• Maelezo ya Jumla

Lini: Alhamisi Februari 17 2022; 2:00pm EAT/12:00pm CET/6:00am EST 

Wapi: Mtandaoni

Muda: Saa moja

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) litazindua toleo la mwaka wa 2022 la Ripoti ya Masuala Ibuka: Masuala Ibuka Yanayoathiri Mazingira kwa mkutano na wanahabari mtandaoni tunapoelekea UNEA 5.2. 

Ripoti ya UNEP ya Masuala Ibuka imetambulisha na kuangazia masuala ibuka yanayoathiri mazingira. Toleo la mwaka wa 2022 linaendeleza kazi hii kwa kutambulisha changamoto za mazingira na masuhuhisho yake ili kuzishughulikiwa kikamilimu kwa mda unaofaa. Baadhi ya masuala yanaweza kuhusu tu eneo, yanaweza kuwa madogomadogo kwa sasa, ila yana uwezekano wa kuenea maeneo mengine au kuathiri ulimwengu mzima yasiposhughulikiwa mapema.

Ripoti hii ina sura ifuatayo: 

  1. Kusikiliza Miji: Kuanzia Mazingira Ya Kelele hadi kwa Mandhari ya Sauti za  Kupendeza  
  2. Mioto Misituni chini ya Mabadiliko ya Tabianchi: Suala Nyeti 
  3. Fenolojia: Mabadiliko ya Tabianchi Yanabadilisha Ruwaza ya Kiasili

Wanajopo: 

  • Andrea Hinwood, Mwanasayansi Mkuu, Kwaniaba ya Bi. Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP
  • Mheshimiwa David Da Silva, Kamishna Mkuu na Mwakilishi wa Kudumu wa Kanada
  • Mheshimiwa Khaled Al-Abyad, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Misri
  • Maarten Kappelle, Mkuu wa Tathmini za Mada za Kisayansi (UNEP)