Mpango kabambe wa kushughulikia mazingira barani Afrika: hatua zinazohitajika
Waheshimiwa, wageni, wenzangu, wabia, mabibi na mabwana.
Nina furaha isiyo na kifani kuwa hapa siku ya leo katika mji unaopendeza wa Durban. Mwanzo, ningependa kushukuru serikali ya Afrika Kusini kwa uongozi wao uliowapelekea kuwa wenyeji wa kongamano hili. Pia ninawashukuru wote waliokusanyika hapa siku ya leo ambao ni kiwakilishi cha nguvu na uwezo wetu kuhusiana na masuala ya mazingira.
Asante sana kwa kujitolea kwenu. Kwa sasa, Afrika ina mpango kabambe wa kushughulikia mazingira. Kuna matumaini ya kuwa na Afrika iliyostawi zaidi.
"Nina maono kuhusu majangwa yetu makubwa, kuhusu misitu yetu, kuhusu mapori yetu makuu. Tusiwahi sahau kuwa ni wajibu wetu kutunza haya mazingira." Hayo ni maneno yake Nelson Mandela. Tunahitaji kuyashughulikia kwa dharura.
Tuna matatizo. Joto linaendelea kuongezeka duniani kwa kasi, bayoanuai inaendelea kuharibiwa kwa kiwango cha kushitua na tunatumia rasilimali nyingi kushinda vile sayari yetu inavyoweza kustahimili. "Viumbe vinakabiliwa na changamoto ya kuangamia," jinsi anavyosema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Lakini, tunafahamu kuwa ni sisi tuliobeba suluhisho- iwe ni kupunguza kiwango cha uzalishaji wa hewa chafu kwa nusu kufikia mwaka wa 2030; kubadili mahusiano yetu na mazingira; au kubadili jinsi tunavyoishi, kutengeneza bidhaa na jinsi tunavyovitumia. Pia, sisi sote tunatambua umuhimu wa kufanya hivyo. Mda wa kushughulikia mazingira unaendelea kuyoyoma.
Afrika, ijapokuwa haijaathiriwa mno na mabadiliko ya tabianchi, itakuwa mojawapo wa waathiriwa wakuu.
Lakini tukiimarisha juhudi zetu za kukabiliana na changamoto za mazingira katika ukanda huu, tutafungua ukrasa mpya kwenye historia ya bara, historia ambayo tukifaulu kukabiliana na changamoto za mazingira, bara litastawi.
Tayari, kuna hatua mwafaka zilizochukuliwa ili hali hii iwe uhalisia kwa siku zijazo. Kuanzia na utunjaji wa wanyamapori, kukuza na kutunza misitu, kukabiliana na uchafuzi na kuweka sheria kuhusu plastiki zinazotumiwa tu mara moja, hadi kutumia nishati isiyochafua mazingira. Afrika itakuwa na mengi ya kuhadithia kuhusu kufaulu kwake. Zaidi ya asilimia 90 zimeithinisha Michango Inayobainishwa na Taifa (NDCs) kushinda eneo lingine lolote duniani. Serikali kutoka pembe zote za dunia zimeweka mikakati ya kipekee ili kushughulikia mazingira.
Hii ndiyo sababu AMCEN haijakosea kuanisha ongezeko la joto duniani na uharibifu wa bayoanuai kama changamoto kuu barani Afrika. Ni ndiyo sababu ni vyema kutambua uchumi unaotegemea bahari na uchumi unaounda vifaa vinavyoweza kutumiwa mara kadhaa kama mojawapo ya njia za kukabiliana na changamoto hizi.
Uwezo wa AMCEN wa kuweka ajenda kuhusiana na mazingira ni muhimu mno kwa ustawi wa jamii na uchumi barani Afrika.
Tunafahamu kuwa AMCEN imechukua hatua mwafaka kwa sababu maamuzi yake yanapotekelezwa tunashuhudia kufaulu kwake. Taka inayoweza kuvundishwa na bakteria nchini Uganda, vifaa vya kukausha vitu kutumia jua nchini Kameruni, mtambo wa kukabiliana na uchafu katika kichinjio kikubwa zaidi mjini Abidjan kinachowezesha maelfu ya wakulima kupata mbolea isiyodhuru mazingira.
Hapa Afrika Kusini, Wizara ya Mazingira inabuni nafasi za kazi kwa kukuza uchumi unaotegemea wanyamapori. Inahimiza ufadhili kwa bidhaa na huduma zilizona manufaa kwa mazingira na watu. Utalii unaotokana na mazingira, bidhaa zinatotokana na mimea na wanyama, bidhaa zinazoweza kuoza katika kampuni za kutengenezea madawa na hali ya kulipia huduma za mifumo ya ekolojia, inatoa mapato na kuboresha maisha ya watu kote nchini.
Miradi hii inaonyesha kuwa inawezekana kukuza uchumi wetu kwa njia endelevu, kwa kubuni nafasi za kazi na kuimarisha maisha ya watu bila kuharibu mazingira. Licha ya hayo, tunastahili kufanikiwa zaidi na kwa kasi. Tunahitaji kuimarisha juhudi zetu na kuhakikisha ni za haki.
