Tarehe 15 mwezi wa Septemba mwaka wa 2020, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula (FAO) walizindua mkakati utakaoongoza utekelezaji wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia.
Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia 2021-2030, unaoongozwa na UNEP, FAO na wabia unajumuisha ekolojia ya maeneo ya nchi kavu maeneo ya pwani na maeneo ya bahari. Ni wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua, itajumuisha msaada kutoka kwa wanasiasa na wafadhili ili kuimarisha uboreshaji.
Jiunge nasi ili kujenga #GenerationRestoration.