- Mitiririko ya fedha za kimataifa za umma za kukabiliana na hali kwa nchi zinazoendelea iliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 22 katika mwaka 2021 hadi dola za Marekani bilioni 28 katika mwaka wa 2022.
- Hata kufikia lengo la Mkataba wa Tabianchi wa Glasgow wa kuongeza ufadhili wa kushughulikia hali maradufu kunaweza tu kupunguza pengo la kifedha la kukabiliana na hali hadi kwa angalau Dola za Marekani bilioni 38 kufikia mwaka wa 2025 kunaweza tu kupunguza pengo la kifedha la kukabiliana na hali kwa kati ya dola za Marekani bilioni 187 na bilioni 359 kwa takriban asilimia 5.
- Pamoja na ufadhili na utekelezaji mkubwa wa kushughulikia athari zinazoongezeka za mabadiliko ya tabianchi, juhudi kubwa zinahitajika za kujengea uwezo na uhamishaji wa teknolojia.
Nairobi, Novemba 7, 2024 – Kadiri athari mbaya za tabianchi zinavyozidi kuongezeka, na kuumiza watu maskini duniani zaidi, Ripoti ya UNEP ya Kukabiliana Na Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2024: Liwe liwalo , kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), inaonyesha kuwa mataifa ni sharti yaimarishe juhudi za kukabiliana na hali, kuanzia na kujitolea kuchukua hatua kuhusu ufadhili katika COP 29.
Ongezeko la wastani la joto duniani linakaribia nyuzijoto 1.5 zaidi kuliko viwango vya kabla ya viwanda, na ubashiri wa hivi punde kutoka kwa Ripoti ya Pengo la Uzalishaji wa Hewa Chafu ya UNEP ilionyesha ulimwengu unaelekea kushuhudua ongezeko hatari la nyuzijoto kati ya 2.6 na 3.1 karne hii tusiposhuhudia kupunguzwa kwa kiwango cha juu cha uzalishaji wa gesi ya ukaa haraka. Ripoti inayotolewa tunapoelekea majadiliano kuhusu tabianchi katika COP 29 mjini Baku, Azerbaijan, ripoti hii inaonyesha kuwa kuna hitaji la dharura la kuimarisha kwa kiwango kikubwa kukabiliana na hali katika muongo huu ili kukabiliana na athari zinazoongezeka. Lakini hali hii inatatizwa na pengo kubwa lililopo kati ya mahitaji ya kifedha ya kukabiliana na hali na mtiririko wa sasa wa fedha za kimataifa za umma za kukabiliana na hali.
"Mabadiliko ya tabianchi tayari yanaathiri vibaya jamii kote ulimwenguni, haswa maskini zaidi na walio hatarini zaidi kuathirika. Dhoruba kali zinaangusha nyumba, mioto misituni inaangamiza misitu, na uharibifu wa ardhi na ukame vinaharibu mandhari ya mazingira,” alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Watu, kipato chao na mazingira wanayoyategemea yako hatarini kwa kweli kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Bila kuchukua hatua, hiki ni kielelezo cha mustakabali wetu na kwa nini hakuna sababu kwa ulimwengu kutokuwa makini kushughulikia hali, sasa."
Mitiririko ya fedha za kimataifa za umma za kukabiliana na hali kwa nchi zinazoendelea uliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 22 katika mwaka wa 2021 hadi dola za Marekani bilioni 28 katika mwaka wa 2022: ongezeko kubwa kabisa la mwaka baada ya mwaka tangu wakati wa Mkataba wa Paris. Hali hii inaakisi hatua zilizopigwa kuzingatia Mkataba wa Tabianchi wa Glasgow, ambao ulihimiza mataifa yaliyoendelea angalau yaongeze maradufu fedha za kukabiliana na hali kwa nchi zinazoendelea kutoka takriban Dola za Marekani bilioni 19 katika mwaka wa 2019 kufikia mwaka wa 2025. Hata hivyo, hata kufikia lengo la Mkataba wa Tabianchi wa Glasgow kunaweza tu kupunguza pengo la kifedha la kukabiliana na hali hiyo, ambalo linakadiriwa kuwa dola za Marekani kati ya bilioni 187 na bilioni 359 kwa mwaka, kwa takriban asilimia 5.
Nchi zinazoendelea zinaposhuhudia hasara na uharibifu unaoongezeka, tayari zinapambana na kuongezeka kwa mzigo wa madeni. Ushughulikiaji madhubuti na wa kutosha wa hali, unaojumuisha haki na usawa, unahitajika kwa dharura zaidi kuliko hapo awali. Mataifa yanaweza kuimarisha ukabilianaji wa hali kwa kupitisha lengo jipya thabiti la takwimu za pamoja kuhusu ufadhili wa tabianchi katika COP 29, na kwa kujumuisha vipengele madhubuti vya kukabiliana na hali katika awamu inayofuata ya ahadi zao za kushughulikia tabianchi, au michango inayoamuliwa na taifa, inayotarajiwa mapema mwaka ujao kabla ya COP 30 mjini Belém, Brazil.
Mikakati na utekelezaji wake hucheleweshwa
Kuhusiana na mikakati, nchi 171 kwa sasa zina angalau chombo kimoja cha kimataifa cha kushughulikia hali – yaani, sera, mkakati au mpango – uliopo. Kati ya nchi 26 zisizo na chombo cha kitaifa cha kuweka mikakati, 10 hazionyeshi dalili yoyote ya kukuza mojawapo; saba kati ya nchi hizi ni nchi zilizoathiriwa na mizozo au nchi dhaifu na zitahitaji usaidizi muhimu kutegemea hali iwapo mfumo wa UAE wa lengo la Kustahimili Tabianchi Duniani kuhusu kuweka mikakati litafikiwa kufikia mwaka wa 2030. Pia, uwezekano wa ufanisi wa mipango ya kitaifa ya kukabiliana na hali (NAPs) kutoka kwa nchi zinazoendelea umechanganyika na unaonyesha umuhimu wa kujitolea kwa dhati kuhakikisha mipango ya kukabiliana na hali itapelekea hatua muhimu katika miktadha hii.
Juhudi za kukabiliana na hali zinaendelekea kuongozeka kwa jumla, lakini hazirandani na ukubwa wa changamoto. Kwa kuongezea, tathmini za miradi ya kukabiliana na hali iliyotekelezwa na msaada kutoka taasisi za kutoa ufadhili chini ya Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) zinaonyesha kuwa takriban nusu yake sio ya kuridhisha au haiwezekani kuwa endelevu bila fedha za mradi kwa muda mrefu. Nchi zinaripoti hatua zilizopiga za utekelezaji wa NAPs zao, lakini ziligundua kuwa kiwango na kasi ya kukabiliana na hali hiyo haitoshi kwa kuzingatia hatari za tabianchi zinazoongezeka. Kwa ujumla, juhudi zaidi zitahitajika ili kufikia lengo la utekelezaji la kimataifa la Mfumo wa Kustahimili Tabianchi Duniani wa UAE.
Ongezeko la ufadhili
Kwa kuzingatia ukubwa wa changamoto, kuziba pengo la fedha za kukabiliana na hali pia kutahitaji mbinu bunifu ili kukusanya rasilimali za ziada za kifedha. Mambo wezeshi zaidi, mbinu mpya na asasi za kifedha ni muhimu ili kupata ufadhili wa kukabiliana na hali, kwa sekta ya umma na ya kibinafsi.
Mambo wezeshi kwa sekta ya umma ni pamoja na uundaji wa mifuko na vyombo vya ufadhili, kuweka bajeti ya kushughulikia tabianchi na kuiwekea malengo maalum, kuyajumuisha katika mipango ya maendeleo ya kitaifa na mifumo ya matumizi ya muda wa kati, na kuweka mikakati ya uwekezaji wa kukabiliana na hali. Haya yanaweza kuungwa mkono na mageuzi yanayopendekezwa kwa taasisi za fedha za kimataifa na benki za maendeleo za kimataifa.
