Siku ya Wanyamapori Duniani (Tarehe 3 mwezi wa Machi) ni siku ya kujivunia viumbe vyote. Kauli mbiu ya mwaka huu, "Kuwezesha kila kiumbe kuishi duniani", inapongeza dunia yetu asilia kwa kuwezesha wanyamapori, mimea na watu kuishi kwa amani.
Mojawapo ya vitu muhimu duniani ni matumbawe. Matumbawe hutoa makaazi kwa aina nyingi ya viumbe baharini. Yanaweza kuchukuliwa kama misitu ya mvua inayopatikana chini ya maji —iliyosheheni viumbe hai na vile visivyoishi, na kwa pamoja, ni mojawapo wa mifumo ya ekolojia ya kipekee iliyo na umuhimu wake mkubwa.
Na je, unafahamu kuwa matumbawe ni muhimu kwa maisha yetu kwenye aridhi kama ilivyo kwa viumbe wanaoishi majini?
Hapa kuna vitu saba vinavyokuunganisha na matumbawe:
- Chakula
Takribani watu nusu bilioni kote duniani hutegemea samaki ambao hutegemea matumbawe kupata chakula. Hata kama unaishi mbali na pwani, kuna uwezekano mkubwa kuwa samaki unaowala walipatikana kutokana na matumbawe. Zaidi ya aina 4,000 ya samaki hutegemea matumbawe, na takribani tani 15 ya samaki zinaweza kuzaliwa na matumbawe mazuri katika eneo la kilomita mraba.
- Mapato
Matumbawe huvutia watalii katika maeneo yanayopatikana. Mamilioni ya wapiga mbizi wanaotumia neli ya hewa ya mzamia na wazamiaji wa kutumia vifaa vya kuvutia hewa hufurika kuona urembo wake kila mwaka. Pia, wasafari wengi hupendezwa na vukwe ambazo matumbawe yametunzwa. Utalii wa aina hii hutoa kipato kutokana na maboti ya wazamiaji na vituo vya utoaji wa huduma kama vile hoteli na mikahawa.
- Ulinzi
Matumbawe hukabilina na dhoruba na mawimbi yanaweza kusabasisha mmomonyoko katika maeneo ya pwani na kuharibu mali au hata kuhatarisha maisha. Hii ni kutokana na umbo lake na 'kuta' yanayojenga chini ya maji yanasaidia kupunguza kasi ya mawimbi. Ulinzi unaotolewa na matumbawe una umuhimu kwa sababu mabadiliko ya tabianchi yana uwezo wa kuongeza kasi na kiwango cha dhoruba kutokea.
- Dawa
Aina mpya ta dawa na virutubishi vya kiafya vinaundwa kutokana na kemikali zinazopatikana kwa aina ya vitu vinavyoishi kwa matumbawe. Ijapokuwa wanasayansi wamekuwa wakifanya hivi kwa misitu, ni hivi majuzi tu ndipo tulipoanza kuchunguza hali za matumbawe. Inamaanisha kuwa kuna uwezekano ndiyo tunaanza kung'amua kuwa dawa nzuri mno zinaweza kutoka kwa matumbawe!
- Utamaduni
Kwa watu wanaoishi maeneo ya pwani ambapo matumbawe hukua, na kwa watu ambo hupiga mbizi na kuona urembo kutokana na rangi mbalimbali na vitu vinavyoishi chini ya maji, matumbawe yana thamani kuliko pesa. Kwa kuongezea, mbali na kutupa huduma na vitu tulivyovitaja hapo juu, ni viwakilishi vya kipekee vya hali changamano na umaridadi wa maisha kwenye sayari yetu. Iwapo umewahi kuona matumbawe, utahisi kuwa kuwepo kwake duniani ni suala la kuvutia.
- Kuchuja maji
Matumbawe yanaweza kusaidia kusafisha maji. Aina nyingi ya matumbawe na sifongo ni vichujio, kumaanisha hukabiliana na chembechembe (vichafuzi ambavyo haviyeyuki majini) majini. Hali hii huzuia chembechembe hizi kuzama baharini na kuichafua kupitia vitu hatari. Mara ingine utakapoingia baharini, usisahau kushukuru matumbawe kwa kusaidia kusafisha
- Fukwe
Huwa inadhaniwa kuwa mchanga unaopatikana fukweni unatokana na makombe yaliyovunjika, lakini matumbawe pia husaidia kuunda fukwe zetu. Hakika, mchanga mwingi unaopatikana katika fukwe nyingi, ni zao la matumbawe yaliyovunjikavunjika. Kwa kuongezea, baadhi ya viumbe wanaoishi katika matumbawe huunda mchanga wanapokula matumbawe. Kwa mfano, pono mnono huweza kuzalisha tani moja ya mchanga kwa mwaka!
Matumbawe ni tofauti na mfumo wa ekolojia uwao wowote ule duniani. Mbali na kutoa uhai kwa wanyama na mimea mbalimbali, matumbawe hutupa rasimali isiyo na kifani na kuimarisha kiwango chetu cha maisha.
Kujifahamisha zaidi jinsi ya kutunza matumbawe, bonyeza hapa Reef Riders Journey, mchezo unaokuwezesha kutambua jinsi matendo ya kila siku ya viumbe husaidia kuimarisha mifumo iliyo hatarini ya ekolojia.