Curioso Photography/Unsplash
29 Jun 2021 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Nchini Tanzania, wenyeji na viongozi waungana pamoja kuokoa mikoko

 

Siku ya Kimataifa ya Tropiki, ambayo huadhimishwa tarehe 29 mwezi wa Juni, inalenga kuhamasisha kuhusu changamoto za kipekee ambazo mataifa ya tropiki hukabiliana nazo kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ukataji miti na ukuzaji wa miji. Kuadhimisha hafla hiyo, UNEP inaangazia kisa cha mwezi wa Julai mwaka wa 2020 kuhusu jamii moja nchini Tanzania inavyokabiliana na uharibifu wa mifumo mikuu ya ekolojia ya maeneo ya tropiki  uliofanyika kwa miaka: mikoko.

  • Tangu kisa hicho kilipochapishwa, mradi huo ulifanya uctafiti katika vitongoji kumi vya Rufiji delta kuhusu uharibifu na matumizi ya mikoko. Utafiti huo ulionyesha kuwa mikoko ilikuwa imepungua kwa takribani asilimia 20 kwa kipindi cha miongo mitatu kutoka kiwango cha takriban mikoko 53,000 katika mwaka wa 1989 hadi kati ya mikoko alfu 43 na alfu 45 katika mwaka wa  2019.
  • Kozi mpya inayota mafunzo kwa wakufunzi pia inasaidia kuunda na kuendesha vilabu vya mikoko shuleni vitakavyohusisha na kuelimisha jamii ya wenyeji.

Kwa watu wengi kati ya watu 30,000 ambao wanaishi katika vitongoji vya Rufiji Delta Kaskazini mwa Tanzania, maisha yanahusu kitu kimoja: mikoko.

Miti hii na vichaka, ambayo hunawiri katika maji ya delta ya chumvi, hutumiwa kupata vifaa vya ujenzi, kuni na mapato, na hutoa mbao zinazothaminiwa ambazo mara nyingi wakazi huziuza ili kujikimu.

Lakini mikoko, ambayo pia ni makazi ya spishi nyingi, kama vile samaki aina ya ray, hongwe, ndege wanaohamahama na kobe wa baharini, wakati mwingine huchukuliwa kama vizingiti vinavyopaswa kukatwa, kwa kukalia ardhi ambayo inaweza kutumika kukuza mpunga na kuchungia mifugo . Utegemeaji wa mikoko kupita kiasi namna hiyo katika Rufiji Delta, makao ya asilimia 50 ya mikoko nchini Tanzania, umesababisha kupungua kwa misitu hii, na kutishia maisha ya wakazi.

Mradi mpya unakusudia kubadili mwenendo huo na kuhimiza usimamizi endelevu wa mikoko ya delta. Mradi huo unasimamiwa na Taasisi ya Sayansi ya Bahari (IMS) ya Tanzania kwa kushirikiana na Huduma ya Misitu Tanzania, Wetlands International, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, na Kikundi cha Utamaduni na Mazingira cha Pakaya. 

Itapelekea viongozi na jamii za wenyeji kufanya kazi pamoja kuunda mpango wa kusimamia misitu ya mikoko, huku wakiweka sheria kuhusu mahali na wakati wa kuivuna. Mifano hiyo pia itafanyia majaribio mbinu za kurejesha misitu katika maeneo ambayo tayari yameathiriwa na maendeleo, hali itakayosaidia wakazi wa delta kufurahia manufaa ya mikoko katika siku zijazo. Juhudi zao za uboreshaji zitazingatia Miongozo ya Uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia katika Ukanda wa Bahari ya Hindi Magharibi, chapisho jipya kutoka kwa Nairobi Convention na wabia ambao hutoa mwongozo wa hatua kwa hatua kuhusu jinsi ya kukuza miradi ya kurejesha misitu kwa ufanisi na kuepuka changamoto za kawaida wakati wa kupanda miti tena.

Mikoko huhifadhi kaboni zaidi ya mara tano kuliko misitu ya maeneo ya ardhi.

Jared Bosire, Meneja wa Mradi, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

Eneo lisilomilikiwa na yeyote

Mikoko, miti inayonawiri vyema katika maji ya chumvi na ambayo hupatikana katika ukanda wa pwani katika maeneo yenye joto kote ulimwenguni, ni nguzo kwa mifumo mingine ya uzalishaji wa kiwango cha juu duniani. Haitoi tu maeneo ya kuzaliana kwa samaki, krasteshia na spishi nyingi zilizo hatarini kuangamia, lakini pia zinatunza fukwe dhidi ya kumomonyoka na kukinga wanadamu dhidi ya mafuriko, vimbunga na dhoruba nyinginezo. Walakini ulimwenguni kote, baadhi ya wataalam wanakadiria kwamba hadi asilimia 55 ya mikoko imedidimia tangu miaka ya 1990.

