa. (WMO)
  • Mwaka wa 2019 ulichukua nafasi ya pili kwa kurekodi kiwango cha juu zaidi cha joto. (WMO)
  • Katika mwaka wa 2019, jumla ya uzalishaji wa gesi ya ukaa, ikijumuisha mabadiliko ya matumizi ya ardhi, ilifikia kiwango kipya sawa na gigatani 59.1 za kabonidioksidi (GtCO2e). (EGR, 2020)
  • Kwa kuzingatia ahadi ambazo hazitoshi kote ulimwenguni za kupunguza uzalishaji wa gezi zinazochafua mazingira, kuongezeka kwa gesi ya ukaa kutokana na jamii kurudi kutumia kaboni nyingi baada ya ugonjwa mtandavu unaweza kupelekea uzalishaji katika mwaka wa 2030 kuongezeka zaidi hadi GtCO2e 60. (EGR, 2020)
wildfires

Tunapaswa kufanya nini ili kudhibiti ongezeko la joto duniani na kushughulikia mabadiliko ya tabianchi kwa dharura?

  • Ili kudhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 1.5, tunahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 7.6 kila mwaka kuanzia mwaka huu hadi mwaka wa 2030. (EGR, 2019)
  • Miaka 10 iliyopita, ikiwa nchi zingechukua hatua kuhusu hii sayansi, serikali zingehitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa  asilimia 3.3 kila mwaka. Kila mwaka tunaposhindwa kuchukua hatua, kiwango cha ugumu na gharama ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu hupanda. (EGR, 2019)
  • Kupunguza mno uzalishaji wa methani ni muhimu ili kusaidia kupunguza ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzijoto 1.5 au nyuzijoto 2, kwa mjibu wa IPCC. Zaidi ya asilimia 75 ya uzalishaji wa gesi ya methani unaweza kupunguzwa na teknolojia iliyopo leo - na hadi asilimia 40 bila gharama yoyote kwa mjibu wa Shirika la Kimataifa la Nishati. (Ukweli kuhusu Uzalishaji wa Methani, UNEP)
  • Kuhifadhi na kuboresha maeneo ya kiasili, kwenye ardhi na majini, ni muhimu ili kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa na kuwezesha kupunguza theluthi moja ya juhudi zinazohitajika katika muongo ujao. (Ukweli kuhusu Hali ya Ushughulikiaji wa Mazingira, UNEP)
  • Kwa kuwa zaidi ya nusu ya Pato la Taifa (GDP) duniani hutegemea mazingira kwa kiwango cha juu au kiwango fulani, kuwekeza kwenye masuluhisho yanayotokana na mazingira hakutapunguza tu ongezeko la joto ulimwenguni lakini pia kutapelekea mapato takribani ya dola bilioni 4 kwa wafanyabiashara na kubuni nafasi mpya za ajira zaidi ya milioni 100 kila mwaka kufikia mwaka wa 2030 . (Ukweli kuhusu Hali ya Ushughulikiaji wa Mazingira, UNEP)
  • Kwa serikali, kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira baada ya COVID-19 kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 25 kutoka kwa viwango vya mwaka wa  2030, na kuwezesha dunia kufikia lengo lake la nyuzijoto 2. (EGR, 2020)
  • Mataifa yalikubaliana kujitolea kisheria mjini Paris kupunguza kiwango cha joto ulimwenguni kisizidi nyuzijoto 2 zaidi ya viwango vya kabla ya viwanda lakini pia yalitoa ahadi za kitaifa za kupunguza au kuzuia uzalishaji wa gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2030. Huu unajulikana kama Mkataba wa Paris. Ahadi za awali za mwaka wa 2015 hazitoshi kufikia lengo, na serikali zinatarajiwa kupitia na kuongeza ahadi hizi kama lengo kuu mwaka huu wa 2021.  
  • Masasisho ya ahadi kwenye Mkataba wa Paris yatapitiwa wakati wa kongamano la mabadiliko ya tabianchi linalojulikana kama COP 26mjini Glasgow, Uingereza mwezi wa Novemba mwaka wa 2021. Kongamano hili litakuwa mkutano muhimu wa kimataifa juu ya changamoto za hali ya hewa tangu Mkataba wa Paris ulipopitishwa katika mwaka wa 2015.
  • Kufaulu au kutofaulu kwa mkutano huu kutakuwa na athari kubwa kwa ulimwengu. Ikiwa nchi haziwezi kukubaliana kuhusu ahadi za kutosha, katika miaka mingine 5, upunguzaji wa uzalishaji gesi chafu unaohitajika utaruka hadi asilimia 15.5 isiyowezekana kila mwaka. Uwezekano wa kutofikia kiwango hiki cha juu zaidi cha kukabiliana na gesi ya ukaa unamaanisha kuwa ulimwengu utakabiliwa na ongezeko la joto ulimwenguni ambalo litaongezeka na kuwa zaidi ya nyuzijoto 1.5. Kila sehemu ya ongezeko la joto duniani zaidi ya nyuzijoto 1.5 utakuwa na madhara makubwa, kwa kutishia maisha, vyanzo vya chakula, kipato na uchumi kote ulimwenguni.
  • Nchi haziko karibu kutimiza ahadi zilizotoa. 
  • Kuongeza ahadi kunaweza kujitokeza kwa njia mbalimbali lakini kwa jumla lazima nchi na uchumi zikabiliane na gesi ya ukaa, ziweke malengo ya kutozalisha gesi ya ukaa, na makataa ya kufikia malengo hayo, haswa kupitia kasi ya kutumia nishati jadidifu na kukoma kwa kasi kwa kutegemea fueli ya visukuku. 
icebergs
Nyuzijoto 1.5

Kwa nini nyuzijoto 1.5 ni muhimu?

Ulimwengu utashuhudia athari mbaya za hali ya hewa kwa nyuzijoto 1.5. Lakini baada ya hapo hali itazidi kuwa mbaya zaidi. Tofauti kati ya nyuzijoto 1.5 na nyuzijoto 2 ni…

  • tofauti kati ya asilimia 70 au asilimia 99% ya matumbawe yanayoangamia.
  • uwezekano mara mbili zaidi kwa dudu, vichavushaji muhimu, kupoteza nusu ya makazi yao.
  • majira ya joto bila barafu katika Bahari ya Aktiki mara moja kwa karne au mara moja kwa muongo.
  • mita 1 kuongezwa kwenye kupanda kwa usawa wa bahari.
  • watu milioni 6 au milioni 16 kuathiriwa na kupanda kwa usawa wa bahari katika maeneo ya pwani mwishoni mwa karne hii.

 

Chanzo: Jopo la Kimataifa Kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC)