Mganda, aliyekuwa mwalimu wa bayolojia na mkiambiaji wa masafa marefu Gerima Mustafa amemaliza kutembea umbali wa kilomita 664 katika eneo la Afrika Mashiriki ili kuhamasisha kuhusu hali ya miti ya shea katika eneo analotoka kaskazini magharibi mwa Uganda, eneo la Sudan na eneo la Sudan Kusini.
Mustafa anasema kuwa matumizi mabaya ya miti ya shea kuchoma makaa na kukata kuni ni hali 'iliyoweka vidonda rohoni mwake' na kumchombea kuchukua hatua. Anahofia kuwa inaweza kuangamia kabisa. Anajiita "Kamanda Mkuu wa Vuguvugu la Kuokoa Miti ya Shea" na mhamasishaji ambaye "husema na kutenda". Ananuia kukusanya fedha kuwezesha kampeni kubwa ya upandaji wa miti ya shea nchini Uganda na nchini Sudan Kusini.
Miti ya shea ilipatikana sanasana katika mifumo ya ekolojia inayopatikana katika maeneo ya ukanda wa mbuga na mwituni linalopatikana barani Afrika kutoka Somalia hadi Senegali.
Inasemekana biashara ya makaa, hasa kutokana na umaskini uliokithiri, vijana kukosa ajira na hitaji la kuni za kupikia mjini ndicho chanzo kikubwa cha kuangamia kwa miti ya shea nchini Uganda. Miti ya shea ambayo huchomeka polepole inaweza kuvutia mno wauzaji wa makaa, na wakulima wengi maskini ambao hujitolea kuiuza ili kugharimia vitu kama vile karo ya shule, bila kufikiria kuhusu madhara ya kudumu.
Hata hivyo, miti ya shea ni ya thamani kubwa siyo tu kutokana na bidhaa inayotokana nayo bali pia huduma ya mifumo ya ekolojia inayotoa.
Miti hii huzalisha matunda na kutupa mafuta—inayojulikana pia kama siagi ya shea—inayotumiwa kupika vyakula vya kiasili, kujipaka na kama dawa. Kwa kasi sasa, huuzwa nje ya nchi au kutumiwa kutengeneza vifaa vya kurembesha ngozi, vinavyoweza kupatikana madukani kote ulimwenguni.
Miti ya shea inaweza kuchukua miaka 10 kabla ya kuanza kuzalisha matunda lakini inaweza kuzalisha matunda kwa kipindi cha miaka 200, ijapokuwa wanasayansi kutoka Shirika la Kilimo cha Misitu Duniani wanasema kuwa ukuaji wa miti mipya huathiriwa na kilimo kinachotumia vifaa vya ukulima vinavyoharibu miche.
“Miti ya shea husaidia kuhifadhi unyevunyevu mchangani na kunufaisha kilimo," anasema Cathy Watson, Msimamizi wa mradi wa Maendeleo katika Shirika la Kilimo cha Misitu Duniani .
"Pia hutoa mchavuzo kwa nyuki, hutoa chakula kwa ndege na vipepeo, na kuwezesha kuwepo na mifumo dhabiti ya ekolojia.
Ijapokuwa mara nyingi ni wanawake ndio huvuna matunda ya shea, biashara ya makaa huendeshwa na wanaume hasa wasiokuwa wenyeji. Makaa hayo hupelekwa mijini mbali mno na miti inapokuzwa. Wakati mwingine hata huuzwa nje ya nchi.
"Wanawake wanahitaji shea, wanaume wahahitaji kipato," anasema Watson.
Na hiki ndicho chanzo cha matatizo na changamoto. Lakini pia inatoa fursa na kujadiliana na kupata suluhu.
"Tusihofie kukabiliana na vitu vunavyosababisha uharibifu wa ardhi na ni sharti tufanye uwekezaji zaidi, tutoe nafasi za ajira kwa vijana, tutunze mitu—huku tukiepuka uharibifu wa ardhi kama sehemu ya kuboreshaji," anasema Frank Turyatunga, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) wa Ofisi ya Ukanda wa Afrika. "Uboreshaj wa ardhi barani Afrika utaendeshwa na watu wa ngazi za chini," anaongezea.
Mustafa alitembea kwa masafa ya kilomita 664 kutoka Mjii Mkuu wa Uganda, Kampala hadi Nairobi, Kenya kwa siku 19. Alikaribishwa vyema na kusaidiwa na wahisani wakati wa safari hiyo.
"Watu wenye maarifa na wanaojitolea kama Gerima Mustafa ni mabalozi wa nia njema kwa jamii zao, nchi zao na kwa bayoanuai kwa jumla," anasema Musonda Mumba, mtaalamu wa UNEP wa masuala ya mandari na mwenyekiti wa sasa wa Ubia wa Kimataifa wa Misitu na Uboreshaji wa Mandhari.
"Tunahitaji wahamasishaji zaidi wa sampuli hii sio tu kuokoa miti ya shea bali pia kuokoa flora na fauna inayounda mfumo wa maisha hapa duniani tunamoishi na tunaoitegemea ili kuishi."
Suluhu kutokana na mazingira ndiyo njia mwafaka ya kuishi vizuri kama binadamu, ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutunza sayari tunamoishi. Hata hivyo mazingira yako hatarini, tunapopoteza aina ya viumbe mara 1,000 zaidi kuliko katika kipindi kingine chochote katika historia na kuna uwezekano wa aina milioni moja ya viumbe kuangamia. Mbali na kipindi muhimu cha kufanya maamuzi, ikiwa ni pamoja na kupitia COP 15 kuhusu Bayoanuai, 'mwaka mkuu' wa 2020 unatoa fursa kuu ya kuokoa mazingira yasiangamie. Hatima ya siku zijazo inategemea hatua tutakazochukua sasa.
Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia kuanzia mwaka wa 2021 hadi mwaka wa 2030, ukiendeshwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na wabia kama vile 'Africa Restoration 100 initiative', 'Global Landscapes Forum' na Muungano wa Kimataifa wa Utunzaji wa Mazingira, hushughulikia mifumo ya ekolojia katika maeneo ya nchi kavu na maeneo ya bahari. Wito unatolewa kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua, itapokea msaada kutoka kwa wanasasia, watafiti wa kisayansi na msaada wa kifedha ili kuboresha kwa kasi. Tusaidie kuboresha muongo huu.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na Abdelkader Bensada: Abdelkader.Bensada@un.org