“Kukua kunakotegemea kuchimba kutoka kwa sayari – na watu wetu – kuna gharama yake,” asema Balozi wa Nia Njema wa UNEP, Don Cheadle, anaposimulia kuhusu historia kuhusu chanzo cha mabadiliko ya tabianchi na jinsi ambavyo kila mtu anavyoweza kutazamia mustakabli kwa matumaini.
Video hii ni sehemu ya mradi wa TED Countdown initiative, unaoleta pamoja mtandao wa waleta mabadiliko ili kufanyia kazi mawazo ya kushughulikia mazingira.
Kwa ushirikiano na Mradi wa Masuluhisho (TSP), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linafanya kazi ili kuboresha uhamasishaji na juhudi zilizopo za masuluhisho yanayotegemea eneo kwa kuzingatia haki ya mazingira katika eneo la Amerika ya Kaskazini.
TSP ni shirika lisilokuwa la serikali linalokuza haki ya mazingira kupitia kwa kutoa ufadhili na kuzungumia hadithi za viongozi walio mstari mbele katika jamii kwenye vyombo vya habari. Wanalenga kuimarisha mabadiliko ya asilimia 100 yatakayowezesha matumizi ya nishati isiyochafua mazingira na kuwezesha upatikanaji bila ubaguzi wa hewa safi, maji safi na mchanga mzuri kwa kuunga mkono mashirika yanayofanyia mazingira haki, hasa yanayoongozwa na wanawake weusi.