Mapya kwenye ripoti iliyotolewa mwaka huu
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ijapokuwa kumekuwa na upunguzaji wa uzalishaji wa kaboniksidi kutokana na janga la korona (COVID-19), ongezeko la joto duniani linaelekea kuwa juu zaidi kwa nyuzijoto 3 katika karne hii – hali itakayofanya kuwa vigumu kufikia malengo ya Mkataba wa Paris ya kudhibiti kiwango cha joto kuwa chini ya nyuzijoto 2 hadi ifikie nyuzijoto 1.5.
Hata hivyo, kujiimairisha baada ya janga la korona kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa takribani asilimia 25 jinsi inavyotarajiwa kufikia mwaka wa 2030, kwa kuzingatia sera zilizowekwa kabla ya COVID-19. Kujiimarisha kwa namna hii kutawezesha utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na serikali chini ya Mkataba wa Paris, na kuwezesha dunia kuwa karibu kufikia viwango vya nyuzijoto 2.
Ripoti hiyo pia inachanganua mikakati iliopo ya kupunguza hewa ya ukaa inatoa muhtasari kuhusiana na ahadi za kutozalisha kabisa gesi ya ukaa na kuchunguza kuhusu uwezo wa jinsi mienendo ya maisha, sekta ya usafiri wa ndege na usafiri ya meli zinavyoweza kusaidia kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi.