Wakati Zipporah Matumbi alipokuwa anakua, alipendezwa na jinsi misitu ya kijijini mwake kinachopatikana Mashariki mwa Kenya ilivyokuwa imejaa miti. Kwa sasa alivyo mtu mzima aligundua kuwa kutokana na kiwango kikubwa cha ukataji wa miti, misitu iliendelea kupungua. Kwa hivyo, aliamua kukusanya wanawake ili kuanza kupanda miche kwa kutumia hela zao wenyewe na kwa kutumia mda wao wenyewe na nia ya kuokoa misitu na kuleta mabadiliko.
"Tulitaka watoto wetu wakulie kwa mazingira mazuri," anasema. "Tuliona jinsi ambavyo maji yalivyopungua mitoni na tukataka maji yaongezeke kwa kuondoa mikatarusi inayotumia maji mengi na kupanda mianzi yenye asili ya Afrika."
Matumbi alishiriki katika Mradi wa UPandaji wa Miti ili Kuboresha Maisha, mradi ambao hupanda miti ya kiasili ili kuhifadhi misitu inayodidimia. Ijapokuwa majina yanakaribiana, ni tofauti na Mradi wa Ukuzaji wa Miti ili Kuboresha Maisha, ambao unahusu upandaji wa miti ya kigeni.
Idadi ya wanawake wa kujitolea wa kikundi cha Matumbi huongezeka jinsi miaka inavyoendelea kusonga mbele; kwa sasa, anasimamia vikundi mbalimbali 12. Kwa kipindi hicho, amegundua kuwa kuna chamgamoto ya kukuza misitu ya kiasili kutokana na vichaka vya miti haribifu iliyotoka kwenye maeneo ya tropiki za Marekani inayotambulika kama lantana camara.
"Lantana camara huwa na maua ya kupendeza, lakini mmea huu ni hatari mno na husababisha madhara katika nchi nyingi za tropiki, kuangamiza mimea ya kiasili na hata pia kufanya misitu kuwa na uwezekano mkubwa wa kudhuriwa na mioto wakati wa kiangazi," anasema Lera Miles, Mtaalamu Mkuu wa Masuala ya Kiufundi wa Mabadiliko ya Tabianchi na Bayoanuai wa Kituo cha Ufuatiliaji na Utunzaji wa Dunia cha Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.
Pia, huathiri wakulima wadogowadogo, majani ya mifugo na maeneo ya njia.
Kwa hivyo Matumbi na kikundi chake walianza kujitolea bila malipo kusaidia Shirika la Misitu la Kenya kung'oa lantana hiyo ili kuizuia kumea tena na kuandaa eneo hilo na kulihifadhi kwa kutumia miti ya kiasili. Miti ya kiasili haikui harakaharaka, lakini ikipata nafasi ya kutosha na ikipogolewa vizuri, inaweza kufanya vizuri.
Matumbi alifahamu fika kuwa kupanda tu miti ili kuwa na misitu haitoshi, kwa hivyo, yeye kuwahimiza wenzake kung'oa lantana na kupanda miti katika mashamba yao. Kupogoa miti hiyo ili kupata kuni huboresha misitu kwa kiasi fulani. Pia, kwa kulisha mifugo mihindi, matawi kutoka vichakani na matawi mengineyo, husaidia kutunza miti kwa sababu mifugo hawatahitaji kuchungwa misituni. Yeye pia hualika wataalamu kutoa mafunzo kwa kikundi chake ya jinsi ya kutumia njia mbadala kujipatia riziki kama vile kuweka nyuki, kushona vikapu ili kuwafanya wasitegemee mno misitu.
"Maisha ya jamii za kiasili huathariwa na aina za mimea hatari ambayo pia huathiri mazingira hasa mfumo wa usambasaji wa maji," anasema Max Zieren, mtaalamu wa UNEP aliye na ujuzi wa zaidi ya miaka 30 katika masuala ya kutunza mazingira, kukuza jamii na kuboresha misitu. "Miradi ya jamii kama ule unaoongozwa na Matumbi inaonyesha fursa zilizopo kwa ushirikiano na serikali ili kukabiliana na kusambaa kwa mimea haribifu-hali inayopelekea kuboresha kwa mashamba yaliyoharibika kama sehemu ya Muongo wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia."
Matumbi anasema anafanya kazi kwa idhini iliyotolewa kwa hiari kupitia mradi waShirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) unaojulikana kama Programu ya UN-REDD, ili kutetea haki za watu wa kikundi chake wanaofanya kazi bila malipo kupitia kwa Muungano wa Kitaifa wa Jamii za Maeneo ya misitu Nchini Kenya. Kikundi hiki kinamsaidia kufanya mashauriano na wameshaandaa mswada wa sera ya kutumika.
Kwa sasa, wanaendelea kufanya kazi bila kuchoka "ili kuwa na mazingira bora yatayopelekea wahusika wote kunufaika."
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ingrid Dierckxsens.