Mfumo wa Kimataifa kuhusu Kemikali - wa Kuwa na Sayari Isiyodhuriwa ya Kemikali na Taka (GFC), ni nguzo muhimu kwa mustakabali ambapo binadamu watanufaika kutokana na kemikali kwa njia salama na endelevu, huku wakiepuka athari zake mbaya.
Mfumo huu, uliopitishwa Septemba mwaka wa 2023 katika Kongamano la tano la Kimataifa kuhusu Ushughulikiaji wa Kemikali (ICCM5), unalenga kutunza sayari na afya ya binadamu, kupigania mifumo thabiti ya utawala na kutekeleza viwango vya kimataifa.
Mfumo huu unawasilisha mpango wa kina ulio na malengo matano ya kimkakati na shabaha 28 za kuongoza nchi na washikadau kushughulikia kwa pamoja mzunguko wa kemikali, ikijumuisha bidhaa na taka.
Mkataba huu wa kipekee wa wadau mbalimbali unaleta pamoja sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa serikali, sekta ya kibinafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika kati ya serikali mbalimbali, vijana na wasomi.
Unaungwa mkono na Azimio la Bonn, azimio la ngazi ya juu pia lililokubaliwa katika ICCM5 mjini Bonn, nchini Ujerumani.
Mambo mapya ni yepi?
Awamu ya kwanza ya kutuma maombi ya Mfumo wa Kimataifa kuhusu Kemikali ilizinduliwa tarehe 1 Oktoba mwaka wa 2024. Waotuma maombi wanaweza kuyatuma hadi tarehe 31 Januari mwaka wa 2025. Pata maelezo zaidi kuhusu Mfuko huu na jinsi ya kutuma maombi au kuchangia.
Je, washikadau wanavyowezaje kushiriki?
- Jiunge na hafla ya uzinduzi wa Mfuko huu katika Jamii ya wataalam tarehe 4 Oktoba 2024.
- Jiunge na mkutano wa tatu ulio wazi kwa kila mtu wa kikundi kazi cha muda kuhusu vipimo na viashirio tarehe 13 Novemba 2024.
Pata maelezo zaidi kuhusu mikutano na matukio ya hivi punde zaidi ya Mfumo wa Kimataifa kuhusu Kemikali:
Wasiliana nasi
tuma baruapepe kwa: unep-gfc.secretariat@un.org