“Mbali na kutunza mifumo mikuu ya ekolojia, mradi wa Rufiji Delta utasaidia Tanzania kufikia ahadi zake chini ya Malengo ya Maendeleo Endelevu mbalimbali, hasa Lengo la 14 kuhusu 'Maisha Chini ya Maji' na Lengo la 13 kuhusu hatua za kushughulikia mazingira," alisema Jared Bosire, Meneja wa Mradi wa UNEP wa Programu ya Bahari ya Kikanda. "Kwa kweli, mikoko huhifadhi kaboni zaidi ya mara tano kuliko misitu ya maeneo ya nchi kavu."

Man standing next to a mangrove sapling
Mikoko michanga katika Delta ya Rufiji nchini Tanzania. Picha: Nairobi Convention

A local effort

Of critical importance, say experts, is the active role local communities will play in the project, particularly in choosing rehabilitation sites and developing harvesting plans.

“I have been involved with many projects over the years that have attempted to reverse the degradation of the mangroves of Rufiji,” said Jumani Yusuf Kikumbe, Outgoing Chairperson of the Nyamisati Village Committee. “These efforts need to include communities from the beginning in an equitable way if they are to be successful.”

IMS and the other project partners hope that lessons from the Rufiji Delta initiative can be applied elsewhere in Tanzania, and across the entire Western Indian Ocean region where mangroves are under similar pressures.

The initiative is being funded by the Global Environment Facility through the Implementation of the Strategic Action Programme for the Protection of the Western Indian Ocean from Land-Based Sources and Activities, executed by the Nairobi Convention. The convention, part of UNEP’s Regional Seas programme, serves as a platform for governments, civil society and the private sector to work together for the sustainable management and use of the Western Indian Ocean’s marine and coastal environment. 

 

Juhudi za wenyeji

Cha muhimu mno, wataalam wanasema, ni jukumu linalotekelezwa na jamii za wenyeji katika mradi huo, hasa katika kuchagua maeneo ya kuboreshwa na kukuza mipango ya uvunaji.

"Nimeshiriki kwenye miradi mingi kwa miaka iliyopita ambayo imejaribu kukabiliana na uharibifu wa mikoko ya Rufiji," alisema Jumani Yusuf Kikumbe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kijiji cha Nyamisati anayestaafu. "Jitihada hizi zinahitaji kujumuisha jamii kutoka mwanzo kwa njia ya usawa ikiwa tunataka kufanikiwa."

IMS na wabia wengine wa mradi wanatumai kwamba mafunzo kutoka kwa mradi wa Rufiji Delta yanaweza kutumika kwengineko nchini Tanzania, na katika eneo lote la Bahari ya Hindi Magharibi ambapo mikoko iinapitia changamoto zilezile.

Mradi huo unafadhiliwa na Kituo cha Mazingira Duniani kupitia kwa Utekelezaji wa Programu ya Mikakati ya Kutunza Bahari ya Hindi Magharibi Dhidi ya Visababishi na Shughuli za Maeneo ya Ardhi, na kutekelezwa na Nairobi Convention. Mkataba huo, sehemu ya programu ya UNEP Bahari za Kikanda, unatumika kama jukwaa la serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi kufanya kazi pamoja ili kuwa na usimamizi na utumiaji endelevu wa mazingira ya Bahari ya Hindi Magharibi na maeneo ya pwani. 

 

Muongo wa UN wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia 2021–2030, unaosimamiwa na UNEP, Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa na wabia kama vile mradi wa Africa Restoration 100, Jukwaa la Kimataifa la Mandhari na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mazingira(IUCN), unashughulikia mifumo ya ekolojia ya nchi kavu, pwani na baharini. Wito wa kuchukua hatua ulimwenguni, utafaidi msaada wa kisiasa, utafiti wa kisayansi na taasisi na fedha ili kufanya uboreshaji kwa kiwango kikubwa. Tusaidie kushughulikia Muongo.

Kupata taarifa kuhusu hali inavyoendelea, tafadhali tembelea www.nairobiconvention.org 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Angela Patnode (angela.patnode@un.org)