Mambo wezeshi katika sekta ya kibinafsi ni pamoja na mbinu mpya na zana zinazolenga kuondoa hatari ya fedha za sekta binafsi kwa kutumia fedha za umma. Haya yanaweza kuungwa mkono na viimarishi na majukwa ya kukabiliana na hali.
Ufadhili wa ushugulikiaji wa hali pia unahitaji kuacha kukabiliana na matokeo, kuwa unaongezeka, na unaozingatia tu mradi kuanza kuwa unaokadiria zaidi, wa kimkakati na wa mabadiliko chanya, vinginevyo hautafikia kiwango au aina za ushughulikiaji wa hali zinazohitajika. Hata hivyo, hii inahitaji hatua katika maeneo ambayo ni vigumu kufadhiliwa: kuunga mkono hali hii, kuna haja ya kutumia ufadhili wa umma wa kimataifa uliopo kimkakati zaidi.
Kwa kuongezea, swali la nani analipia ukabilianaji wa hali pia halijashughulikiwa vya kutosha. Katika mifumo mingi ya ufadhili, gharama kuu za kukabiliana na hali hubebwa na nchi zinazoendelea; hali hii inaweza kusaidia kuziba pengo la kifedha, lakini hairandani na kanuni ya majukumu ya kawaida lakini majukumu yaliotofautishwa na uwezo wake mtawalia, au na kanuni ya mchafuzi kulipia.
Kujengea uwezo na teknolojia
Mbali na fedha, kuna umuhimu wa kuimarisha ujengeaji uwezo na uhamishaji wa teknolojia ili kuboresha ufanisi wa hatua za kukabiliana na hali - hali inayorandana na kuzingatia mbinu za utekelezaji katika COP29.
Kurejelea mahitaji ya uwezo na teknolojia kunapatikana kila mahali katika stakabadhi za UNFCCC, ikizingatia zaidi maji, chakula na kilimo. Hata hivyo, jitihada za kukidhi mahitaji haya mara nyingi haziratibiwi, ni ghali na za muda mfupi. Pia kuna ushahidi mdogo kwamba juhudi hizi zinanufaisha makundi yaliyotengwa na yalio na uwakilishi mdogo. Sababu kadhaa hupunguza ufanisi wa uhamishaji wa teknolojia. Miongoni mwa zilizoenea zaidi ni vikwazo vya kiuchumi na kifedha, kama vile gharama za juu za uwekezaji wa kwanza, ugumu wa kupata mikopo, na mifumo ya kisheria na ya kutunga sheria inayohitaji sera za ndani kuiunga mkono.
Ripoti hii inatoa mapendekezo ya uboreshaji wa hali hii:
- Juhudi za kushughulikia hali zinapaswa kutumia uwezo uliopo, kutoa msisitizo sawia kwa teknolojia na hali wezeshi, na kutoa kipaumbele kwa usawa wa kijinsia na masuala ya ujumuishaji wa jamii.
- Ushahidi thabiti zaidi unahitajika, ikijumuisha ushahidi kutoka kwa ufuatiliaji na tathmini ya mahitaji ya uwezo na teknolojia, itakayoshughulikia kazi na na gharama zake halisi.
- Kujenga uwezo na uhamishaji wa teknolojia vinapaswa kuunga mkono ukabilianaji wa hali katika sekta mbalimbali, viwango mbalimbali na vipaumbele vya maendeleo.
- Mikakati ya kukabiliana na hali inapaswa kukuzwa kwa kuzingatia uelewa kamili wa mahitaji badala ya kutoka kwa mtazamo wa kusukuma teknolojia fulani, na kuifanya kuwa sehemu ya mikakati mipana ya maendeleo.
MAKALA KWA WAHARIRI
Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)
UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Kitengo cha Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa