Video

Mshindi wa tuzo la utengenezaji filamu, Jeff Orlowski, ni Bingwa wa Dunia wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kutokana na mafanikio yake ya kutuma jumbe nzito kuhusiana na mazingira kwa watazamaji kote ulimwenguni.

Video

Mobike ni Bingwa wa Dunia wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kutokana na maono yake ya ujasiriamali ya kutoa suluhisho kwa uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuzingatia soko.

Video

Wang Wenbiao, Mwenyekiti wa Kikundi cha Elion Resources Group ni Bingwa wa Dunia wa mwaka wa 2017 kutokana na mafanikio yake ya kudumu.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cochin ni uwanja wa ndege wa kwanza kutumia nishati ya jua duniani. Hutekeleza kazi zake zote kwa kutumia nishati ya jua. Ni uwanja wa ndege mkubwa zaidi na wenye shughuli nyingi zaidi katika jimbo la Kerala nchini India, na pia ni uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi nchini India kwa kuzingatia mlolongo wa ndege za kimataifa. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cochin ulianza kufanya kazi kikamilifu kwa kutumia nishati ya jua mwaka wa 2015 - mradi ulioanzishwa na Mkurugenzi Mwendeshaji Vattavayalil Joseph Kurian.

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa hujivunia kufanya kazi na wabia kutambua na kusherehekea mafanikio ya kipekee ya washindi wa tuzo la Mabingwa wa Dunia.

Ni kutokana na ukarimu wao mkuu ndipo tunapoweza kuendelea kusherehekea mafanikio yao. Wabia wetu hufadhili juhudi za Mabingwa wa Dunia na Vijana Bingwa Duniani.

Weibo

Weibo imejitolea kuimarisha juhudi za kushughulikia utunzaji wa mazingira na maendeleo endelevu. Tayari imefadhili kampeni kadhaa za Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kwa mitandao yake katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na Siku ya Mazingira Duniani na kampeni ya Wild for Life.

Tuzo la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. 

UNEP inatafuta kupendekezwa kwa watu binafsi na mashirika yanayofanya kazi kupata masuluhisho bunifu na endelevu ya kuboresha ardhi, kuimarisha ustahimilivu kwa ukame, na kupambana na kuenea kwa majangwa. 

Upendekezaji wa wawaniaji wa awamu ya mwaka wa 2024 unaendelea kwa sasa

.

Upendekezaji unaweza kufanywa katika viwango vinne

Mchakato wa kuchaguliwa

Wafanyakazi wa UNEP na wataalam wa mada husika huchagua kutoka kwa orodha ya mapendekezo yaliyopokelewa kutoka kote duniani. Mtu yeyote anaweza kutoa mapendekezo/kupendekezwa. Katika mwaka wa 2023, UNEP ilipokea mapendekezo 2,500, na kuwa mwaka wa tatu mfululizo wa kupokea mapendekezo mengi zaidi.  

Vigezo vya kuchaguliwa ni kama vifuatavyo:

  • Athari: Je, juhudi za aliyependekwa zimepelekea manufaa makubwa ya kimazingira au zimeonyesha kuwa na uwezekano mkubwa wa kurudufishwa na kuimarishwa zaidi?
  • Mambo mapya: Je, aliyependekezwa amefanya au kupelekea kitu kipya na bunifu?   
  • Ushawishi:  Kisa cha aliyependekezwa kinavutia kwa kiwango kipi?

 

Kutoka kwa washindi kutoka nyanjani na viongozi wa taasisi hadi kwa wanasiasa wa kipekee na taasisi za utafiti, UNEP inasherehekea Washindi wanaofanya maamuzi ya kipekee kwa manufaa ya dunia yetu. 

Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2005, tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa na Umoja wa Mataifa ni tuzo la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira. 

Kila mwaka, UNEP hutuza watu binafsi na mashirika yanayofanya kazi kupata masuluhisho bunifu na endelevu ya kushughulikia changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na bayoanuai, na kemikali, uchafuzi na taka. Mabingwa hubadilisha uchumi wetu, huvumbua, huongoza mabadiliko ya kisiasa, hupambana na ukosefu wa haki ya mazingira na kupigania malighafi zetu. 

Mabingwa wa Dunia huwatuza watu katika vitengo vinne:

  • Uongozi unaozingatia sera Maafisa wa sekta ya umma wanaoongoza hatua za kimataifa au kitaifa za kushughulikia mazingira. Wao huendeleza mijadiliano, kujitolea kwa dhati na kuchukua kwa manufaa ya sayari.
  • Motisha na kuchukua hatua Viongozi wanaochukua hatua madhubuti zinazopelekea mabadiliko chanya ya kutunza dunia yetu. Maongozi yao ni ya kupigiwa mfano, wanatuhimiza kubadilisha mienendo yetu na kutia moyo mamilioni ya watu.
  • Maono ya ujasiriamali Watu walio na maono ya kipekee yanayoenda kinyume na hali ya kawaida ya kukuza mustakabali usiochafua mazingira. Wao hukuza mifumo, kubuni teknojia mpya na kujitokeza na maono mapya ya kipekee.  
  • Sayansi na ubunifu Waanzilishi wanaotumia teknolojia kikamilifu kwa manufaa makuu ya mazingira. Ubunifu wao unaweza kupelekea kuwepo na siku za usoni endelevu.

