Karoo, eneo linalopatikana Afrika Kusini, ni mahali ambapo ni vigumu kupata kipato kutokana na kilimo—sehemu kubwa ya eneo hilo haina maji kwenye ardhi. Jina lake linatokana na neno la Kikhoisani lenye maana ya “ardhi yenye kiu”.
Tangu jadi, ardhi hiyo ilitumiwa na wafugaji lakini, kiangazi, kulisha mifugo hadi majani yaishe na kuvamiwa na wanyama pori kulipelekea shughuli hii kuwa hatari. Vitu vinavyowinda na kula wanyama vilidhibitiwa kwa kutumia ua, mitego, sumu na uwindaji. Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi yenye maeneo makubwa yaliyowekewa ua ulimwenguni. Hali hii ina athari kubwa kwa bayoanuai na kwa matembezi ya wanyama.
Kwa sasa, uchunguzi mpya wa majaribio unaofanywa kwa hekta takribani 25,000 na unaojumuisha wachungaji, umefaulu kuongeza idadi ya wanakondoo wanaozaliwa na ongezeko la nyama ya ng'ombe katika ardhi wazi ya kuchungia huku ikisaidia kukuza mimea na kuimarisha bayoanuai kwa wakati mmoja.
Fair Game ni ubia kati ya Wakfu wa Landmark, Idara ya Kitaifa ya Kushughulikia Masuala ya Mazingira na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Mradi unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani, Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini na wahisani kutoka Afrika Kusini. Ni njia ya kipekee ya kutumia wachungaji(binadamu) katika mashamba makubwa ya biashara ya ufugaji.
Mojawapo ya kazi ya mchungaji ni kutengeneza kraals zinazoweza kuhamishwa, au mahali pa kufungia mifugo ili kulinda kondoo na mifugo dhidi ya wanyama vamizi, hasa mbweha mwenye mgongo mweusi na paka wa mwituni.
kraals, zilizotengenezwa kutokana na nyavu za mizigo zilizounganishwa kwa kutumia vigingi vya chuma, huwekwa katika maeneo yaliyo hatari mno na hutumiwa usiku. Virutubishi kutoka kwa kinyesi cha wanyama na kwato zinazosaidia kupasua ardhi ndani ya kraals husaidia kuboresha ardhi iliyoharibika. Ili kuzuia kulisha mifugo hadi majani yaishe wakati wa mchana,kraals huhamishwa kila juma.
“Kutokana na kuwepo kwa wachungaji na matumizi ya kraals kwa miezi 30 iliyopita, licha ya kiangazi kibaya katika eneo hilo, idadi ya mifugo imeongezeka kutoka kwa kondoo wa kike 1,000 hadi kuwa na kondoo 2,000, na kutoka kwa ng'ombe 250 hadi 360,” anasema Bool Smuts, Mkurugenzi wa masuala ya mazingira, daktari wa binadamu na mkurugenzi wa Wakfu wa Landmark.
"Katika kipindi kiki hiki, hakuna rekodi iliopo ya wanyama walioripotiwa kupotea kutokana na kuvamiwa, swala lililopelekea kufaulu kupunguza kabisa mzozo wa uvamizi kutoka kwa binadamu au kutoka kwa wanyama vamizi. Katika kipindi cha hivi majuzi kilichoshuhudia kiangazi kibaya mno, tulifaulu kutunza mifugo vizuri na kutunza veld [kiwanja] pia tulipunguza chakula cha ziada,” aliongezea.
Fair Game ina manufaa kwa mpango wa mfumo wa ekoloji uhaohusisha ufuatiliaji na utathmini wa karibu unawezesha shughuli ya uzalishaji wa mifugo kwa njia rafiki na wanyama-pori unaozingatia maslahi ya wanyama na kufanya jamii kuwajibika. Mpango huo uliokaguliwa na kuidhinishwa na Shirika la Wiwanda vya Nyama la Afrika Kusini, unakuza bayoanuai, na kutunukia wazalishaji wanatunza mashamba yao kwa kuzingatia utunzaji wa ekolojia kifedha.
Wanyama vamizi huwinda wawindo yake asilia
Manufaa kwa bayoanuai ya kuwa na wachungaji ni kwamba, wanyama vamizi walio huru wamegundua maeneo wanayoweza kuwinda wawindo yao asilia bila kuwalenga mifugo. Na manufaa ya kiafya kwa mifugo na ya utunzaji wa mifugo kutokana na kuwa na wachungaji ni kukuwa na ukaguzi na ufuatiliaji wa kila siku wa mifugo unaoweza kupelekea kugundua mapema mifugo walio na majeraha au walio magonjwa. Ijapokuwa kuachisha kondoo kunyonya na kuanza kuwapa chakula kulifaulu kwa asili mia 70 kabla ya kuwa na wachungaji, hali hii sasa imeimarika zaidi, anasema Smuts.
“Tulitaka kutekeleza mtindo mbadala wa ufugaji wa mifugo unaokabiliana na hali ya kulisha mifugo hadi majani yaishe, majangwa na madhara mabaya kwa bayoanuai na kuepukana na njia hatari za kukabiliana na wanyama vamizi. Tumenufaika kutokana na utafiti uliochukua zaidi ya karne kuhusu chui na uchunguzi wa mzozo wa wanyama wadogo wanaowinda na kuua mifugo uliofanywa na Wakfu wa Landmark,” anaongezea.
Wachungaji hufanya kazi wakibadilishana zamu kwa mda wa siku sita: masaa 24 mara mbili, masaa 8 mara mbili na kuchukua ofu ya masaa 48. Wanalipwa asili mia 70 zaidi kuliko ujira wa kawaida wa wafanyakazi wa shambani na kazi yao huonewa fahari mashambani.
“Mashamba ya Fair Game yamesaidia kuzuia kuharibika kwa veld na pia yamewezesha kustahimili kiangazi hali ambayo imewezesha wakulima wa Fair Game, sio tu kuongeza idadi ya mifugo yao wakati wa kiangazi, bali pia kuuza kondoo na ng'ombe kwa bei nzuri," anasema Jane Nimpamya, Meneja wa Mfuko wa Mazingira Duniani. “Mradi huu unaweza kutekelezwa katika maeneo mengine kame ambayo wakulima wa mifugo wanakabiliwa na changamoto ya wanyama wanaowinda na kuua mifugo wao,” anaongeza.
Katika mwezi wa Mei mwaka wa 2019, Mradi wa Wakfu wa Landmark wa Kurejesha Bayoanuai kupitia Uchungaji 'Shepherding Back Biodiversity Project' (Fair Game ni mshirika) ulitambuliwa kwa huduma zake zinazosaidia na kuitunza sayari wakati wa hafla ya kila mwaka ya Eco-Logic Awards.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na Jane Nimpamya au Bool Smuts