Kwa mjibu wa ripoti hiyo, kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kutapunguza athari na gharama zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi. Kufikia lengo la nyuzijoto 2 kama inavyohitajika chini ya Mkataba wa Paris kunaweza kupunguza hasara kwa mwaka kufikia asilimia 1.6, ikilinganishwa na asilimia 2.2 itayowezesha kufikia nyuzijoto 3. Ijapokuwa janga la COVID-19 linatarajiwa kuathiri uwezo wa nchi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuwekeza kwenye ushughulikiaji wa mabadiliko ya tabianchi kutegemea na eneo ni uamuzi utakakuwa na manufaa kwa uchumi.