Tuzo la Mabingwa wa Dunia limewatuza washindi 116, ikijumuisha viongozi duniani na watu wanaobuni teknolojia. Wanajumuisha Viongozi wa dunia 27, watu binafsi 70 na makundi au mashirika 19. 

2019 Champions of the Earth award ceremony. Photo: UNEP

 

Thank you for subscribing.

Kisa cha SEKEM kinaanzia jangwani nchini Misri na hema, trekta na piano.

Katika mwaka wa 1977, mwanzilishi wa shirika hili la maendeleo, Ibrahim Abouleish, alirudi nchini Misri baada ya miaka 20 ya kufanya kazi nje ya nchi katika kemia na famakolojia.

Wakati huo, Misri ilikuwa inakabiliwa na mtanziko. Ilihitaji kulisha idadi ya watu inayoongezeka kwa kasi, lakini sekta yake ya kilimo ilikuwa duni, mashamba yalikuwa yakigeuka na kuwa majangwa, na matumizi ya kupita kiasi ya dawa za kuua wadudu na mbolea za kemikali yalikuwa yakidhuru udongo.

Kwa hivyo, kwenye eneo ambalo halikuwa limewahi kuguswa la jangwa la kaskazini-mashariki mwa Cairo, Abouleish alisimamisha hema na kuanzisha SEKEM. Shirika lililopewa jina la hieroglifu ya "uhai wa jua ”, shirika hili baadaye likawa kitovu cha kilimo cha bayodinamiki, aina ya kilimo hai kinachosisitiza amani kati ya mazingira, maendeleo ya binadamu na imani ya kidini.

Vitega uchumi viwili vya kwanza vya Abouleish vilikuwa trekta na - kifaa kilichowashangaza wakulima wadogo wa eneo hilo - piano.

Mwanawe, Helmy, afisa mkuu mtendaji wa SEKEM kwa sasa, anasema piano iliashiria umuhimu wa "mihimuko na hisia" kwa kuunganisha binadamu na mazingira. Wawili hao waliongoza SEKEM pamoja hadi kifo cha Ibrahim katika mwaka wa 2017.

"Kwa baba yangu, kila mara ilikuwa ni kukuza uhusiano na jangwa ambapo, bila ya chochote, unakuza viumbe," Helmy Abouleish anasema huku akitabasamu wakati wa mahojiano na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).

Sasa, miaka 47 baada ya kuanzishwa kwake, SEKEM imekua na kuwa shirika la maendeleo lililo na nyanja nyingi ambalo linasaidia kukabiliana na kuenea kwa majangwa, kukuza mifumo thabiti ya chakula, kukabiliana na umaskini na kushughulikia janga la mabadiliko ya tabianchi. Mwishoni mwa mwaka, SEKEM inasema kuwa itakuwa imesaidia wakulima 15,000 kukumbatia kilimo cha bayodinamiki tangu mwaka wa 2022, na kuendeleza shughuli hiyo katika angalau hekta 19,000 za mashamba.

Uboreshaji wa SEKEM wa ardhi iliyoharibika na majangwa na kuyafanya kuwa mifumo inayofanya kazi na inayoweza kuzalisha hutoa ahueni inayohitajika kwa mifumo ya ekolojia iliyo hatarini, wataalam wanasema. Kote duniani,  hekta milioni 12 za ardhi  zilizo na uwezo wa kuzalisha tani milioni 20 za nafaka hupotea kutokana na ukame na kuenea kwa majangwa kila mwaka.

Kutokana na juhudi zake za kukabiliana na uharibifu wa ardhi na kuenea kwa majangwa huku ikihimiza maendeleo endelevu, SEKEM imetajwa kuwa Bingwa wa Dunia wa mwaka wa 2024– tuzo la Umoja wa Mataifa ya ngazi ya juu zaidi - katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali. SEKEM ni mojawapo wa washindi sita katika kundi la mwaka wa 2024 .

"Mara nyingi, njia ambayo wanadamu hutumia kuzalisha chakula sio endelevu. Hili ni tishio kwa dunia asilia na uwezo wetu wa muda mrefu wa kujilisha wenyewe,” anasema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "SEKEM inaonyesha kuwa inawezekana kufanya mifumo ya chakula kufanyia kazi watu na sayari, ambayo ni muhimu ili kushinda majanga kwa mazingira kama vile majangwa na kurejesha amani kati ya wanadamu na mazingira."

