Kaulimbiu: Amani na mazingira
Tembelea ukurasa rasmi kongamano.
Mkutano wa 16 wa Kongamano la Nchi Wanachama (COP) wa Mkataba wa Uanuai wa Kibayolojia (CBD) ataendelea mjini Cali, Colombia kuanzia tarehe 21 Octoba hadi tarehe 1 Novemba mwaka wa 2024.
Mkutano wa 11 wa Kongamano la Nchi Wanachama unatumika kama Mkutano wa Wanachama (MOP) wa Itifaki ya Cartagena ya Usalama wa Mazingira na MOP ya tano ya Itifaki ya Nagoya ya Upatikanaji wa Rasilimali za Kijenetiki na Kugawana kwa Njia ya Haki na Usawa wa Manufaa yanayotokana na Matumizi yake pia utafanyika katika kipindi hicho hicho.
Wakati wa COP 16, serikali zitapewa jukumu la kukagua hali ya utekelezaji wa Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal. Wanachama wa Mkataba huu wanatarajiwa kuonyesha kurandana na Mikakati ya Kitaifa ya Bayoanuwai na Mkakati Kazi (NBSAPs) na Mfumo huu. COP 16 itaendeleza zaidi mfumo wa ufuatiliaji na kuendeleza ukusanyaji wa rasilimali za Mfumo wa Bayoanuai Duniani. Miongoni mwa majukumu mengine, COP 16 pia inalenga kukamilisha na kutekeleza mfumo wa kimataifa kuhusu ugawaji sawa na wa haki wa manufaa kutokana na matumizi ya taarifa za kidijitali zinazotolewa kwa mfululizo kuhusu rasilimali za kijenetiki.
Nyenzo zaidi:
- Kazi ya UNEP kuhusiana na mazingira
- Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal (rasilimali)
- Kuimarisha utekelezaji wa Mfumo Wa Kimataifa wa Bayoanuai (hotuba)
- Miezi tatu muhimu ya diplomasia ya mazingira (hotuba)
Ukrasa huu utasasishwa kwa kuongezea taarifa zaidi.
This page will be updated with more information.