Uchafuzi unahatarisha mifumo ya ekolojia na afya ya binadamu, iwe ni kupitia kwa kwa uchafuzi wa hewa, udongo na maji, au kwa kukumbana na kemikali hatari.
Kemikali na taka ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, lakini zisiposhughulikiwa ipasavyo zinaweza kusababisha matatizo ya kiafya kwa binadamu na uharibifu wa mazingira.
Kufikia mwaka wa 2025, miji duniani itazalisha tani bilioni 2.2 za taka kila mwaka, zaidi ya mara tatu ya kiwango kilichozalishwa katika mwaka wa 2009.
UNEP inakuza mbinu za pamoja zinazoonyesha manufaa ya kiuchumi, kimazingira na kiafya za kemikali na ushughulikiaji mwafaka wa kemikali na taka.
Lengo letu ni kuhimiza sera na uwekezaji unaopunguza hatari za kemikali kwa afya na kwa mazingira.
Nchi zinashughulikia kikamilifu changamoto zinazohusiana na uchafuzi wa hewa, udongo na maji, pamoja na kukumbana na kemikali hatari, kupitia Makubaliano ya Kimataifa ya Mazingira.
UNEP inatekeleza wajibu wajibu muhimu wa kuunga mkono ushirikiano wa nyanja mbalimbali ili kukuza mikakati na hatua za kutekeleza Mfumo wa Kimataifa kuhusu Kemikali uliopitishwa hivi karibuni.
Our work on chemicals and pollution action supports multilateral environmental agreements and is carried out through public-private partnerships.
The work of UNEP on chemicals and pollution action is led by the Industry and Economy Division.