Sheldon Cooper/ SOPA Images/Sipa USA via Reuters
20 Jan 2021 Tukio Matumizi bora ya rasilimali

Kukuza chakula endelevu

Sheldon Cooper/ SOPA Images/Sipa USA via Reuters

Watu wengi wameapa kuwa wataanza kufanya mazoezi, kula matunda zaidi na kula mboga zaidi kama sehemu ya maazimio ya Mwaka Mpya. Lakini je, itakuwaje ikiwa maazimio ya mwaka huu hayatajihusisha tu na chakula – ila yatajumuisha kupunguza kiwango cha mazao ya lishe bora yanayotupwa?

Huku ndiko kujitolea ambako Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linatarajia ili kuwezesha kufikia Ajenda ya Maendeleo Endelevu.

Makadirio kote ulimwenguni yanaonyesha kuwa takribani theluthi moja ya mazao ya chakula cha binadamu huharibika au kutupwa kila mwaka. Tani bilioni 1.3 ya matunda, mboga, nafaka, na mimea ya mizizi hupungua kupitia kwa umwagikaji au kuharibika kupitia mifumo ya jinsi inavyoshughulikiwa kutoka mashambani hadi sokoni, au kuharibika na kumwagika mikononi mwa wauzaji na hatimaye mikononi mwa watumiaji.

Katika dunia inashohudia utapiamlo unaochangia takribani asilimia 45 ya vifo miongoni mwa watoto chini ya umri wa miaka mitano katika nchi zinazoendelea, na wakati ambapo matumizi ya vyakula vilivyosagwa mno vinachingia kuongezeka kwa idadi ya watu wanene mno, kuwajibikia maazimio ya Mwaka Mpya siyo suala la kutekelzwa tu na mtu binafsi – ni muhimu mno kama sehemu ya ubinadamu.

Ni muhimu pia kwa maslahi ya sayari yetu. Uzalishaji, matumizi na uharibifu wa chakula - na athari yake kwa mazingira - ni mada muhimu itakayojadiliwa mwaka huu wakati wa Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEA-5), utakaojiri mtandaoni kati ya tarehe 22 na tarehe 23 mwezi wa Februari mwaka wa 2021.

UNEP na wabia wanakuza uchanganuzi wa kina wa data kote ulimwenguni inayohusiana na uharibifu wa chakula, ambayo itazinduliwa wakati wa mkutano huo mkuu. Chini ya mada 'Food Waste Index', makala hayo yatatolewa kwa umma wakati wa UNEA-5. Inatoa makadirio mapya ya chakula kwa kila nyumba, kwenye sekta za uuzaji na na utoaji wa huduma za chakula katika ngazi ya taifa, na kutoa methodolojia itakayowezesha nchi kupima na kufuatilia Lengo la Maendeleo Endelevu la 12.3, hali inayolenga kupunguza maradufu uharibifu wa chakula unaofanywa na wauzaji na watumizi wa chakula na kupunguza kiwango cha chakula kinachopungua kufikia mwaka wa 2030.

A farmer shows oranges harvested at a farm in El Nobaria, northeast of Cairo
Mkulima anaonyesha mazao machungwa yaliyovunwa katika shamba la El Nobaria, kaskazini mashariki mwa Cairo. Picha: Reuters/Mohamed Abd El Ghany

Mifumo ya baadaye ya chakula

Kilimo na msukumo wa kuzalisha bidhaa kwa bei nafuu, na kwa haraka iwezekanavyo ni sehemu ya chanzo kikuu cha uharibifu wa bayoanuai. Uzalishaji wa chakula unaohitaji rasilimali nyingi unaotegemea mno maatumizi ya mbolea, kemikali za kuua wadudu na unyunyiziaji wa maji unaotegemea mifumo changamano na mifumo changamano ya nishati inamaanisha nafasi ya kukaliwa na wanyamapori inapungua, ikijumuisha ndege, mamalia, wadudu na vijidudu. Kwa sasa, mifumo ya kisiasa na kiuchumi inagharimu wakulima mashamba yao.

"Janga la corona (COVID-19) lilionyesha vizingiti na vizuizi katika mifumo yetu ya kimataifa ya chakula. Tuna fursa ya kujiimarisha vyema baada ya korona na kuangalia upya jinsi tunavyopanda, vuna, uza na kula aina mbalimbali ya mazao kutoka kwa mazingira," alisema Clementine O'Connor, kutoka UNEP anayefanya kazi na Programu ya Mifumo ya Chakula Endelevu.

Kufanyia marekebisho mifumo yetu ya chakula hakutasaidia tu kuboresha bayoanuai na maeneo ya makazi lakini pia kunaweza kuimarisha fursa sokoni kwa wakulima wadogowadogo – ambao wengi wao ni wanawake wanaojikwamua kifedha kupitia uzalishaji endelevu wa matunda na mboga.

Ni mwaka wenye mafanikio?

Wakati wa UNEA-5, mkutano utakaondeshwa kupitia mtandaoni na wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, sekta binafsi, mashirika ya uraia, wanasayansi na viongozi wengineo utatoa fursa ya kushiriki na kukumbatia matendo mema yatakayoleta mabadiliko kwa mifumo ya chakula. Safari ya kuelekea kuwa na uzalishaji ya matumizi ya chakula kwa njia endelevu itakayotokana na mkutano huo mkuu itaendelea kuanzia mwaka wa 2021 kuendelea, huku mtutano wa kwanza kuwahi kutokea wa UN, Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula.

Mwaka wa 2021 umetengwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula (FAO), kama Mwaka wa Kimataifa wa Matunda na Mboga wa 2021 kuonyesha umuhimu wa matunda na mboga kwa lishe ya binadamu, maisha ya binadamu, kuwepo na chakula cha kutosha na kuwa na afya njema.

covid-19 response logo

Maudhui Yanayokaribiana