Picha: Unsplash/James Donaldson
29 Jun 2022 Tukio Ocean & Coasts

Hatarini, bahari ni muhimu kwa mustakabali wa wanadamu: mtaalam wa UNEP

Picha: Unsplash/James Donaldson

Wiki hii, viongozi duniani wamekusanyika mjini Lisbon, Ureno, kwa  Kongamano la Bahari la Umoja wa Mataifa. Azimio la kisiasa linatarajiwa kutolewa.

Kongamano hilo linatokea wakati wa kipindi kinachorejelewa na wataalam kama muhimu kwa bahari duniani, ambayo inafanya kazi chini ya shinikizo la changamoto za tabianchi, uchafuzi uliokithiri na uharibifu wa bayoanuai.

Tuliketi na Leticia Carvalho, Mratibu Mkuu wa Tawi la Bahari na Maji Safi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), ili kujadili kinachopaswa kufanywa ili kutunza bahari duniani. 

Nazungumza kama mtaalamu wa masualaya ya bahari, uwekezaji katika bahari yetu ni uwekezaji katika kuwepo kwetu. 

Leticia Carvalho, UNEP

Kwa nini linajulikana kama kongamano la Bahari?  Je, si tuna bahari tano? 

Leticia Carvalho (LC): Tuna majina ya bahari tano kuzingatia jiografia yake - Pasifiki, Atlantiki, Hindi, Akitiki na Kusini. Lakini kwa kweli ni chanzo cha maji inayofunika zaidi ya asilimia 70 ya Dunia!  Kukifikiria kama chanzo kimoja cha maji ni kusisitiza umihimu wa kusimamia bahari kwa njia endelevu.  Kutunza sehemu za bahari kunahitaji kuitunza yote. Chochote kinachotokea katika sehemu moja ya bahari, kama vile uchafuzi wa plastiki au uvunaji wa mchanga, huathiri bahari nzima. 

Katika mwaka wa 2015, viongozi duniani walikubaliana kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 17, ili kudumisha kuwepo kwa watu na sayari. SDG 14, Maisha Chini ya Maji, iliweka malengo kabambe ya kutunza na kuboresha bahari. Hata hivyo, baadhi ya walioweka malengo ya 2020 hawajayafikiwa, na wengine hawaelekei kuyafikia. Tufanye nini ili kukabiliana na hali hii?

Leticia Carvalho (LC): SDG 14 ina uwezo mkubwa wa kushughulikia changamoto za aina tatu kwa sayari na kuimarisha ukuaji wa uchumi. Bahari ndio mfumo wetu mkuu zaidi wa ekolojia, na bado, ndio unaofadhiliwa kidogo zaidi kwa SDGs zote.  Hii haina mantiki unapoelewa kuwa maisha kwenye sayari kama tunavyojua yasingewezekana bila bahari bora.  Pengo la ufadhili linahitaji kurekebishwa kwa haraka.  Nikizungumza kama mtaalamu wa masuala ya bahari, uwekezaji katika bahari yetu ni uwekezaji katika kuwepo kwetu. 

Je, kuwekeza katika bahari kuna umuhimu gani kwa maisha yetu?

LC: Bahari hutoa nusu ya oksijeni tunayopumua na ina wajibu muhimu katika uthabiti wa hali ya hewa na ruwaza ya hali ya hewa tunayotegemea kukuza chakula. Bahari imekuwa muhimu katika kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa duniani na kufyonza joto la ziada kutoka hewani mwetu tangu nyakati za kabla ya viwanda. 

Uwekezaji katika SDG 14 ndiyo njia ya pekee ya kulinda spishi nyingi baharini huku ukiwezesha utalii, biashara, utoshelezaji wa chakula na maisha ya mabilioni ya watu.

Kwa nini Kongamano la Bahari la Umoja wa Mataifa ni muhimu sana?  

LC: Kongamano la Bahari linatarajiwa kutekeleza wajibu muhimu wa kuanzisha awamu mpya ya kushughulikia bahari - wajibu utakaoongozwa na sayansi, teknolojia, uvumbuzi na fedha. Linatokea wakati muhimu ambapo ulimwengu unataka kushughulikia matatizo mengi yaliyokita mizizi katika jamii zetu - matatizo ambayo yanahitaji masuluhisho yanayojikata kwenye SDGs. 

