UNEP inatafuta wahakiki kutoka nje kutoa maoni, ikijumuisha kubainisha masuala, data, au taarifa yoyote itakayojumuishwa katika ripoti ya Hali ya Mazingira Ulimwenguni (GEO-7) Rasimu ya Pili ya Kielelezo (SOD) na kwa Rasimu ya Kwanza (FOD) Muhtasari wa Watungasera (SPM.
Unaweza kutuma maombi kupitia tovuti ya kutuma maombi kufikia tarehe 30 Septemba mwaka wa 2024.
Kuhusu GEO-7
Hali ya Mazingira Ulimwenguni (GEO) ni ripoti kuu ya UNEP, inayotoa tathmini jumuishi ya vichochezi vya mabadiliko ya mazingira, hali ya sasa ya mazingira, ufanisi wa kuyashughulikiwa kupitia sera na maamuzi ya kufikia mustakabali tofauti unaowezekana katika kipindi ya muda na kipindi kirefu.
Kutokana na wito wa Nchi Wanachama katika azimio la 5/3 la Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP ilianzisha utayarishaji wa toleo la saba la tathmini ya Hali ya Mazingira Ulimwenguni (GEO-7) na Muhtasari unaoandamana nao kwa Watungasera, itakayozinduliwa katika UNEA-7 mwaka huu. Kipindi cha uhakiki wa wataalam wa GEO-7 SOD na FOD SPM kimepangwa kwa sasa kuanzia tarehe 1 Novemba mwaka wa 2024 hadi tarehe 15 Januari mwaka wa 2025.
Maelezo zaidi yatawasilishwa kupitia barua pepe kwa wataalam walioteuliwa kutoka kwa visanduku vya barua unep-ewad-geohead@un.org au georead@cedare.int.