Kwa kuwa kwa sasa mfumo huu umepitishwa, kuimarisha hatua katika sekta mbalimbali na katika jamii ili kufikia malengo na shabaha za GBF ni muhimu kushughulikia vyanzo vikuu vya uharibifu wa bayoanuai na kupika jeki ajenda ya mazingira.
Malengo makuu manne yanayohitaji kufikiwa kufikia mwaka wa 2050 yanazingatia ubora wa mifumo ya ekolojia na afya ya viumbe ikijumuisha kuangamia kwa spishi kutokana na shughuli za binadamu, matumizi endelevu ya bayoanuai, mgao sawa wa faida, na kuhusu utekelezaji na ufadili kujumuisha kuziba pengo la ufadhili wa bayoanuai la dola bilioni 700 kila mwaka.
Miongoni mwa malengo ishirini na tatu yanayopaswa kufikiwa kufikia mwaka wa 2030 ni pamoja na asilimia 30 ya uhifadhi wa ardhi na bahari, asilimia 30 ya ureshaji wa mifumo ya ekolojia iliyoharibiwa, kupunguza kwa nusu kuanzishwa kwa spishi vamizi, na kupunguza dola bilioni 500 kwa mwaka kwa ruzuku inayodhuru.