Showing 1 - 6 of 12
12 results found
Arcenciel (Lebanon), kampuni inayotuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni shirika linalokuza mazingira safi na bora na kuchangia msingi wa kuwekwa kwa mkakati wa kitaifa wa kushughulikia taka nchini Lebanon. Kwa sasa, arcenciel huchakata zaidi ya asilimia 80 ya taka za hospitali zinazoweza kuambukiza magonjwa nchini Lebanon kila mwaka.
Constantino (Tino) Aucca Chutas (Peru), ambaye pia ametuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ameanzisha mfumo wa upandaji miti katika jamii unaoendeshwa na wenyeji na jamii za kiasili. Hali ambayo imepelekea miti milioni tatu kupandwa nchini Peru. Pia anaongoza juhudi kabambe za upandaji miti katika nchi zingine za eneo la Andes.
Sir Partha Dasgupta (Uingereza), aliyetuzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu, ni mwanauchumi mashuhuri ambaye ukaguzi wake wa kipekee kuhusu uchumi wa bayoanuai unatoa wito kutafakari upya mno kuhusu uhusiano wa binadamu na mazingira asilia ili kuzuia mifumo muhimu ya ekolojia kuporomoka.
Dkt Purnima Devi Barman (India), anayetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali, ni mwanabiolojia wa wanyamapori anayeongoza "Jeshi la Hargila", vuguvugu la wanawake pekee la uhifadhi mashinani linalojitolea kulinda Korongo aina ya Greater Adjutant Stork dhidi ya kuangamia. Wanawake hawa hutengeneza na kuuza nguo zilizo na michoro ya ndege hao, na kusaidia kuhamasisha kuhusu spishi hii huku wakiweza kujitegemea kifedha.
Cécile Bibiane Ndjebet (Cameroon), anayetuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni mtetezi asiyechoka wa haki za wanawake za kumiliki ardhi barani Afrika, hali inayohitajika kuwawezesha kutekeleza wajibu muhimu wa koboresha mifumo ya ekolojia, kupambana na umaskini na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia anaongoza juhudi za kushawishi kuwepo na sera kuhusu usawa wa kijinsia katika usimamizi wa misitu katika nchi 20 barani Afrika.
Michelle Bachelet, Rais wa Chile, ni Bingwa wa Dunia wa mwaka wa 2017 kutokana na uongozi wake wa kipekee wa kuunda maeneo ya bahari yaliyohifadhiwa na kukuza nishati jadidifu.