Peter Thomson, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Bahari, anasema, udhabiti na ustahimilivu wa bahari una mwisho.

Nini ujumbe wako kwa wanaohudhuria?

LC: Ombi langu kwa viongozi wa dunia ni kujitokeza na kufanya mabadiliko yanayohitajika ili kubadilisha sera, biashara na mitindo ya maisha ili kuwa endelevu zaidi, isiyodhuru wala kuharibu bahari. Mojawapo ya wito wangu mkuu ni kukomesha ruzuku hatari zinazowezesha kutumia bahari kupindukia na kudhuru masuluhisho endelevu.  Ubunifu hauwezi tu kushindana na bei za chini zisizokuwa za kweli.

Watu wa kawaida wanaweza kufanya nini ili kutunza na kuboresha bahari?

LC: Ushauri wangu utakuwa kufanya maamuzi yanayojali bahari wakati wa kununua bidhaa au chakula kutoka baharini kutumia tu unachohitaji.  Fanya mabadiliko madogo kwa maisha yako ya kila siku ili kupunguza kiwango cha gesi ya ukaa, ambacho kinachangia kuongezeka kwa urari wa bahari.  Na usisahau kwamba sote tunaweza kupigania bahari.  Unafanya uamuzi mwafaka kwa kuunga mkono kampuni zinazojaribu kuunga mkono mambo yanayojali mazingira.  Kadiri tunavyofanya maamuzi kwa uelewa zaidi kama watumia bidhaa ndivyo mashirika ya biashara yatakavyowajibika.

Je, UNEP inasaidia vipi kutunza bahari?

LC: UNEP inafanya kazi na washirika wa ndani na wa kimataifa, kama vile serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na sekta ya kibinafsi, kutoa sayansi inayowezesha kuchukua hatua za kisera na kuhamasisha umma kuhusu vitisho kwa bahari. Tunafanya kazi na serikali ili kusaidia kuunda maeneo ya bahari yaliyohifadhiwa.  Tunatumia uwezo wetu wa kuitisha mitano kote duniani kutoa wito wa kupunguza kiwango cha gesi ya ukaa kinachizalishwa na binadamuhasa katika sekta zinazohusiana na bahari.  Pia tunaunga mkono miradi muhimu, kama vile Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Sayansi ya Bahari ili kuwa na Maendeleo Endelevu na Mfuko wa Kimataifa wa Miamba ya Matumbawe

Je, umeona hatua za kutia moyo katika jitihada za kutunza bahari?

LC: Ndiyo. Nchi nyingi zinaahidi kuunda maeneo ya bahari yaliyohifadhiwa  na kutekeleza mikakati mingine madhubuti wa kuhifadhi kutegemea eneo.     Pia tunaona kuongezeka kwa uzingatiaji wa maarifa ya kiasili. Haya ni muhimu ili kufanikiwa. Jamii za kiasili zimeishi kwa amani na mazingira kwa karne nyingi kupitia mikakati iliyofanyiwa majaribio.   

Hatimaye, katika Mkutano wa tano wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini Nairobi, Kenya, mwezi wa Machi mwaka wa 2022, Nchi Wanachama zilikutana kupitia chombo cha kihistoria kinachoziunganisha kote duniani ili kukabiliana na uchafuzi wa plastiki, ikjumuisha mazingira ya baharini. Hii itafikia kilele katika mwaka wa 2024, kasi ya kuvunja rekodi kwa makubaliano ya kimataifa kama haya.

 

Kongamano la Bahari, lililoandaliwa kwa pamoja na Serikali za Kenya na Ureno, linatokea wakati muhimu ambapo ulimwengu unatafuta kushughulikia matatizo mengi yaliojikita katika jamii yetu yaliyofichuliwa na janga la COVID-19 na ambayo yanahitaji  mabadiliko makubwa ya kimuundo na masuluhisho ya pamoja ambayo yamejikita katika SDGs.  Ili kuhamasisha uchukuaji wa hatua, mkutano huo utatafuta kuekuza masuluhisho ya kibunifu yanayohitajika sana kwa kuzingatia sayansi yanayolenga kuanzisha awamu mpya ya kushughulikia bahari duniani.

 

Maudhui Yanayokaribiana