Nchi ya Burkina Faso inatekeleza mikataba kadhaa ya kimataifa kuhusiana na mazingira – ikijumuisha Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii (2016 hadi 2020), inayolenga "kukuza uchumi dhabiti, usiobagua kwa njia endelevu". Ila mabadiliko ya kudumu si suala dogo. Katika mwaka wa 2019, nchi ya Burkina Faso iliorodheshwa nambari 141 kati ya nchi 162 kwa kuzingatia hatua iliyopiga kufikia Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.
Akaunti ya Maendeleo na Umoja wa Mataifa (UNDA) ni mradi wa miaka minne, ulioubuniwa kuwezesha taasisi za kitaifa kutekeleza na kufuatilia kikamilifu vipengele vya mazingira vya Ajenda ya 2030. Kuuongezea kwa kuunda sera na mikakati ya kitaifa, nchi zinazoshiriki husaidiwa kuunda data za kina za mazingira, na kuzitoa mara kwa mara na kushiriki maarifa kupitia mitandao ya kikanda.
Afisa wa Kuratibu Maendeleo wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Jean Jacob Sahou anajadili mafanikio na changamoto za mradi huo nchini Burkina Faso – ikijumuisha kazi yake wakati wa COVID-19.
Nchi zinapaswa kuelewa kipengele cha mazingira katika Malengo ya Maendeleo Endelevu na uhusiano wake na ahadi nyinginezo na kuweza kuchukua hatua dhabiti.
Maendeleo endelevu yana umuhimu gani kwenye mpango wa Burkina Faso wa kukuza uchumi?
Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii (PNDES) unalenga kukuza uchumi usiobagua kupitia utenganezaji na utumiaji wa bidhaa kwa njia endelevu. Mojawapo ya malengo yake makuu ni "kukabiliana na mienendo ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kuwa usimamiaji wa malighafi na rasilimali za mazingira unaendeshwa kwa njia endelevu".
Kufikia malengo ya mazingira kutatuwezesha kufikia matarajio makuu ya Ajenda ya 2030 na Malengo yake ya Maendeleo Endelevu 17. Nchi zinapaswa kuelewa kipengele cha mazingira katika Malengo ya Maendeleo Endelevu na uhusiano wake na ahadi nyinginezo na kuweza kuchukua hatua dhabiti. Taasisi za kitaifa zinapaswa kurekebisha jinsi zinavyofanya maamuzi, kubuni sera, kutunga sheria na kuripoti kuhusu masuala ya maendeleo endelevu: inamaanisha kuhakikisha taarifa sahihi na maarifa vinapatikana kwa urahisi, kushirikiana na kuwa na uratibu unaokata sekta mbalimbali – ndani na nje ya taasisi, na kuweka taratibu bila ubaguzi.
UNDA husaidia vipi ujumuishaji wa masuala ya mazingira kwenye sera ya umma?
Ili kushughulikia mahitaji yaliyopo, mradi wa UNDA umeundwa ili kujenga uwezo wa taasisi kitaifa kuziwezesha kutekeleza na kufuatilia kikamilifu vipengele vya mazingira vya Ajenda 2030 katika njia inayoeleweka na jumuishi; na kuunda data ya kiwango cha juu ili kuwezesha kufanya uamuzi na kuongoza utekeleza wa Ajenda nchini Burkina Faso.
Kufanikisha mradi huu, UNEP hushirikiana na mashirika mengine na taasisi za serikali Nchini Burkina Faso, Vikosi vya Umoja wa Mataifa katika nchi, na Waratibu wa Nchini wa UN, na mifumo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ili kujengea wahusika wakuu uwezo wa kiufundi katika wizara husika - ikijumuisha wizara za maendeleo, fedha, kilimo, na mazingira - kutekeleza na kufuatilia kikamilifu vipengele vya mazingira vya Ajenda ya 2030 katika njia iliyoratibiwa, jumuishi na inayoweza kupimika kisayansi; na ofisi za kitaifa za data ili kuweza kutoa data ya kina kuhusiana na mazingira, data na taarifa zinazojumuisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) na data kuhusu Mikataba ya Kimataifa ya Mazingira (MEA)
Mradi huu umekabiliana vipi na changamoto kutokana na ugonjwa wa korona?
Licha ya changamoto kutokana na mkurupuko wa ugonjwa wa korona, UNEP ilinufaika na msaada wa wabia kama vile Jumuia ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mazingira; na hivyo mradi wetu uliendeleza makongamano kadhaa katika mwezi wa Machi mwaka wa 2020. Hii ilijumuisha mafunzo ya jinsi ya kutumia 'Analytical Grid' ya Maendeleo Endelevu kwa wanachama wa kamati ya mikataba ya kimataifa kuhusiana na mazingira, na kutoa mafunzo ya kitaifa ya Kutathmini Ukuaji wa Kimazingira na Kutathmini Ukuaji wa Uwezo wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ili kuwezesha mashiriki kujumuisha vyema maendeleo endelevu, ukuzaji wa mazingira na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mikakati ya maendeleo katika ngazi ya eneo na ngazi ya kitaifa. Wahusika pia hujengewa uwezo wa kutumia vifaa vya kufuatilia mabadiliko katika mikakati ya maendeleo katika ngazi ya eneo na miradi inayohusu mabadiliko ya tabianchi.
Je, ni vipi ambavyo nchi imejiandaa kufikia mikakati ya kitaifa na Malengo ya Maendeleo Endelevu?
Mradi huu umeboresha hali ya kujengea taasisi uwezo katika ngazi ya eneo na ngazi ya kitaifa kuhusiana na masuala ya kukuza mazingira endelevu na kuyajumuisha katika michakato muhimu ya maendeleo, ikijumuisha vingele vya uchumi, mpangilio na data.
Tafiti-zinazojumuisha ule wa COVID-19-zitakuwa muhimu wakati a kuchangua matokeo ya PNDES zijazo, zitakazojumuisha vipengele dhabiti vya mazingira na kuingiliana mno na Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Kutokana na hali hii, serikali inajengewa uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yake chini ya Ajenda 2030, ikijumuisha uwezo wa kutoa taarifa katika ngazi ya kimataifa kuhusu hatua zake za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Kwa kuzingatia umuhimu mkuu wa mikataba ya kimataifa kuhusu mazingira na malengo yake, ibara zake pia hushughulikia vifaa vya kiufundi na msaada unaotolewa kupitia mradi huu, ambao hatimaye utasaidia nchi ya Burkina Faso kuwa na uelewa mpana kuhusu uanuai wa malengo ya mazingira yanayopaswa kufikiwa.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Jean Jacob Sahou: jean-jacob.sahou@un.org.