Kufaulu kwetu kutategemea sana uwezo wetu wa kunufaika na rasilimali mbili kuu barani-vijana wake na utajiri unaotokana na malighafi.
Kuna vijana wengi Afrika kuliko eneo lingine duniani lakini theluthi moja hawana ajira.
Ijapokuwa takwimu hizi ni za kutisha, ninayo matumaini. Ninaona watu wenye uwezo wa kufanya kazi kutokana na nguvu zao na kuweza kubadilisha bara letu katika karne zijazo.
Iwapo ustawi wa bara unategemea nguvu za watu wake, inamanisha mali ghafi ya Afrika ndio ufunguo wa kuufungua. Kwa misitu na majangwa aliozungumuzia Mandela; baharini, kwenye maeneo oevu na mitoni ndilo ytegemeo la kustawisha bara. Hatuwezi kufaulu kuboresha maisha ya watu na kustawisha Afrika na watu wake bila kukuwa na mazingira mazuri.
Ili kuwezesha Afrika kuwa na ustawi wa kudumu kutokana na malighafi yake, ni sharti tubadili jinsi tunavyokuza uchumi wetu kutoka kwa bidhaa zinazotumiwa mara moja hadi bidhaa zinazoweza kutumiwa mara kadhaa. Tubadili mienendo ya "kuunda, kutumia na kutupa" na kuiga ile ya "kutengeneza upya, kutumia tena na kukarabati". Mfumo huu unatambua kuwa ukuaji wa uchumi inadhibitiwa na changamoto za ekolojia zilizopo kwenye sayari yetu.
Uzuri wa bidhaa zinazoweza kutumiwa mara kadhaa ni kuwa hupunguza nyingi ya changamoto zinakabili mazingira kwa sasa. Utafiti unapendekeza kuwa matumizi ya kanuni za kuwezesha bidhaa kutumiwa tena na tena kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa asilimia 99 kwenye baadhi ya sekta, na kurahisisha kufikia malengo ya Paris.
Uchumi unaotegemea bidhaa zinazoweza kutumiwa tena na tena utawezesha kufikia malengo ya mwaka wa 2030 ya Ajenda ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya Afrika ya mwaka wa 2063.
Changamoto tunazoshuhudia za mazingira ni za kimataifa. Hii ndiyo sababu tunahitaji sasa, kuliko kipindi kingine chochote mashirika ya kimataifa kama vile AMCEN.
Hii ni kwa sababu hatuwezi kuwa na siku za usoni tunazozitaka bila kusaidiwa. Kuna msemo kwa lugha yangu ya Kiswahili, Chombo hakiendi ikiwa kila mtu anapiga makasia yake: Tunahitaji juhudi za pamoja Wakati wa Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Mazingira, Kameruni, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Guinea ya Ikweta zilitoa ahadi ya kutunza misitu yao ili kuwezesha misitu katika eneo la Afrika ya Kati kuendelea kuwapa watu milioni 50 mapato na kudumisha ruwaza ya mvua katika eneo hilo. Na kupitia mradi wa UNEP wa Mradi wa Kimataifa wa Peatlands (GPI), tunasaidia nchi 28 ikijumuisha Jamhuri ya Kongo (ROC), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Peru na Indonesia ili kuziwezesha kutunza rasilimali zao kwa njia endelevu.
Mabibi na mabwana, ushirikiano wa nchi za kiafrika ni muhimu kwa hatima ya sayari yetu.
Na nina imani kuwa tutaendelea kushuhudia uongozi imara barani Afrika tunapoendelea kutekeleza yale tuliyokubaliana wakati wa Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Mazingira, wakati tunapokaribia Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Mazingira utakaokuwa Madrid mwishoni mwa huu mwaka na ule utakaojiri Uchina mwaka wa 2020.
Takribani robo moja ya rasilimali duniani zinapatikana barani Afrika. Ninaona bara hili likiweka malengo yanayoweza kukadiriwa na yanayoweza kutekelezwa ili kudhibiti uharibifu wa bayoanuai kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa wa kushugulikia bayoanuai baada ya mwaka wa 2020. Hii ni kupitia kwa kuimarisha thamani ya bayoanuai kwa maisha, kwa utamaduni na ustawi kwa manufaa ya vitu vyote.
Kwa kubuni na kutekeleza sera, pia tunahitaji msaada wa viongozi kutoka kwa sekta ya fedha, sekta ya viwanda, sekta na upangaji wa ujenzi wa miji na sekta ya kilimo.
Tunahitaji kila msaada tunaoweza kupata. Hii ni kwa sababu hatimaye, vijana wanatarajia tuwajibike kwa sababu tunawaona kila mahali mijini mwetu, kuanzia Nairobi hadi Accra. Wanafahamu wanachokihitaji, na hatuwezi kuwafelisha.
Mabibi na mabwana, ukubwa wa changamoto hizi unaweza kutukatisha tamaa. Lakini tumejiami na elimu, vifaa na kujitolea kwetu ili kukabiliana na changamoto zilizopo. Na ninaamini kuwa bila shaka tutafaulu. Ninawatakieni kila la heri wakati mnapoweka historia kupitia kongamano la AMCEN.