Kupanda mbegu 

Kwa milenia kadhaa, kilimo kimekuwa nguzo ya uchumi wa Misri. Hutoa riziki kwa asilimia 55 ya jumla ya dadi ya watu nchini, lakini miongo kadhaa ya kuenea kwa majangwa, uharibifu wa ardhi na kuongezeka kwa idadi ya watu vimefanya kuhakikisha utoshelezaji wa chakula kuwa changamoto, kulingana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Katika juhudi za kukidhi ongezeko la mahitaji ya chakula na kusaidia idadi ya watu ambapo zaidi ya robo ya watu wanaishi katika umaskini, Misri kwa muda mrefu imekuwa ikitegemea matumizi ya mbolea za kemikali na dawa za kuulia wadudu. Hizi mara nyingi huzingatiwa kama njia za bei nafuu zaidi ya kuimarisha mavuno. Lakini zikitumiwa kupita kiasi, zinaweza kuingia kwenye maji ya ardhini na kudhoofisha muundo wa udongo, kumomonyoa ardhi na hatimaye kutoa nafasi kwa majangwa.

SEKEM inaepuka mbolea za kemikali. Inafanya kazi na wakulima kote nchini ili kuhakikisha aina mbalimbali za mimea na wanyama - kuanzia kwa nyuki hadi kwa bundi - wamo mashambani, kimsingi kuunda mifumo ndogo ya ekolojia. SEKEM hunufaika kutumia mabaki ya mimea na samadi ya wanyama ili kuongeza mavuno ya mazao. Mzunguko huu hudumisha afya ya udongo na husaidia kufanya mashamba kustahilili kuenea kwa majangwa.

Kilimo cha bayodinamiki pia kinaweza kutoa msaada unaohitajika katika vita dhidi ya janga la mabadiliko ya tabianchi, wataalam wanasema. Udongo wenye afya ni miongoni mwa njia bora zaidi za kuhifadhi hewa ya ukaa inayoongeza joto kwenye sayari. Udongo pia ni makazi kwa zaidi ya asilimia 25 ya bayoanuai ya kimataifa na husaidia viumbe wengi juu ya ardhi, kulingana na FAO .

Matumaini ya mavuno 

SEKEM inasema inalenga kusaidia wakulima 40,000 kuanza kufanya kilimo cha bayodinamiki kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2025 kwa ushirikiano na Chama cha Bayodinamiki cha Misri. Kufikia mwaka wa 2028, lengo ni kufikia wakulima 250,000 wenye mashamba ya ukubwa wa ekari milioni 1.6.

Hali hii ni tofauti na siku za awali za SEKEM, wakati kilimo cha bayodinamiki kilikuwa dhana ambayo haijafanyiwa majaribio barani Afrika, anasema Abouleish.

"Baba yangu alitaka kuthibitisha kuwa unaweza kutafakari upya kuhusu uchumi, kutafakari upya kuhusu kilimo," anasema. "Aliyaita maono yake 'Uchumi wa upendo'."

Miongoni mwa jitihada nyingine za SEKEM ni jitihada za kuboresha hekta 1,000 za jangwa na kuanzisha jamii inayojitosheleza. Huku asilimia 96 ya ardhi nchini Misri ikiwa jangwa, mpango uliopewa jina la "Kufanya Jangwa kuwa Kijani" unalenga kulisha maelfu ya watu huku ukiondoa hewa ya ukaa.

Kutoka kwa hema katika jangwa ambalo halijaguswa, SEKEM imekua hadi kuwa shirika ku la maendeleo. Inaendesha shule, vituo vya kutoa mafunzo na chuo kikuu, kutayarisha wakulima na vijana kukabiliana na uharibifu wa ardhi na kuenea kwa majangwa.

SEKEM huuza bidhaa za kilimo hai ndani na nje ya nchi, na ushirikiano wake na benki za Ulaya na miungano ya kimataifa huwezesha uwekezaji unaoendelea katika mbinu za kilimo cha bayodinamiki nchini Misri. Vipengele mbalimbali vya mpango huo ni pamoja na kampuni maalum zinazojumuisha kampuni za kutengeneza dawa za kiasili, mavazi, na kadhalika.

Baada ya Ibrahim Abouleish kuadhimisha katika mwaka wa 2017 - maadhimisho ya miaka 40 ya SEKEM - Helmy Abouleish na shirika walianzisha mpango utakawaongoza hadi mwaka wa 2057. Mpango huo unajumuisha kupanua kilimo cha baodinamiki kwa wakulima milioni 7 nchini Misri.

"Tusipofikia haya, hatutakuwa tumefikia maono yetu ya awali," Abouleish anasema. "Watu wengi walituambia haya hayawezekani. Lakini sisi ni wataalamu katika mambo yasiowezekana. Tunapenda mambo yasiowezekana."